Na James Magai
MAWAKILI
wanaomtetea mwigizaji wa filamu, Elizabeth Michael maarufu kwa jina la
Lulu anayekabiliwa na kesi ya mauaji, wamewasilisha Mahakama Kuu, Kanda
ya Dar es Salaam maombi ya uchunguzi wa umri wa mteja wao.
Lulu
anakabiliwa na kesi ya mauaji ya msanii mwenzake Steven Kanumba katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akidaiwa kutenda kosa hilo nyumbani kwa
marehemu Machi 7, mwaka huu.
Mawakili
hao waliwasilisha maombi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Mei 7,
mwaka huu wakiiomba iamuru kesi ya msanii huyo isikilizwe katika
mahakama za watoto wakidai kuwa mteja wao ni mtoto.
Hata
hivyo, mawakili hao waligonga mwamba baada ya mahakama hiyo kutupilia
mbali ombi hilo ikisema ingawa kesi bado iko katika hatua za awali,
haiwezi kufanya uchunguzi huo kwa kuwa haina uwezo wa kusikiliza kesi
hiyo.
Jana,
mawakili wanaomtetea msanii huyo waliwasilisha maombi Mahakama Kuu
wakiiomba itoe uamuzi kama Mahakama ya Kisutu ina uwezo wa kuamua
ufanyike uchunguzi wa umri halali wa msanii huyo kwa kuwa wanaamini kuwa
ina mamlaka hayo.
Katika
maombi hayo namba 46 ya mwaka 2012, yaliyosilishwa na Wakili Peter
Kibatala kwa niaba ya jopo la mawakili hao, pia wanaiomba Mahakama Kuu
kama itaridhika kuwa Mahakama ya Kisutu haina uwezo huo, basi yenyewe
ifanye uchunguzi huo.
Akifafanua
juu ya maombi hayo, Kibatala ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Chama cha
Wanasheria Tanganyika (TLS), alisema Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009,
Kifungu cha 113 inaruhusu Mahakama kufanya uchunguzi wa umri wa
mshtakiwa.
Wakili
Kibatala alisema lengo la uchunguzi huo ni kuifanya ijiridhishe kama
mshtakiwa ni mtoto au ni mtu mzima kwa lengo la kuangalia maslahi ya
mtoto.
“Baada
ya uchunguzi huo, mahakama ikijiridhisha kuwa ni mtoto, basi mwenendo
wa kesi hiyo utaendeshwa kwa maslahi ya mtoto kwa mujibu wa Kifungu cha
4(2) cha Sheria ya Mtoto,” alisema.
Alisema kifungu hicho huelezea ulinzi na maslahi ya mtoto katika uendeshaji wa kesi kwa watoto wanaokinzana na sheria.
Alisema kifungu hicho huelezea ulinzi na maslahi ya mtoto katika uendeshaji wa kesi kwa watoto wanaokinzana na sheria.
Mawakili
hao wakiwa katika Mahakama ya Kisutu, walidai kwamba msanii huyo ana
umri wa miaka 17 na kwa maana hiyo bado ni mtoto na kesi yake haipaswi
kusikilizwa katika mahakama za kawaida kama mtu mzima.
Katika uamuzi wake, Hakimu Mkazi Augustina Mmbando anayesikiliza kesi hiyo alisema bado iko kwenye upelelezi na kwamba kulingana na jinsi ilivyo isingekuwa busara kuamua hoja yoyote na aliutaka upande wa utetezi uwasilishe maombi hayo kupitia Mahakama Kuu.
Katika uamuzi wake, Hakimu Mkazi Augustina Mmbando anayesikiliza kesi hiyo alisema bado iko kwenye upelelezi na kwamba kulingana na jinsi ilivyo isingekuwa busara kuamua hoja yoyote na aliutaka upande wa utetezi uwasilishe maombi hayo kupitia Mahakama Kuu.
Wakati
akiwasilisha maombi hayo awali Mahakama ya Kisutu, kiongozi wa jopo la
mawakili wanaomtetea msanii huyo, Wakili Kennedy Fungamtama alidai kuwa
mteja wao ana umri wa miaka 17 na si 18 kama inavyotamkwa mahakamani.
Alidai
kuwa hata cheti cha kuzaliwa walichokiwasilisha mahakamani, kinaonyesha
mahali na tarehe aliyozaliwa mshtakiwa hivyo kuwa na umri wa miaka 17.
Fungamtama
alidai kuwa kulingana na Sheria ya Mtoto ya 2009, inatafsiri kuwa mtoto
ni yule aliye na umri chini ya miaka 18 hivyo katika suala la mteja
wao, alipaswa kushtakiwa katika mahakama ya watoto.
Hata hivyo,.... Soma zaidi; http://www.mwananchi.co.tz
No comments:
Post a Comment