Msanii wa filamu nchini Elizabeth
Michael a.k.a Lulu akiwa Mahakamani mapena leo wakati alipofika
kusikiliza mashtaka yake yanayomkabili kuhusiana na tuhuma za mauaji ya
msanii mwenzake,Marehemu Steven Kanumba Lulu akiwa mahakamani
hapo.Lulu akiwasili Mahakamani hapo.
Mahakama Kuu kanda ya
Dar es salaam imepanga kutatoa uamuzi juu ya umri wa msanii wa filamu
nchini Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu anayekabiliwa na kesi
ya mauaji ya msanii mwenzake Steven Kanumba Aprili 7 mwaka huu.
Jaji Fauz Twaib leo
alisikiliza mapingamizi ya mawakili wa serikali kuhusiana na maombi ya
mawakili wanaomtetea Lulu waliyowasilisha mahakamani hapo kuiomba korti
hiyo aidha ichunguze umri wa Lulu anayedai ana miaka 17 au iamuru
mahakama ya kisutu kuchunguza.
Baada ya kuwasilishwa
maombi hayo leo ilikuwa ni siku ya kusikilizwa maombi mahakamani
ambapo wakili Shadrack Kimaro wa Serikali alipinga vikali maombi hayo
kuwepo mahakamani hapo akidai kuwa hayakustahili kuwepo na badala yake
yatupwe.
Alidai walichofanya
ni kinyume cha sheria ilipaswa wakate rufaa kwasababu maombi
yalishafika mahakama ya kisutu inakosikilizwa kesi hiyo na kutolewa
maamuzi hivyo haikuwa sahihi kufungua maombi mapya wakati sio maombi
mapya.
Aliwashauri mawakili
wa Lulu aidha kukata rufaa maamuzi ya Kisutu au kuomba maamuzi yale
kufanyiwa mapitio. Hata hivyo alidai kifungu cha sheria kilichotumika
kuwasilisha maombi hayo sio sahihi ilipaswa kitumike kifungu ambacho
kitaipa mamlaka korti hiyo kusikiliza maombi.
Mawakili wa Lulu,
Furgence Masawe, Peter Kibatala na Kennedy Fungamtama hawakukubaliana
na hayo,ambapo Fungamtama aliiomba mahakama kupokea maombi yao na
kutolea uamuzi kwasababu ndiko maombi yao yanakotakiwa kupelekwa.
Aliusoma upya uamuzi
uliotolewa Kisutu na kudai kuwa haukuwa uamuzi bali maelekezo ya
mahakama na wao wamefata maamuzi hayo yaliyowataka kuwasilisha maombi
yoyote Mahakama Kuu kwasababu mahakama ile haina mamlaka ya kusikiliza
kesi ya mauaji.
Baada ya kusikiliza mabishano hayo ya kisheria mahakama hiyo imepanga kutoa maamuzi Juni 16 mwaka huu
No comments:
Post a Comment