Thursday, July 26, 2012

Waziri Wa Uchukuzi Dr Mwakyembe Azindua Huduma mpya Za Shirika La ndege La Qatar kutoka KIA




Mgeni rasmi katika uzinduzi huo,waziri wa mawasiliano na uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe akimkabidhi Mkurugenzi mtendaji wa masoko wa shirika hilo Bw. Marwan Koleilat  kwa niaba ya shirika hilo la ndege la Qatar zawadi ya picha yenye kivuli cha Mlima Kilimanjaro .
Mkurugenzi mtendaji wa masoko wa shirika la Qatar Bw. Marwan Koleilat  kwa niaba ya shirika hilo akimpa Mgeni rasmi katika uzinduzi huo,waziri wa mawasiliano na uchukuzi Dr. Harrison zawadi  ya yenye nembo ya ndege ya shirika hilo la Qatar.
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo,waziri wa mawasiliano na uchukuzi Dr. Harrison akizungumza mbele ya wageni waalikwa wakiwemo na wahariri wa habari kutoka vyombo mbalimbali (hawapo pichani),mapema leo kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa KIA.
Mkurugenzi mtendaji wa masoko wa shirika la Qatar Bw. Marwan Koleilat  kwa niaba ya shirika hilo akizungumza mbele ya wageni waalikwa wakiwemo na wahariri wa habari kutoka vyombo mbalimbali (hawapo pichani),mapema leo kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa KIA
Kutoka kulia ni Mkurugenzi mtendaji wa masoko wa shirika la Qatar Bw. Marwan Koleilat,Waziri wa Uchukuzi Dr.Harrison Mwakyembe,Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya KADCO, Balozi Hassan Omar Gumbo Kibelloh pamoja na Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki wakijadiliana jambo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya KADCO, Balozi Hassan Omar Gumbo Kibelloh lakizungumza machache na pia kumkaribisha mgeni rasmi na wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla hiyo mapema leo iliofanyika kwenye uwanja wa KIA.
 Wakuu wa uzinduzi wakipga makofi kwa pamoja mara baada ya uzinduzi huo.
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo,waziri wa mawasiliano na uchukuzi Dr. Harrison akipiga makofi wakati kikundi cha ngoma za asili kikitumbuiza,shoto kwake ni Mkurugenzi mtendaji wa masoko wa shirika la Qatar Bw. Marwan Koleilat
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya KADCO, Balozi Hassan Omar Gumbo Kibelloh akimkaribisha Mkurugenzi mtendaji wa masoko wa shirika la Qatar Bw. Marwan Koleilat mara baada ya kuwasili na ndege ya shirika hilo aina ya Ndege namba QR546,shoto kwake ni  Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya KADCO, Balozi Hassan Omar Gumbo Kibelloh akimpokea Mgeni rasmi,Waziri wa Uchukuzi Dr Harrison Mwakyembe mara baada ya kuwasili KIA tayari kwa uzinduzi
Mgeni rasmi,Waziri wa Uchukuzi Dr Harrison Mwakyembe akishuka kwenye ndege ya Qatar kwenye Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) akiwa ameambatana na Mkewe pamoja na  Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki.
 Ndege ya Qatar ikiwasili kabla ya kuzinduliwa rasmi KIA.
 Ikifanyiwa shower kwa mbwembwe zote.
 Wageni waalikwa mbali mbali wakisubiri kushuhudia uzinduzi huo.


Pichani kulia ni Mkuu wa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro Mhe.Novatus Makunga akizungumza jambo  na Mhariri Mkuu wa gazeti la Tanzania Daima,Bw.Absalom Kibanda.

Naibu Waziri Wa Uchukuzi Dkt. Charles Tizeba Afanya Ziara Bandari Ya Dar es Salaam

Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Charles Tizeba akifafanua jambo kwa uongozi wa Wizara, Bandari na Mkurugenzi Mtendaji wa Kitengo cha Kupakia na kupakua makontena TICTS, kulia kwa Naibu Waziri ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Bw. John Mngodo, Kushoto kwa Naibu Waziri ni Meneja Msaidizi wa Bandari ya Dar es Salaam, Bi Winnie Mulindwa, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo(aliyevaa tai ya blue), Mhandisi Omar Chambo, na Kulia kwa Katibu Mkuu ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Kupakua na Kupakia Makontena (TICTS), Bw. Neville Bisett.
Naibu Waziri wa Uchukuzi,Dkt. Charles Tizeba (Mb),akiongea na baadhi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania(hawapo pichani),wakati alipotembelea Taasisi hiyo leo jijini Dar es Salaam,Kushoto kwa Naibu Waziri ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Mhandisi Omar Chambo, Naibu katibu Mkuu wa Wizara hiyo (wa pili kushoto),Bw. John Mngodo. Na aliyevaa Kizibao ni Meneja Msaidizi wa Bandari ya Dar es Salaam,Bi. Winnie Mulindwa.
Meneja Msaidizi wa Bandari ya Dar es Salaam, Bi. Winnie Mulindwa, akitoa taarifa ya namna Bandari ya Dar es Salaam inavyofanya kazi kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Charles Tizeba (aliyeshika kichwa), ambaye amefanya ziara ya siku moja katika Bandari ya Dar es salaam. Kushoto kwa Naibu Waziri ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Omar Chambo, Kulia kwa Katibu Mkuu ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,Bw. John Mngodo, Kushoto kwa Meneja Bandari Msaidizi ni Mkurugenzi wa Idara ya Usalama na Mazingira kutoka Wizara ya Uchukuzi,Bi. Tumpe Mwaijande.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya kupakua na kupakia makontena Bandarini (TICTS), Bw. Neville Bisett akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Charles Tizeba (Mwenye Suti ya Mikono Mifupi),wakati alipofanya ziara ya siku moja kuangalia ufanisi wa Kampuni hiyo katika Bandari ya Dar es Salaam leo.Kulia kwa Naibu Waziri ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi,Bw. John Mngodo.(Picha Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi).

