Wednesday, June 27, 2012

Polisi Kagera Yatoa Taarifa Za Matukio Mbalimbali


Haya ndio mafanikio ya operation maalumu iliyoendeshwa na jeshi la polisi mkoani Kagera kuanzia juni 8, mwaka huu.




Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera Peter Kalangi akionyesha misokoto ya bangi iliyokamatwa na jeshi la polisi, pembeni yake ni mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai mkoani humo Peter Matagi.




Sehemu ya vifaa vya maabara mali ya shule ya sekondari ya Nyakato iliyoko mkoani Kagera ambavyo jeshi la polisi lilivikamatwa.




JESHI la polisi mkoani Kagera linamshikilia Peter Mabara (28) msukuma mwenyeji wa Kahama kwa tuhuma ya kusababisha kifo mwanafunzi wa kidato cha pili wa shule ya sekondari ya Kaagya iliyoko tarafa ya Bukoba.

Akisimulia tukio hilo mbele ya waandishi wa habari ofisini kwake mbele ya waandishi wa habari jana kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera Peter Kalangi alisema Mabara ambaye ni mchunga Ng’ombe anatuhumiwa kumuua Advea Makanyaga (16) juni 24 mwaka huu.

Kalangi aliwaambia waandishi habari kuwa Marehemu kabla ya kifo chake alitumwa na bibi yake Mariselina Bigira (53) mhaya mkazi wa mshozi kupeleka chakula porini kwa mtuhumiwa wa mahuaji ambaye alikuwa akichunga Ng’ombe wanamilikiwa na bibi yake huyo.

Alisema marehemu huyo alipoenda porini hakurudi tena hadi mwili wake ulioonekana umetelekezwa porini juni 25, mwaka huu, Kalangi alisema mwili wa marehemu huyo ulikutwa umwekewa jiwe kubwa kichwani huku ukiwa na majeraha mbalimbali kwenye mwili na shingo ya marehemu huyo ikiwa inalegea kama iliyonyongwa.

Kamanda huyo alisema jeshi la polisi lilipopata taatifa hizo lilikwenda kwenye tukio na kuanza kufanya kazi ya upelelezi, alisema upelelezi wa awali wa jeshi hilo ulionyesha uhusiano wa kifo mwanafunzi huyo na mchunga ng’ombe.

Aliendelea kusema kuwa kilichodhihirisha uhusiano wa kifo cha marehemu na mchunga ng’ombe huyo ni hatua yake ya kutaka kutoroka, alisema mchunga ng’ombe alinaswa na jeshi la polisi eneo la standi kuu mabasi Bukoba akitaka kutoroka kwenda kwao kahama.

Kalangi alisema taarifa nyingine za awali za kiupelelezi zinaonyesha kuwa mchunga ng’ombe huyo alikuwa akimtaka mapenzi mwanafunzi huyo kwa kipindi kirefu na mwanafunzi huyo alikuwa akimkatalia.

Aidha, kamanda huyo wa jeshi la polisi alieleza mafanikio ya operation iliyoiendesha ya kupambana na uharifu mkoani Kagera kuanzia juni 8, mwaka huu, alisema jeshi hilo lilifanikiwa kukamata shamba la bangi hekta 1 na magunia 2 ya bangi wilayani Biharamulo lililokuwa linamilikiwa Alfred Philip aliyetoroka.

Alisema pia jeshi hilo lilifanikiwa misokoto ya ya bangi ikiwa kwenye gunia, mirungi gunia moja na gramu 400 ambapo watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani, aliendelea kusema katika wilaya za muleba na karagwe jeshi hilo pia lilikamata magunia matatu ya bangi.

Alimaliza kwa kusema jeshi la polisi litaendelea na misako yake ya kupambana na wale wote wanaojihusisha na vitendo vya uharifu,”hii sio nguvu ya soko nitawashughulikia wote wenye nia mbaya ndani ya jamii, ndugu wananchi nawaombeni mniunge mkono” alisema Kalangi.




Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akisalimiana na Mbunge wa Lindi Mjini , Salum Baluany kwnye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Juni 25,2012. Kulia ni Mtoto wa Waziri Mkuu, George Bush. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)




Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua zabibu wakati alipotembelea shamba la Tendaji Agro lililopo katika kijiji cha Chikopelo wilayani Bahi, Dodoma juni 24, 2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Maisha Yanaendelea

 kijiji cha Kalambazite Sumbawanga.

Kamati Ya Lowassa Yaivaa Wizara Ya Membe


KAMATI ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama imeanza ziara ya siku 14 katika balozi za Tanzania kwenye nchi za Marekani, Ulaya na Asia kukagua namna zinavyotekeleza mambo ya sera na uchumi.

Ziara ya Kamati hiyo inayoongozwa na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa ilitangazwa jana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar ers Salaam wakati wajumbe 20 wa Kamati hiyo na makatibu sita wanaondoka nchini.

Hata hivyo, wakati Kamati hiyo ikienda kutembelea balozi hizo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe mwenye dhamana na balozi hizo, alisema ziara hiyo haikuja wakati sahihi, kwa kuwa Mkutano wa Bunge la Bajeti unaendelea.

Lakini, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ziara hiyo, Lowassa alisema ziara hiyo imekuja wakati sahihi kwa kuwa hiyo pia ni kazi ya Bunge.

Katika ziara hiyo, Kamati hiyo imegawanyika katika makundi sita yatakayotembelea balozi 14 katika nchi 14. Wabunge hao ni yeye Lowassa, Vita Kawawa, Khalifa Suleiman Khalifa, Rachel Mashishanga na Beatrice Shelukindo ambao watatembelea balozi za Canada, Washington na New York, Marekani na London, Uingereza.

Wengine ni Mohamed Ibrahim Sanya, Mchungaji Israel Natse ambao watatembelea New Delhi, India na Kuala Lumpur, Malaysia.

Kundi jingine lina Mussa Zungu, Brigedia Jenerali Hassan Ngwilizi, Betty Machangu na Mussa Hassan Mussa linaotembelea balozi za Japan na China.

Kundi la nne litakalotembelea Ujerumani na Sweden, linawahusisha Anna Abdallah, John Shibuda na Augustino Massele, huku wabunge wengine akiwamo Mohamed Seif Khatib, Hilda Ngoye na Anastazia Wambura watatembelea balozi za Brussels, Ubeligiji na Geneva, Uswisi.

Kundi la mwisho linalotembelea Paris Ufaransa na Rome Italia, linawahusisha wabunge John Chiligati, Engen Mwaiposa na Masoud Abdallah Salim.

Kauli ya Membe
Ziara hiyo imeonyesha kumshangaza Waziri Membe akisema kuwa hajui wanakwenda kufanya nini huko.
Akizungumza na gazeti dada la The Citizen jana katika uwanja huo, Waziri Membe aliyekuwapo katika uwanja huo, alisema ziara hiyo haikuja wakati sahihi.

“Shughuli za Kamati huko nje huwa ni kujifunza kutoka kwa wenzao kwenye mataifa tofauti, na ziara hii hilo halikufanyika….lakini nimesikia wanakwenda kutembelea balozi zetu huko nje na sio zilizoko katika bara la Afrika,” alisema Waziri Membe.

Aliongeza kuwa, “Hapo inabidi sote tujiulize kama lengo ni kuangalia utendaji wa balozi zetu mbona sasa zinakuwa za Ulaya na Asia peke yake?"

Waziri Membe alifafanua kuwa kwenda kutembelea balozi si tatizo, lakini katika kipindi hiki ambacho Bunge la Bajeti linaendelea mjini Dodoma, kwa busara ya kawaida, mbunge anatakiwa kuwa bungeni akifuatilia Bajeti.

Alisema kulingana na ratiba ya Bunge, ziara kama hiyo ilitakiwa kufanyika wakati wa vikao vya Kamati za Bunge, lakini si sasa ambapo Bunge linakutana.
Licha ya kukanusha mara kwa mara, Waziri Membe na Lowassa wamekuwa wakitajwa kuwania Urais kupitia CCM siku za usoni, jambo ambalo limekuwa likiwataja wabunge hao kama mahasimu wa kisiasa.

