Na Mwandishi Wetu
Bukoba
MEYA wa halmashauri ya manispaa ya
Bukoba Anatory Amani ameanza kuwatishia amani waandishi wa habari
walioko mkoani Kagera wanaojaribu kueleza ukweli juu ya miradi ya
maendeleo ambayo manispaa hiyo inataka kuitekeleza na kwa kushirikiana
na wabia.
Katika hali isiyo ya kawaida meya huyo alimkwida tai
mwandishi wa habari wa gazeti la Mtanzania, Audax Mutiganzi na mfukuza
ofisini kwake kwa kumsukuma nje kwa nguvu, alikuwa ameandama na ofisa
mkuu mtendaji wa benki ya posta nchini Sabasaba Moshingo aliyekuwa
kwenye ziara ya siku mbili mkoani Kagera.
"Toka, toka, toka
ofisini kwangu sikutaki unatuandika vibaya wewe ni mtu mbaya kwetu
hatukutaki kabisa na kamwe utawahi kukanyaga ofisini kwangu, toka nje ya
ufisi yangu maramoja" alisema hiyo huku akinyanyuka kwenye kiti chake
na kumkwida mwandishi tai na
kumsukuma nje na kufunga mlango kwa nguvu.
Amani alimfukuza
mwandishi huyo kwa madai kuwa anaandika habari mbaya zinazohusiana na
manispaa hiyo hasa zinazohusina na miradi ya iliyoghubikwa na utata hasa
kwa upande wa kanuni na sheria za manunuzi ambayo ni pamojan na ya
ujenzi wa soko kuu na wa upimaji wa viwanja.
Meya huyo kabla ya
kumfukuza mwandishi huyo alitoa maelekezo kwa kaimu Mkurugenzi wa
manispaa ya Bukoba, Steven Nimziirwa alimweleze meneja wa Benki ya posta
Maduhu Makoye amueleze mwandishi huyo asiingie kwenye ofisi ya Meya
huyo kwa madai hataki kukutana naye.
Nimziirwa alifanya kama
alivyoagizwa na meya wake, mwandishi huyo pamoja na taarifa hiyo alikaa
kimya akaendelea kutekeleza wajibu wake wa kukusanya taarifa za matukio
ya ziara ya ofisa mkuu mtendaji wa benki ya posta nchini.
Mwandishi baada ya kufanyiwa unyama huo na meya alienda moja kwa moja hadi kituo cha polisi kutoa taarifa juu ya tukio hilo
yenye kumbukumbu namba BU/RB/3161/2012, taarifa hiyo ilifunguliwa kituo kikuu cha polisi.
Meya
huyo amekuwa na tabia ya kuwatishia waandishi wa habari, hivi karibuni
aliwatishia waandishi wa habari wa kituo cha radio Kasibante kilichoko
mkoani Kagera kwa madai ya kuhoji miradi inayotekelezwa na manispaa kwa
kushirikiana na wabia.
Amani alipotafutwa ili athibitishe
malalamiko yaliyotolewa na mwandishi wa habari simu yake ilikuwa inaita
bila kupokelewa, alitumiwa ujumbe mbalimbali wa maandishi kwenye simu
yake na waandishi wa habari lakini alikataa kuujubu.
Hivi
karibuni gazeti ka Mtanzania lilikuwa likifuatilia kwa karibu miradi ya
maendeleo ambayo manispaa inataka kuitekeleza kwa kushirikiana na wabia,
gazeti hili lilikuwa linaelezea ukikwaji wa taratibu za manunuzi za
kuiteua kampuni ya OGM mwandisi mshauri wa mradi wa ujenzi wa soko kuu
la Bukoba.
Katika mradi huo kampuni ya OGM ambayo inadaiwa kutokuwa na sifa za kuufanyia
mradi huo usanifu itachota zaidi ya milioni 590.
Mwisho
No comments:
Post a Comment