Thursday, June 27, 2013

Bugabo Bukoba Vijijini Maisha yanaendelea

MAMBO YA WAZIRI MKUU

 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Bw. Lars Christian Rais Mtendaji wa STATOIL kampuni ambayo imegundaua gesi katika maji ya bahari yenye kina kirefu katika eneo la Mtwara, bungeni mjini Dodoma Juni 27, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia kwa Nchi za Tanzania, Burundi na Uganda, Ofisini kwake bungeni ini dodoma Juni 27,2013.  (Picha na

Maisha,,,,,,,,,,,,,,,,,,

untitled3 1d8e4

Magazeti


DSC 0062 182df
DSC 0063 855f0
DSC 0064 13dba
DSC 0065 fc1e7
DSC 0066 8089a
DSC 0067 12814
DSC 0068 3f083


DSC 0069 f2646
DSC 0070 73b4c
DSC 0071 8d03b
DSC 0072 23bbb
DSC 0073 2b9d4
DSC 0074 5a769
DSC 0075 8ce12
DSC 0076 cf808
DSC 0077 11466
DSC 0078 b69d3
DSC 0079 dfe20


Rais Obama anaelekea Afrika Kusini

senegal 94b3a
RAIS wa Marekani Barack Obama leo Ijumaa anaelekea Afrika Kusini ambapo miongoni mwa shughuli zake atazuru kisiwa cha Robben Island  alikozuiliwa jela rais wa zamani Nelson Mandela kwa miaka 27.
Rais Obama anakwenda nchini humo wakati Mandela akiwa katika hali mbaya ya afya. Rais huyo wa zamani anatibiwa katika hospitali moja ya Pretoria.  
Alihamis rais Obama alisema ziara yake katika eneo ambalo watumwa wa Afrika waliondoka barani humo kwenda Amerika kaskazini imempa hamasa mpya ya kulinda haki za binadamu.
Obama alitembelea kisiwa cha Goree kwenye ufukwe wa Senegal Alhamis.   Wanahistoria wanasema maelfu ya Waafrika wanaume kwa wanawake wakiwa wamefungwa minyororo walishikiliwa huko na kupitia kile kilichoitwa mlango wa kutorudi tena kupanda meli ya watumwa wakielekea bahari ya Atlantic.  
Rais Obama alisema ziara yake katika kisiwa hicho ilimpa hisia kali na nafasi ya kutathmini upya biashara ya utumwa katika karne ya 16 na 19. Chanzo: Voaswahili

BILAL AFUNGA MAFUNZO YA UOFISA NA UKAGUZI MSAIDIZI

untitled4 c5693
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifunga rasmi mafunzo ya Uofisa na Ukaguzi Msaidizi wa Chuo cha Polisi cha Dar es Salaam, leo Juni 27, 2013 kwenye hafla hiyo iliyofanyika katika Chuo hicho kilichopo Kurasini jijini Dar es Salaam. Picha na OMR

untitled5 11ef8
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimvisha Cheo cha Heshima, Mhitimu wa Mafunzo ya Uofisa na Ukaguzi Msaidizi wa Chuo cha Polisi cha Dar es Salaam, S/SGT Juma Sadiki Bahati, wakati wa hafla ya kufunga mafunzo hayo iliyofanyika leo Juni 27, 2013 chuoni hapo jijini Dar es Salaam


untitled6 e40c9
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti Cheo cha Heshima, Mhitimu wa Mafunzo ya Uofisa na Ukaguzi Msaidizi wa Chuo cha Polisi cha Dar es Salaam, Akama Mohamed Shaaban, wakati wa hafla ya kufunga mafunzo hayo iliyofanyika leo Juni 27, 2013 chuoni hapo jijini Dar es Salaam

Tuesday, June 25, 2013

MWENYEKITI UVCCM TAIFA: SIAFIKI SERIKALI MFUMO WA SERIKALI TATU


MWENYEKITI UVCCM TAIFA
ARUSHA, Tanzania

MWENYEKITI wa Umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi Taifa (UVCCM), Sadifa Juma Hamisi, amepinga vikali kuwepo kwa mfumo wa serikali tatu kama inavyopendekezwa katika rasimu ya katiba.

Sadifa ameyasema hayo wakati akizungumza na wanachama wasomi wa UVCCM kutoka katika vyuo vikuu mkoani kilimanjaro katika hafla ya kuwaaga wasomi hao na ambapo pia ametunuku vyeti vya uanachama kwa wanafunzi 312 pamoja na kuwakabidhi kadi za uanachama wanachama wapya.


Mwenyekiti huyo ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Donge (CCM) zanzibar, amesema uwepo mfumo wa serikali tatu ni mzigo mkubwa kwani kutokana na uduni wa uchumi wan chi yetu itakuwa vigumu kuendesha serikali tatu kwa maana ya serikali ya Zanzibar, serikali ya Tanzania bara na ule wa muungano.