Kilichotokea kwenye kamati
Tayari Kamati hiyo imewahi kuripotiwa kuingia katika mvutano Membe, ambapo Juni 6, mwaka huu ilimbana ikisema alichelewa kugawa vitabu vya bajeti yake kwa wajumbe wa Kamati.

Mmoja wa wajumbe wa Kamati hiyo aliliambia gazeti hili kwamba wajumbe waligomea Bajeti hiyo kutokana na kuchukizwa na kitendo hicho na kutokuonyesha madeni ya wizara yakiwamo makato ya wafanyakazi kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii.

Ofisa Habari na Mawasiliano wa Wizara hiyo, Assah Mwambene alipinga taarifa hizo, lakini akafafanua kilichotokea kuwa hoja ya vitabu kuchelewa iliibuka, na tayaru waziri aliwaeleza wajumbe kuwa hilo ni suala ambalo lilitokana na kamati husika.

Alisema vitabu hivyo viliwasilishwa mwisho wa wiki, lakini kwa kuwa labda haikuwa siku za kazi, ndiyo maana havikuwafikia mapema wajumbe.
Chanzo: Mwananchi. http://www.mwananchi.co.tz/habari

Marekani Yataja Makundi Hatari Afrika Makundi matatu ya kigaidi Barani Afrika yameanza kushirikiana katika harakati zao. Hii ni kwa mujibu wa Mkuu wa jeshi la Marekani anayesimamia shughuli za usalama kanda ya Afrika. Jenerali Cater Ham amesema kundi la Al Qaeda Afrika Kaskazini limekuwa likiwasaidia wanachama wa Boko Haram nchini Nigeria na mabomu.


Akizungumza mjini Washington afisa huyo amesema waasi wanaodhibiti kaskazini mwa Mali wameendelea kutumia eneo hilo kuendesha harakati zao ikiwemo kupanga njama za kutekeleza mashambulio.Jenerali Ham ni kamanda wa kitengo cha idara ya ulinzi ya marekani kinachofuatilia masuala ya usalama barani Afrika{Africom} na makao makuu yako Ujerumani.
Kitengo hiki kinaimrisha harakati zozote za kijeshi Afrika ikiwemo mashambulio ya kutumia ndege bila rubani dhidi ya wapiganaji wa Kisomali wa Al shabaab.

Tayari kuna wanajeshi 100 wa Marekani wanaosaidia kumsaka kiongozi wa waasi Uganda Joseph Kony ambao wanasimamiwa na kitengo cha Jenerali Ham.

Afisa huyo ametaja makundi hatari zaidi ikiwa ni pamoja na kundi la Al Qaeda Afrika Kaskazini{AQIM}, Boko Haram na Al-Shabab.

Ameongeza tisho kubwa ni kwamba makundi haya yameanza kushirikiana katika kufanikisha harakati zao.

Mapema mwaka huu nchi ya Mali ilishuhudia mapinduzi ya kijeshi na kufuatiwa na kudhibitiwa kwa eneo nzima la Kaskazini na makundi yanayotetea kujitenga ya Tuareg na wapiganaji wa kiisilamu.

Wakosoa Matumizi Ya Kiingereza, Uzungu Kwenye Filamu Za Kitanzania



Na Mwandishi Wetu

Wadau wa Sanaa wamehoji uhalali wa wasanii wa filamu kutumia kiingereza kwenye majina ya filamu zao huku wakishangazwa na kazi hizo kubeba maudhui ya kizungu zaidi.


Wakizungumza wiki hii kwa nyakati tofauti kwenye programu ya Jukwaa la Sanaa, wadau hao walishangazwa kitendo cha filamu hizo kutumia majina ya kizungu wakati hapa kwetu kuna filamu nyingi kutoka nje zinazotumia lugha za kihindi, kichina, kifaransa na zinafanya vizuri.


