Monday, April 29, 2013

Maisha Yanaendelea

03 9ea2a
Mafundi ujenzi wakiendelea na kazi, Hii ni Barabara ya Morogoro eneo la magomeni Jijini Dar es salaam.

DKT. BILAL AKUTANA NA NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE, UJUMBE MAALUM WA SYRIA


03 41812
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkaribisha Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria, Hussam A'ala, wakati akimkaribisha ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam
04 0a173
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria, Hussam A'ala, na ujumbe wake wakati alipofika Ofisini kwa Ikulu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mazungumzo
05 450ef
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi kutoka kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria, Hussam A'ala, baada ya mazungumzo

Godbless lema aachiwa huru kwa dhamana



lema ec6a0

Mbunge Arusha, Godbless Lema
Mahakama kuu ya Arusha mapema leo asubuhi imemuachia huru kwa dhamana mbunge  wa Arusha mjini,kwa mashariti ya kuwa na mdhamini mmoja mwenye kitambulisho, na asaini hati ya dhamana yenye thamani ya shilingi milioni moja.

Watu 30 wavamia, kuvunja nyumba

1 7d1c6
Zaidi ya watu 30 usiku wa kuamkia jana walivamia na kuivunja nyumba ya Yasinta Malisa, iliyopo Kunduchi Ununio ,kando ya Bahari ya Hindi, huku wakimtishia kwa bastola mlinzi wa nyumba hiyo.
Kutokana tukio hilo Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, amemtaka mmiliki wa nyumba hiyo kuwasilisha vielelezo vya umiliki wa eneo hilo polisi.

Hatua hiyo inalenga katika kuwawezesha polisi kuvipitia na kumpa ushauri wa ama kwenda mahakamani au kumkamata anayeshukiwa kubomoa nyumba hiyo.
"Wanatakiwa kuwasilisha vilelezo vya umiliki wa eneo hilo, lakini pia inaonyesha kuwa kuna mgogoro katika eneo husika. Vielelezo ndivyo vitaonyesha kila kitu na tutajua wapi kuna tatizo," alisema Kenyela.
Mmoja wa walinzi wa nyumba hiyo, Saitoti Nang'oro na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Ununio, Iddi Musa, walisema watu hao walivamia mtaa huo saa 9 usiku wakiwa na marungu, mapanga na bastola.
Akizungumzia na gazeti hili, Yasinta alisema baada ya kufiwa na mume wake mwaka jana, aliamua kuendeleza ujenzi wa nyumba hiyo, lakini siku tatu baada ya kuanza kazi, watu hao walivamia na kuivunja nyumba yake.
"Hili eneo tulilinunua kutoka kwa wazawa wa hapa Ununio na nina vilelezo halali, ila nashangaa kitendo kilichofanyika tena kimefanyika usiku, sasa kama wanamiliki eneo kihahali kwa nini waje usiku, mbona hakuna hata vilelelezo vyao katika ofisi za Serikali ya mtaa," alihoji.
Alisema alinunua eneo hilo miaka 20 iliyopita, huku akisisitiza kuwa eneo hilo halijapimwa na Serikali na wamiliki wake wanauza maeneo yao kama mashamba. Akisimulia alivyonusurika kuuawa Nang'oro alisema akiwa lindoni, aliona kundi la watu likija na wakati akijiandaa kuwahoji walimkamata na kumfunga kamba.
"Mmoja ndio alinishika na kunifunga kamba, wengine walikuwa wakibomoa nyumba kwa kutumia vyuma vikubwa. Yule aliyekuwa amenishika alikuwa pia ameshikilia bastola na aliniambia kuwa nisipokuwa mtulivu au nikikimbia atanipiga risasi," alisema Nang'oro.
Kwa upande wake, Musa alisema tangu achaguliwa kushika nafasi hiyo, vielelezo vilivyopo katika ofisi yake vinaonyesha kuwa mwenye eneo hilo ni Yasinta na siyo mtu mwingine.HCANZO MWANANCHI

Maisha Yana.................

1 2cb96
 Mbarali, Mbeya

Magazeti


1 61022
2 b0c24
3 c97b0
4 b0918
5 ef0e4

6 851ad
7 9255c
8 b491b
9 786fe
10 e8f99
11 a3f59
12 da17a

Saturday, April 27, 2013

Maisha Yanae........................

8 d6afc
Mfanyabiashara wa matunda katika Manispaa ya Morogoro akiwa na mtoto wake huku akipanga Embe kando ya barabara ya Madaraka eneo la Luna wakati akisubiri wateja.Fungu moja huuzwa kwa Sh1,000                      :Picha na Juma Mtanda

Magazeti


1 9b7c0
2 341cb
3 90275
4 96d67
5 8e224
soma mengine zaidi

6 263ce
7 96cfa
8 896d8
9 fef77
11 96d0f
12 f71eb
13 9c934
 

Yanga bingwa 2012/13 baada ya Azam kutoka sare 1-1 na Coastal Union

Yanga f391d
Kikosi cha Yanga

Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe Dar es salam
Klabu ya Yanga ya Dar es salaam leo imejitangaziwa ubingwa wake wa 24 wa ligi kuu soka Tanzania bara baada ya wapinzani wake wakubwa kwa muda mrefu klabu YA Azam fc kutoa sare ya kufunga bao 1-1 na Wagosi wa kaya Coastal unioni katika dimba la CCM Mkwakwani jijini Tanga.

