BAADA ya vurugu na maandamano na kuchomwa moto baadhi ya makanisa zilizosababishwa na Kikundi cha Uamsho,Serikali imetakiwa kuunda tume ya kukichunguza kikundi hicho chenye mwuelekeo kama Al-Shabab cha nchini Somalia.
Kauli hiyo ilitolewa na
Mkurugenzi wa Taasisi ya Kiislam (TIPF), Sadiq Godigodi, wakishirikiana
na mwanaharakati Chifu Msopa jijini Dar es Salaam jana kuwa wanalaani
vugurugu zote zilizosababishwa na kikundi hicho.
"Watanzania tunapaswa kuwa
makini na Kikundi hiki kwani sisi tukiwa Waislam tunaifahamu vizuri
historia ya Al-Shabab ilivyoaanza kwani walianza kama hivi sasa hatutaki
kuingiza nchi hii katika matatizo ya kuuwana kama ilivyotokea nchini
Rwanda 1994"alisema Godigodi.
Alisema wanaitaka serikali
kukichunguza kikundi hicho kwa kuwa kinakwenda kinyume na malengo yake,
kwani kilianzishwa kwa ajili ya kufanya mihadhara, kueleimisha, maadili
ya dini, kufanya ibada na mambo yote anayohitaji Mungu (Alla SW).
Aidha, wanalaani vurugu
zote zilizosababishwa na baadhi ya watu wa Uamsho kwa kusema makanisa
hayakutendewa haki hata kidogo kwa kuwa kanisa si serikali wala Tume ya
Uchaguzi au Chama cha siasa.
Godigodi alikwenda mbali
kwa kusema wanawalani wale wote wanaopinga muungano kwani hata Mwenyezi
Mungu anawachukia wote wanaotaka kujitenga au kufanya ubaguzi wa aina
yeyote ya Dini, Kabila au rangi, kwani Mwenyezi Mungu aliwawakea
misingi ya kuheshimu dini za watu wengine na wale wasiokuwa na dini.
Godigod alisema Waislama
wanakishangaa kikundi hicho kwa kufanya mihadhara ya kuleta chuki kwa
baadhi ya Waislama wa Zanzibar kama vile kupinga muungano wa Zanzibar na
Tanganyika wakati kuna utaratibu umewekwa wa kutoa maoni kuhusu suala
hilo.
Vile vile kuwakataa baadhi
ya watu kutoka Bara wanaoishi kuondoka Visiwani humo kama walivyosoma
katika vyombo vya habari (huu ni ubaguzi), na kupinga utoaji wa maoni
kuhusu mchakato wa Katiba mpya.
Hata hivyo, alisema
Zanzibar ni Kisiwa chenye idadi kubwa ya waislam na vyama vikubwa vyenye
idadi kubwa ya wanachama ambapo vyama hivyo vina ushawishi kwa wananchi
mbalimbali.
Alisema baada ya muafaka
wa CCM na CUF Wazanzibar wamekuwa kitu kimoja wakishirikiana kwa kila
jambo ni dhahiri kwamba kila Mzanzibari anhitaji maisha ya umoja na
ushirikiano.
Hata hivyo kuna taarifa kuwa Serikali ya Mapinzi Zanzibar imesimamisha shughuli zote za Kikundi hicho cha Uamsho.
No comments:
Post a Comment