“Hoja kwamba, wanatumia majina ya kiingereza ili kuteka soko la kimataifa ni ya kitoto, mbona hapa kwetu kuna filamu nyingi za kihindi na kichina zinanunuliwa kwa wingi? Hapa kuna udhaifu katika kutengeneza filamu zenye ubora tujikite huko”alisema Mzee Nkwama Bhallanga.


Kwa mujibu wa wadau wengi waliozungumza, filamu ni taaluma inayozungumza kwa kutumia picha na vitendo zaidi hivyo haihitaji mtazamaji kufahamu lugha iliyotumiwa ili afahamu maudhui na ujumbe unaowasilishwa na kazi husika ya filamu.


“Maneno kwenye filamu si muhimu sana, kinachozungumza ni matendo na picha zaidi, ndiyo maana kuna watu wanaangalia picha za Kikorea na wanaburudika na kuelewa kinachoendelea” alisema Godfrey Lebejo ambaye ni Murugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na habari, BASATA.


Aliongeza kuwa, kinachoitesa tasnia ya filamu kwa sasa ni kukosekana kwa weledi na uhalisia wa tamaduni zetu kunakosababishwa na wimbi kubwa la watu kujiingiza kwenye filamu ili kufanikisha mambo yao yaliyo nje ya maadili na utamaduni wetu.


“Inawezekana vipi utengeneze filamu ambayo baba, mama na watoto hawawezi kukaa pamoja kuitazama? Tufike mahali tuseme mambo haya ya kipuuzi basi kwenye filamu zetu” alionya Lebejo.


Awali akiwasilisha mada kuhusu Filamu, wasanii na haja ya kujiendeleza kielimu, Msanii wa filamu Emmanuel Myamba maarufu kam Pastor Myamba alisema kuwa, tasnia ya filamu inakosa weledi hivyo kuhitaji mabadiliko.


“Ni wazi ukiangalia filamu zetu zinakosa weledi katika uandishi wa miswada, uongozaji, uhariri na hata uumbaji wa wahusika. Lazima tukubali udhaifu huu turekebishe” alisema Myamba ambaye kwa sasa amefungua kituo cha mafunzo ya filamu kiitwacho Tanzania Film Training Centre (TFTC) kilichoko Ubungo.

Katibu Wa Vijana CCM (uvccm) Singida ‘Omary Mtuwa’ Akanusha Kuhamia Chadema.




Katibu wa umoja wa vijana CCM (UVCCM) mkoa wa Singida,Omary Hassan Mtuwa akitoa taarifa yake kwa waandishi wa habari (hawapo kwenye picha) ya kukanusha taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari kuwa amekihama Chama Cha Mapinduzi na kujiunga na CHADEMA.Picha na Nathaniel Limu.

Katibu wa umoja wa vijana CCM (UVCCM) mkoa wa Singida, Omary Hassan Mtuwa, amekanusha vikali taarifa iliyotolewa na vyombo vya habari, kwamba amekihama chama chake na kujiunga na chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Mtuwa alisema taarifa hizo ni za uwongo uliopea, uzushi na zinalenga kumgombanisha yeye na chama chake pia na viongozi kwa ujumla.

Akifafanua, Mtuwa alisema taarifa hizo zimechapishwa na gazeti moja la kiswahili la kila siku (juni 18) mwaka huu ukurasa wa mbele ulibeba kichwa cha habari kuwa CHADEMA yavuna viongozi wa CCM.

Katibu huyo,alisema taarifa zilizoandikwa kwenye gazeti hilo zilizohusisha cheo cha Katibu wa vijana wa CCM mkoa wa Singida na kwamba anasoma chuo kikuu cha Ruaha, ni za uwongo mtupu.

Mtuwa alisema taarifa hiyo imemkosesha amani na imewasikitisha mno kwa vile, wahusika hawakumtendea haki kwa kumuuliza juu ya madai ya kuhamia CHADEMA. Mwandishi wa habari hiyo, ameandika taarifa hiyo bila kupata maoni kutoka kwake.