Happy Birthday Spika Makinda

Bi Lina Kitosi akimlisha Mhe. Spika keki kwa niaba ya Wafanyakazi wa Bunge wakati wa Birthday yake ya 63 iliyofanyika jana mjini Dodoma, Fullshangweblog inakutakia maisha marefu Mh. Spika Anne makinda na mungu akupe hekina na Busara ili uweze kuliongoza vyema bunge letu kwa maendeleo ya Tanzania
Ni Birthday ya 63 ya Mhe. Spika Anne Makinda, Mb.
  Keki ya Birthday

Mwanamke Shule...!Maisha Yanaendelea


Mansour Yusuf Himidi; Hata Nikivuliwa Uwanachama Wa CCM, Sitabadili Mawazo Yangu Kuhusu Muungano


Mweka Hazina wa Chama cha Mapinduzi kwa upande wa Zanzibar, Mansour Yusuf Himidi, amesema atasimamia mtazamo wake kuhusu muundo wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar unaofaa hata kama itapelekea kuvuliwa uwanachama.
 
 
Magazeti Magazeti 
::










Tuesday, July 24, 2012

Maisha Yanaendelea


Matukio Mbalimbali Mjini Bukoba


Hali hii inaonyesha kwa jinsi gani basi la Sumry ambalo hufanya safari zake kati ya miji ya Dar es salaam na Kagera linavyowapa usumbufu waendesha vyombo vya moto, katika hali ya kawaida basi la sumry uegeshwa katika eneo hili la ushahilini kwenye eneo ya barabara, eneo hili hutumiwa na wamiliki wa basi hili katika kupakia na kupakia abiria tofauti na mabasi mengine ambayo hufanya shughuli maeneo ya standi kuu ya mabasi, hali hii inawapa usumbufu mkubwa watumiaji wa barabara linapoegeshwa basi la Sumry, kama mnavyoona.



Maegesho yasiyo rasmi yaliyoko eneo la uswahilini lililoko katika manispaa ya Bukoba karibu na Q Bar yanayotumiwa na basi la Sumry ambayo sio rasmi.



Baadhi ya wajumbe wa kamati inayoratibu shughuli za kukusanya maoni yaa uundwaji wa katiba mpya, kamati hiyo kwa sasa inakusanya maoni katika manispaa ya Bukoba, hapa inakusanya maoni maeneo ya uwanja wa uhuru.



Waliojitokeza kutoa maoni wakiwa kwenye mstari wakijiandaa kuelezea mapendekezo yao.



Mmoja wa wakazi wa manispaa akitoa maoni.



Baadhi wya wakazi wa manispaa ya Bukoba wakisikiliza mapendekezo yaliyokuwa yakitolewa ya uundwaji wa katiba mpya ya jamhuri.

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII BALOZI KHAMIS KAGASHEKI AMALIZA ZIARA YA KUTANGAZA UTALII NCHINI MAREKANI


  1. Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Sued Kagasheki akimkabidhi tuzo ya kinyago Bi. Jena Fox, mwanahabari kutoka Jarida maarufu la nchini Marekani la Travel Agent Magazine jijini New York hivi karibuni. Tuzo hii ilitolewa na Bodi ya Utalii nchini kufuatia uandishi mzuri wa makala mbalimbali za kutangaza ukanda wa utalii wa kusini katika soko la Marekani 
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akiwafnya mahojiano na mwanahabari Jena Fox kutoka jarida la Travel Agent Magazine jijini New York hivi karibuni.Katika mahojiano hayo Balozi Kagasheki alipata fursa ya kuelezea furdsa mbalimbali za vivutio vya utalii nchini kwa soko la Marekani.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii nchini Dk. Sloyce Nzuki akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa Chama cha Mawakala wa Wageni cha Marekani (USTOA) Bi. Peggy Murphy mara baada ya kufanya nae mazungumzo juu ya namna ya kuongeza idadi ya wageni nchini kutoka Marekani jijini  New York hivi karibuni.

Magazeti Magazeti