Matokeo hayo yana maanisha, Azam FC waliokuwa washindani wakuu wa Yanga SC waliojikusanyia pointi 56 kibindoni, hawawezi tena kufikisha pointi hizo ambazo wanazo mabingwa hao wapya, kwani hata wakishinda mechi zao nyingine  mbili zilizobaki, watamaliza na pointi 54. 


Shukurani kubwa kwa  nyota wa Coastal union Danny Lyanga, ambaye aliifungia Coastal bao la kusawazisha dakika ya 72 akipokea pande maridhawa kutoka kwa nyota wa zamani wa Yanga Pius Kisambale. 
Azam ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao katika mchezo wa leo, lililofungwa na beki Aggrey Morris kwa penalti dakika ya 60, baada ya mshambuliaji wa zamani wa Yanga SC, Gaudence Mwaikimba kuchezewa rafu kwenye eneo la hatari  na beki Yussuf Chuma- na refa Andrew Shamba wa Pwani akaamuru pigo hilo.

Matokeo haya yanakuwa sawa na Coastal kulipa fadhila kwa Yanga, kwani hata wao, ubingwa wao pekee wa Ligi Kuu waliochukua mwaka 1988 ulitokana na ‘msaada’ wa wana Jangwani hao.

Kilichobaki kwa Yanga sasa ni kulinda heshima kutokana na kubakiwa na mechi mbili ambapo watashuka dimbani kuvaana na Coastal union waliowapa ubingwa msimu huu pamoja na mechi ya kufunga dimba dhidi ya Mnyama Simba uwanja wa Taifa Dar es salaam

Lakini licha ya Coastal union kuwapa ubingwa wanajangwani hao, Kocha mkuu wa wagosi Wakaya Hemed Morroco  amesema mchezo wa leo walistahili kushinda na kilichokwamisha ushindi leo ni waamuzi kuchezesha hovyo.

“Unajua Azam walikuwa na Presha kubwa ya kutaka ushindi, lakini tuliwabana na waamuzi wameshindwa kuchezesha vizuri na ndio maana wameambulia sare vinginevyo walikuwa wanafungwa leo”. Alisema Morroco.

Kikosi cha Coastal Union leo kilikuwa; Shaaban Kado, Hamad Khamis, Othman Tamim, Philip Mugenzi, Yussuf Chuma, Abdi Banda, Joseph Mahundi, Razack Khalfan, Pius Kisambale/Mohamed Soud dk85, Suleiman Kassim ‘Selembe’/Danny Lyanga dk71 na Twaha Shekuwe. 
Azam FC; Mwadini Ally, Himid Mao, Erasto Nyoni, David Mwantika, Aggrey Morris, Jabir Aziz/Salum Abubakar ‘Sure Boy Jr.’ dk75, Brian Umony/Seif Abdallah Karihe dk68, Ibrahim Mwaipopo, Gaudence Mwaikimba/Abdi Kassim ‘Babbi’ dk82, Humphrey Mieno na John Bocco ‘Adebayor’.

TASWIRA MBALIMBALI ZA SHEREHE ZA MIAKA 49 YA MUUNGANO

Published in Jamii
00 6acbb

11 eeed4

22 4d38c

33 8d047

Monday, April 22, 2013

MAMA SALMA KIKWETE AZINDUA WIKI YA CHANJO KITAIFA.

24Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipata maelezo kutoka kwa Mtaalam wa maabara wa kituo cha afya cha Mlandizi ,wilayani Kibaha katika mkoa wa Pwani, Bwana Sostenes  Nyang’olo, jinsi ya kuchukua vipimo vya damu na makohozi kutoka kwa wagonjwa wakati wa uzinduzi wa wiki ya chanjo kitaifa iliyofanyika huko Mlandizi tarehe 22.4.2013. 25Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na akinamama na akina baba waliowaleta watoto wao kwa ajili ya chanjo wakati wa uzinduzi rasmi wa wiki ya chanjo kitaifa iliyofanyika huko Mlandizi, wilayani Kibaha tarehe 22.4.2013. 26Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na akinamama na akina baba waliowaleta watoto wao kwa ajili ya chanjo wakati wa uzinduzi rasmi wa wiki ya chanjo kitaifa iliyofanyika huko Mlandizi, wilayani Kibaha tarehe 22.4.2013. 28Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na akinamama na akina baba waliowaleta watoto wao kwa ajili ya chanjo wakati wa uzinduzi rasmi wa wiki ya chanjo kitaifa iliyofanyika huko Mlandizi, wilayani Kibaha tarehe 22.4.2013. walioweza kuwaleta watoto wadogo kwenye chanjo wakiambatana na wake zao. 42 43Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifuatana na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Mheshimiwa Dr. Seif Rashid wakishiriki kuimba na kikundi cha kwaya cha Anglican Compassion kutoka Bagamoyo wakati wa uzinduzi rasmi wa chanjo kitaifa ulifanyika katika kijiji cha Mlandizi 

Maisha Yanaendelea

2 30a7b
Hapa ni Dar es salaam magomeni kagera barabara ya morogoro, msimu huu wa mvua na marundo haya ya taka je tuta nusurika na magojwa ya mlipuko?:Picha na  mjegwa blog Dar es salaam.

Magazeti

1 710d5
2 f0948
3 ffbc5
4 8898b
5 0ba69
soma mengine zaidi

6 32935
7 e52aa


8 bef73
9 81bd2
10 d390d
11 0d99d
12 02940
13 04549

15 70e6b
16 6090d