“Jamani tusidanganyane, kuendesha serikali tatu ni mzigo, kwa uduni wa uchumi wetu sidhani kama itakuwa rahisi kuendesha serikali tatu, kama kutakuwa na serikali tatu kuna hatari ya kuvunjika kwa muungano wetu huu maana uwezo kuchangia hatuna, tutajiingiza kwenye matatizo makubwa, vijana tuwe makini na tutumie taaluma zetu kuhimiza umuhimu wa kuwepo kwa muungano huu wa sasa,"


Aidha Sadifa amewahimiza vijana kuwa mfano mzuri kwa jamii huku akiwahimiza kuwa waadilifu, wazalendo, kujiamini na kuwa na nidhamu hali ambayo itasaidia kuwepo kwa amani na usalama wa nchi.Amesema bila amani na muungano wa wananchi maendeleo hayawezi kupatikana katika nchi ambpo aliwataka vijana kuwa mtari wa mbele kuwaelimisha wananchi wa kawaida juu ya umuhimu wa kuenzi, kudumisha na kuimarisha muungano wa zanzibar na Tanganyika  kama njia pekee ya kuhakikisha nchi inakuwa na amani siku zote.

“Vijana tuna wajibu kubwa wa kuwaenzi waliotuletea muungano wetu wa sasa, taaluma zetu ziwe dira ya jamii katika kuenzi, kudumisha na kuimarisha muungano wetu kwani ndio njia pekee ya kusaidia kudumisha amani na usalama wan chi yetu, tuepuke kujiingiza katika mkumbo wa wale wanaodai nchi haitatawalika,” amesemaHata hivyo Sadifa amewataka vijana kutodanganyika na vyama vinavyoeneza chuki na maandamano yasiyokuwa na msingi wowote huku akifafanua kuwa kisheria kuandamana na haki ya msingi lakini ifuate sheria na yassingilie haki za wengine.

“Chama pekee katika nchi hii ni CCM, kuna vyama vingine vimeanzishwa ambavyo mimi binafsi naviita ‘Saccos’, hauwezi ukajikopesha fedha kienyejienyeji kama alivyofanya Dk. Slaa! Vijana tuwe makini na saccos hizi ambazo ajenda zao ni kukopeshana na vurugu tu,” amesema Sadifa

Kwa upande wake mwenyekiti wa shirikisho la wanafunzi wa vyuo vikuu wanachama wa CCM kilimanjaro, Wakati Mtulya akizungumzia changamoto wanazokumbana nazo, alisema kumekuwa na urasimu ndani ya bodi ya mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu, ambapo mikopo imekuwa ikitolewa kwa watu wasiostahili huku walengwa wakiendelea kutaabika.

Amesema kuwa kumekuwa na mchezo ndani ya bodi hiyo, ambapo mikopo imekuwa ikitolewa kwa watoto wa matajiri huku wastahili ‘watoto wa wakulima’ wakibaki kuzungushwa na kuwekewa masharti magumu ya kupata mikopo hiyo jambo ambalo limekuwa likichangia kuwepo kwa vitendo vibaya miongoni mwa wanafunzi hao.

“Mikopo ni yetu, sio ruzuku, lazima tukopeshwe kwa wakati kwani lazima tutairudisha lakini jambo la kusikitisha, bodi hii imekuwa ikitoa mikopo kwa watoto wa masaki, huku sisi watoto wea mkulima tukiendelea kuzungushwa na kuwekewa masharti magumu ili kupata mikopo hiyo, hili ni tatizo,” amesema Mtulya (habari na TAIFA LETU.com).

Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Sadifa Juma Hamisi (katikati) akiwa na mwenyekiti wa UVCCM kilimanjaro, Fredrick Mushi (kulia) na Kaimu Katibu wa CCM mkoa wa Kilimanjaro, Aluu Segamba katika Hafla ya kutunuku Vyeti kwa wanachama wa UVCCM vyuo vikuu Kilimanjaro.

Mwenyekiti wa UVCCM Kilimanjaro akiongoza maandamano kuelekea katika ukumbi wa CCM mkoa ambapo ndipo ilikofanyikia mkutano mkubwa wa UVCCM jana
Viongozi waandamizi wa CCM mkoani Kilimanajro katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa

Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Sadifa Juma Hamisi Akipokea Maandamano ya Wanafunzi wa Vyuo vikuu Kilimanjaro ambao ni makada wa UVCCM mkoani Kilimanjaro
Katibu wa UVCCM manispaa ya Moshi, Bwana Makwaiya akisakata Rumba muda mfupi baada ya maandamano kuwasili katika makao makuu ya CCM mkoa wa kilimanjaro

Sadifa akikabidhi cheti cha unachama kwa mwanafunzi wa chuo kikuu muccobs jana, jumla ya wanavyuo 312 walipata vyeti vya uanachama wa UVCCM

Mwenyekiti wa shirikisho la Vyuo Vikuu mkoani Kilimanjaro, Wakati Mtulya

Sadifa (aliyevaa suti) akiongoza vijana kucheza kwaito katika ukumbi wa CCM mkoa wa Kilimanjaro

Soka La Bongo

                                   

Magazeti


DSC 0028 35a04
DSC 0029 17da2
DSC 0030 a9986
DSC 0031 82f07
DSC 0032 9cf89


DSC 0033 74e6c
DSC 0034 bdf2b
DSC 0035 43af4
DSC 0036 e497e
DSC 0037 5759e
DSC 0038 effa3
DSC 0039 79fdc
DSC 0040 a1003
DSC 0041 822fd
DSC 0042 42def
DSC 0043 95b9a