Bukoba
Kanal
mstaafu Fabiani Massawe ni mkuu wa mkoa wa kagera amewashauri
wanachama na waandishi wote mkoani humu kuandika habari za uchunguzi
wakifuata misingi,maadili na kanuni za uandishi wa habari ili kufanya
kazi yao kuwa nyepesi na isiyokuwa na migongano isiyokuwa ya lazima.
Massawe
aliwashauri waandishi kuandika habari za uhakika kwa kutumia vyanzo
sahihi kabla ya kuandika habari na kutoandika habari zinazopendelea
upande mmoja na zenye maslahi binafsi ili kuepuka kusababisha
migawanyiko ndani ya jamii inayoweza kusababisha uvunjifu wa amani ambapo alitoa mfano wa vita vya Kimbali vilivyosababishwa na uchochezi wa baadhi ya vyombo vya habari huko nchini Rwanda.
Aliwataka
waandishi kuacha tabia ya kuomba mishiko au bahasha ndipo waandike
habari kwa madai kuwa tabia hiyo ni kujidhalilisha na kuonekana
waandishi ni watu wa kulalamika kila wakati kuwa hawana kitu jambo
ambalo ameziomba klabu na waajiri wa vyombo mbalimbali kulifanyia kazi
kwani ni kero inayowafanya watoa habari kujenga uadui na waandishi kwa
madai kuwa wamekuwa wakitishia kuwa wakinyimwa mishiko hawaandiki habari
ya aina yoyote.
Pia
amewashauri waajiri wa vyombo mbalimbali vya habari hususani radio za
kijamii zipatazo tano za mkoa wa Kagera kutafuta utaratibu wa kuwaondoa
waandishi makanjanja ambao wamekuwa wakiajiriwa kwani wanalipwa ujira
mdogo huku waandishi wenye ujuzi na kazi hizo wakikosa nafasi jambo
ambalo amedai kuwa matokeo yake wamekuwa wakitumia radio hizo kujadili
maisha ya watu na kuongea mambao yasiyofaa katika jamii huku wengine
wakitangaza habari za mapenzi tu wakati kuna habari zinazogusa jamii
mfano wahamiaji haramu na rushwa hazipati nafasi jambo ambalo amedai
kuwa ni kuidhalilisha taaluma hiyo muhimu.
Kanal
Massawe alikuwa mgeni rasmi katika sherehe za kuadhimisha sikuukuu hiyo
ya uhuru wa vyombo vya habari ambapo kwa mkoa wa Kagera ilifanyika
katika ukumbi wa Coffee Tree in ndani ya Manispaa ya Bukoba na
kudhaminiwa na muungano wa vilabu vya waandishin wa habari
nchi (UTPC)na kuudhuliwa na viongozi mbalimbali wa mkoa huo ikiwa ni
pamoja na Mwenyekiti wa bodi ya kahawa nchini Pius Ngeze,Kamanda wa
Takukuru mkoa Domina Mkama,Kaimu kamanda wa polisi mkoa Vitus
Mlorele,mkuu wa Wilaya ya Bukoba Samweli Kamote na viongozi wa vyama vya
siasa mkoa na Wilaya.
Aidha mkuu
huyo wa mkoa aliiahidi kuwachangia kiasi cha shilingi milioni moja kama
mchango wa kununulia kiwanja cha kujenga ofisi ya klabu hiyo ili waweze
kuondokana na usumbufu wanaoupata wa kupanga kwenye
majumba ya watu ambapoa wamekuwa wakiwasumbua mara kwa mara pasipokuwa
na sababu za msing .
Katika
hatua nyingine klabu ya Waandishi wa habari mkoani Kagera (KPC) imetoa
msaada mbalimbali katika wodi za wagonjwa katika hospitalia ya mkoa wa
Kagera.
Tukio hilo lililifanyika May 5 katika hospitali hiyo kwa kukabidhi misaada mbalimbali katika wodi za watoto hospitalini hapo.
Mwenyekiti
wa Klabu ya waandishi wa habari mkoani Kagera John Rwekanika alisema
kuwa wanachama wa KPC wapatao 34 wamelazimika kutoa misaada hiyo
katika tamasha lao lakuadhimisha uhuru wa vyombo vya habari duniani
iliyoadhimishwa mei 5 badala ya mei 3 mwaka huu inayoadhimishwa kila mwaka kutokana na wanachama na wanachama wengi kukabiliwa na majukumu mwengi katika tarehe rasmi inayoadhimishwa ulimwenguni.
Alisema
kuwa misaada iliyotolewa ni pamoja na sabuni,sukari na biskuiti vyote
vyenye thamani ya shilingi laki 2 ambapo vyote viligawiwa katika wodi za
watoto ambazo alizitaja kuwa ni namba saba yenye wodi mbi A na B
tofauti na kuwa jumla ya watoto 55 waliolazwa katika hospitalia hiyo
wamepokea misaada.
Alisema
kuwa waandishi wa habari ni sawa na taasisi au jumuiya yoyote ya kirai
inyopaswa kushirikiana na raia katika shughuli zote za kijamii kuwa
kutokana na chama chao kuwa na ushirikiano wa dhati wameonelea kutumia
fursa hiyo kuungana na wagonjwa,wazazi na wauguzi wa hospitali hiyo.
Kwa
upande wake kaimu mganga mfawidhi wa hospitalia hiyo Dk.Leonce Mboyerwa
alisema kuwa kitendo kilichofanya na waandishi wahabari hao wa Klabu
hiyo ni cha kizalendo na kuwa kimeonyesha ni kiasi gani waandishi
walivyo na mchango mkubwa katika jamii.
Mboyerwa
aliongeza kuwa waandishi wa habari wanafanya kazi katika mazingira
magumu lakini wameweza kuonyesha moyo wao wa upendo katika maadhimisho
yao ya uhuru wa vyombo vya habari kwa kuungana na jamii inayowategemea
kuwa hata taasisi nyingine za Kiserikali na zisizo za Kiserikali
wanapswa kuiga mfano uliotolewa na wanachama na uongozi wa KPC.
Aidha
mmoja wa wazazi katika Wodi ya watoto namba saba A Joyce Rweyemamu
alisema waandishi wa habari wameonyesha kitendo cha utu na kuwa
wameionyesha jamii kuwa wao ni kioo cha jamii.
Alisema
kuwa pamoja na misaada walioipokea kutoka kwaandishi hao kuwa wawapo
katika hospitali hiyo wanakabiliwa na changamoto ya kukosekana kwa
madawa na kuwa mgonjwa aliyelazwa analazimika kujinunulia madawa ambapo
wagonjwa wengine wanakuwa hawa uwezo wa kujinunulia madawa kuwa jambo
hilo linadhiri afya na kusababisha vifo vya mara kwa wagonjwa.
Naye
mku wa idara ya watoto hospitalia ya mkoa wa Kagera Gerad Kabyemera
alikiri kuwepo kwa hari hiyo ya upungufu wa madawa na kuwa tatizo hilo
halisababishwi na uongozi wa hospitali balia linasababishwa na stoo kuu
ya madawa makao mkauu ya afya Dar Es Salaam.
Kabyemera
alisema kuwa uongozi wa hospitali unaomba wastani wa asilimia 100 ya
madawa kutoka makao makuu lakini wanatumiwa wastani wa asilimia 40 ya
madawa walioomba ambayo hayawezi kutosheleza mahitaji ya wagonjwa
kulingana na idadi ya wagonjwa wanaolazwa katika hospitali hiyo.
mwisho
No comments:
Post a Comment