WATU wawili wamepoteza maisha yao papo hapo na wengine watano kujeruhiwa
baada ya kuripukiwa na bomu lililodaiwa kurushwa na watu wasiojulikana
katika kijiji cha Kamwendo kata mbuba tarafa Rulenge wilayani Ngara
mkoani Kagera.
Taarifa zilizotolewa na kamanda wa jeshi la polisi
mkoani Kagera Hennry Salewi,juu ya tukio hilo,ameeleza kuwa tukio hilo
la kusikitisha lilitokea juzi Mei 13 majira ya saa 3 usiku ambapo
wahanga wa mlipuko wa bomu walikuwa wakitoka kuangalia taarifa katika TV
iliyokuwepo kijijni kwao,ambapo wakati wakitoka nje walirushiwa bomu na
watu wasiojulikana ambao walitokomea gizani kwani ulikuwa usiku wa
giza.
Salewi amesema kuwa wawili waliopoteza maisha hapo hapo ni Felista William(57) na kijana Antiba Adrian(14)wote wakazi wa
kijijini hapo,huku majeruhi wakiwa watano ambao amewataja kuwa
ni Anatoria John(40)aliyeruhiwa shavu la kushoto,Angelina
Benard(29)alijeruhiwa paja mguu wa kushoto na Anna William(28)ambaye
alijeruhiwa tumboni.
Wengine ni Dikson Maton(28)alijeruhiwa paja
mguu wa kulia pamoja na Ndaishimiye Daniel(17)ambaye pia alijeruhiwa
tumboni,wote wahanga hao walikuwa wakitoka kuangalia taarifa ya habari
kabla ya kurushiwa bomu hilo.
Kamanda Salewi amekana kuwa bomu
hilo halikurushwa ndani ya jengo bali lilirushwa nje mlangono ambapo
wahanga walikuwa ndo wanatoka kuangalia taarifa ya habari kama ilivyo
kawaida ya watu kukusanyika katika sehemu kuangalia taarifa ya
usiku,japo jeshi la polisi linaendelea kufanya uchunguzi juu ya kisa cha
kurushwa bomu hilo.
Aidha,Salewi amesema kuwa matukio ya mabomu
katika mkoa wa Kagera,si ajabu kwani ni mara nyingi kila opereisheni za
polisi ni lazima wakikamatwa majambazi lazima wabainike na mabomu ya
kutupewa kwa mkono.
Amesema kuwa ingawa tukio hilo linahusishwa
na ugomvi wa mashamba kati ya marehemu na wahusika wengine,lakini bado
uchunguzi un aendelea kwani miaka miwili iliyopita mtoto wa marehemu
(Felista)naye alirushiwa bomu kama alivyorushiwa mama yake na alikufa
papo hapo.
Amebainisha kuwa matukio ya mabomu katika kijiji
hicho,yawezekana kusababishwa na mwiingiliano uliopo baina ya raia wa
nchi jirani(Burundi)kwani kijiji kiko mpakani na hata shilingi
inayotumika ni ya nchi jirani,hivyo kila wakati matukio yanakuwa ni ya
kutumia silaha.Hivyo kuwaomba wananchi kutoa ushirikiano iwapo kama
kunataarifa zingingine juu ya tukio hilo.
MWISHO
No comments:
Post a Comment