Agizo hilo lilitolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho Nape Nnauye siku ya Ijumaa baada ya kupokea malalamiko ya Umoja wa Vijana wa chama hicho(UVCCM)waliodai baadhi ya madiwani wamegeuza majengo ya Saccos kwa ajili ya matumizi ya ofisi zao.
Nape
alikuwa Wilayani humo kufungua Baraza la vijana wa UVCCM ambalo pia
lilihudhuriwa na wanachama wa chama hicho na viongozi mbalimbali huku
kukiwa na mwitikio mdogo wa vijana.
Nape
aliwataka madiwani hao kujenga ofisi zao na kuwa wanatakiwa kuondoka
katika majengo hayo na kuwa wasisubiri vijana waendelee kulalamikia
suala hilo linaloathiri ukuaji wa vyama hivyo.
"Madiwani
jengeni ofisi zenu acheni zifanye kazi ya Saccos,kama madiwani mliweza
kushawishi wapiga kura wakawachagua tushawishi pia tukujengee
ofisi"alisema Nape
Aidha Nape alisema endapo madiwani hao wataendelea kutumia majengo ya Saccos kama ofisi zao wanaweza pia kuhatarisha ukuaji na lengo zuri la kuanzisha wa vyama hivyo vya kuweka na kukopa.
Awali
Katibu wa UVCCM Wilayani Missenyi Philbert Ngemera katika taarifa yake
kwa Nape alisema majengo ya Saccos yalioyengwa kila Kata na aliyekuwa
mbunge wa Jimbo hilo Dk Diodorus Kamara yametekwa na baadhi ya madiwani
na kuzifanya kuwa ofisi zao.
Pia alihainisha changamoto mbalimbali zinazowakabiri vijana kuwa
ni pamoja na upandaji holela wa bidhaa na vijana kukimbia chama hicho
kwa madai ya kutowajali huku wakiendelea kuwa na maisha magumu.
Aidha
alisema katika baadhi ya maeneo wamekosa vijana wakujitokeza kugombea
uongozi kwa kile alichodai ni wengi wao kukosa sifa na kuwa hadi sasa
vijana 178 wamekimbia chama hicho na kuhamia Chadema idadi aliyosema ni
ndogo ikilinganishwa na vijana wengi wanaoendelea kuiunga mkono CCM.
Kaatika
hotuba yake pia Nape aliwaeleza vijana kuwa wana nafasi ya kuchagua
viongozi wanaofaa kukiimarisha chama na kuwa wasikubari kurubuniwa hasa
katika kipindi hikia mbacho CCM inaendelea na uchaguzi wa ndani.
Mbali
na kusema kuwa mageuzi ni lazima ndani ya chama hicho ili kuendana na
wakati pia alisema hata wakuu wa Wilaya walioteuliwa hivi karibuni chama
kimewaeleza wasifanye mchezo katika maeneo yao kwani nyumbani kwao ni
CCM.
Kwa
mujibu wa Nape wakuu hao wa wilaya wanatakiwa kufanya kazi kwa masirahi
ya chama na kuongeza kuwa ikitokea chama kingine kinachukua dola nacho
kinachagua viongozi wake.
No comments:
Post a Comment