Tuesday, May 22, 2012

Wakuu Wa Wilaya Mkoani Kagera Kuyaweza Maagizo Ya Kanali Massawe?


Wakuu wa wilaya wapya wa mkoa wa Kagera wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Kagera mara baada ya kula kiapo wiki iliyopita.




Na Angela Sebastian
Bukoba
Mkuu wa mkoa wa Kagera Kanal mstaafu  Fabian Massawe amewaagiza wakuu wa Wilaya wapya kuhakikisha wanasimamia mapato na matumizi sambamba na miradi mbalimbali katika Halmashauri za Wilaya zao ili kuondoa ubadhirifu wa fedha za umma ambao umekuwa ukifanywa na baadhi ya watendajikatika Halmashauri hizo na Manispaa.
Alitoa wito huo wiki iliyopita wakati akiwaapisha wakuu wapya wa Wilaya saba za mkoa huu walioteuluiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete hivi karibuni.
Kanal Massawe alisema kuwa wakuu wa Wilaya wanakazi kubwa ya kusimamia mapato na matumizi ya Serikali na kuthibiti suala la ubadhilifu wa fedha ya umma ambao umekuwa ukifanywa na baadhi ya watenaji  wa Halmashauri  wasiokuwa wadilifu.
“Hii nitimu ya ushindi aliyoiteua mh.Rais na kuwa na imani nayo kwahiyo mnatakiwa kuonyesha imani hiyo kwa vitendo,kuweni na macho makali kama ya mwewe anavyomnyemelea kifaranga na kumnasa kuhakikisha mnasimamia kwa  karibu miradi mbalimbali ya Halmashauri zenu na Manispaa ikiwa ni pamoja na kusimamia mapato na matumizi na pale watakapobainika wafujaji wa pesa wachukuliwe hatua  na kufikishwa mahakamini wakati uchunguzi ukiendelea”alisema Massawe
“Hatuhitaji kuwasubiri wageni waje kubaini matatizo tulionayo wakati sisi tupo sitaki kuona mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali anakuja kugundua madudu ya ubadhilifu wakati sisi tupo tunachelea madudu hayo nataka hiyo iwe historia mkoani hapa, tufanye kazi kwa nguvu zote kwa usimamiazi wa karibu wa miradi, tukague miradi mbaliambali ya maendeleo ikiwa ni pamoja na barabara,vyumba vya madarasa na miradi mingine zinazojengwa kwa pesa ya umma kwani asilimia kubwa hazijengwi kwa viwango vinavyokusudiwa  kwa kulingana na pesa iliyotolewa”aliongeza Masawe.
Alisema kuwa Serikalia imekuwa ikitoa aasilimia 80 ya mapato yake katika Halmashauri kwa ajili ya kuhudumia wananchi lakini wananchi hawafaidiki na pesa hiyo bali wajanja hujichakachulia na kuwafanya wananchi kukosa maendeleo na kuichukia Serikalia yao kwa sabaua ya wachache wasio na maadili lazima tuwashughulikie kwa kasi kubwa .
Aliwataka wakuu hao wa Wilaya kuhakikisha wanahamasisha viongozi wa ngazin za chini yao kuanzia vitongoji na kata kuitisha vikao na mikutano ya wananchi ili waweze kuibua miradi ya maendeleo wao wenyewe ili kuondoa tatizo la kuwa miradi inayoletwa katika maeneo yao ni ya Serikali ambapo wakipata elimu wataweza kuibua wenyewe na kuimiliki bila kusema si yetu ni ya Serilakali ambapo alitoa mfano wa shulez akata ambazo hapo mwanzo wananchi walisema ni mali ya Serikali lakini wameelimishwa na kutambua kwamba ni mali yao na kuweza kuchangia bila tatizo.
Aidha aliwasihi wakuu hao kupamba na suala la magendo ya kahawa mabalo limeshamili katika mkoa huu kwani walanguzi hao hukosesha mapato Serikali.
Aliwataka kuhimiza wananchi kutunza  amani ambayo ni tuni ya Taifa hili na kukemea vitendo vya kujichukulia sheria mikononi ambavyo husababishwa imani za kishirikina ambayo ni kero na changamoto kubwa inayo ukabili mkoa wa Kagera na viongozi wake.
Pia amewataka kuhakikisha wanasimamia vyanzo vya maji na utunzaji wa mazingira na kama mtu akibainika anaharibu mazingira kwa kuchoma moto  au kujenga katika vyanzo vya maji na kufanya uharibifu wa aina yoyote  katika sula la mazingira achukuliwe hatua ikiwa ni sambamba na kufikishwa mahakamani kwa sheria ya uharibifu wa mazingira.
 
Aliwataka kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya zoezi la sense ya watu na makazi ambalo itafanyika mwezi Agost mwaka huu ili Serikali iweze kupata takwimu sahii ya watu inayowahudumia.
Akiongea kwa niaba ya wakuu hao wa Wilaya kanal mstaafu Suleman Njiku ambaye ni mkuu wa Wilaya ya Misenyi alisema kuwa  wameapa kuhakikisha wanafanya kazi kwa bidii na nguvu zao zote ili kuwaletea wananchii maendeleo ya kweli na si vinginevyo.
 
Wakuu wa wilaya walioapishwa ni Costantine kanyasu (Ngara),Richard Mbeho (Biharamulo),Dali Rwegasira (Karagwe),Zipora Pangani (Bukoba),Limbules Kipuyo (Muleba),Kanal mstaafu Issa Njiku (Missenyi) na Luten kanali mstaafu Benedict Kitenga (Wilaya mpya ya Kyerwa).
mwisho

No comments:

Post a Comment