“Kama kweli CHADEMA wamevuna viongozi kutoka CCM,hilo mimi silijui na wala silitambui.Lakini kwa upande wangu, wameogopa na wamewapotosha Watanzania kwa kusema katibu wa UVCCM mkoa wa Singida,kahamia CHADEMA”,alisema na kuongeza;

“Mimi Omary Hassan Mtuwa,bado ni mwanachama hai wa CCM na ni mwaminifu wa kiwango cha juu.Nitaendelea kukitumikia chama changu kwa nguvu zote bila kutetereka hadi tone la mwisho”.

Alisema amefedheshwa na kuonewa sana na taarifa hiyo, iliyosheheni uwongo mwingi na kusababisha usumbufu mkubwa kwa mwajiri wake, familia yake na jamii kwa ujumla.

“Kwa hiyo, naomba gazeti hilo lifute,liniombe radhi na kutangaza hatua hiyo kupitia ukurasa wa mbele kama ambavyo limefanya katika kunichafua.Tofauti na hivyo,nitalazimika kwenda mahakamani kudai haki yangu”,alisema Mtuwa. 

Chanzo: MOblog.  http://dewjiblog.com

Mahakama Yatoa Onyo Kwa Madaktari

Chanzo:  http://www.fullshangweblog.com

Vodacom Yahamasisha Wabunge Kutumia Malipo Ya Baada...!




Baadhi ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,wakifafanuliwa jambo na Meneja wa wateja wa Malipo ya baada wa Vodacom Tanzania Bi. Yvone Bayona,jinsi ya kujiunga na mpango wa malipo ya baada ya kampuni hiyo katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma. Vodacom inaendesha zoezi maalum la kuwahamasisha wabunge kujiunga na mpango wa mteja mmoja mmoja wa malipo ya baada katika juhudi za kujiimarisha kisoko.




Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Salvatory Machemli (Ukerewe - Chadema) na Danstan Mkapa (Nanyumbu - CCM) wakielezewa na Afisa wa Vodacom Tanzania Bi.Melinda Siarra,jinsi ya kujiunga na mpango wa malipo ya baada ya kampuni hiyo katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma. Vodacom inaendesha zoezi maalum la kuwahamasisha wabunge kujiunga na mpango wa mteja mmoja mmoja wa malipo ya baada katika juhudi za kujiimarisha kisoko.
 Kutoka Blog ya Michuzi: http://issamichuzi.blogspot.com

Misha Yanaedelea



Kibondo igoma Moja

                                 


                                  

Taarifa Kutoka Kampuni Ya Bia Tanzania (TBL)




            TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

                           Toleo la Leo 

MASHINDANO YA NGOMA ZA ASILI YA BALIMI EXTRA LAGER 2012 KUTIMUA VUMBI KUANZIA JUNI 30.

Dar Es Salaam, June 25th 2012:
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia bia yake ya Balimi Extra Lager, leo imezindua rasmi mashindano ya ngoma za asili ya Balimi Extra Lager kwa mwaka 2012. Mashindano haya ambayo yametokea kupendwa sana na wakazi wa kanda ya ziwa yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi katika mikoa mbali mbali ya kanda ya ziwa kuanzia Juni 30.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo Jijini Dar es Salaam, meneja wa Bia ya Balimi Extra Lager Bi. Edith Bebwa alisema; Bia ya Balimi Extra Lager imekuwa ikiendesha mashindano haya maarufu kama “Mashindano ya Ngoma za Asili ya Balimi Extra Lager” kwa zaidi ya miaka saba sasa , na kwa kweli napenda kusema kuwa ni mashindano yaliyotokea kupendwa sana katika kanda yetu hii ya ziwa,
Lengo kuu la kudhamini mashindano haya ni kushirikiana na wakazi wa kanda ya ziwa katika kuenzi na kulinda tamaduni za kanda alisema Bi Edith .
Kwa mwaka huu wa 2012, mashindano yataanza rasmi tarehe 30 Juni katika ngazi za mikoa na kumalizika tarehe 21 Julai. Tutaanza na mkoa wa Mwanza ukifuatiwa na mikoa ya Mara, Kagera, Shinyanga na Tabora, katika mpangilio ufuatao.

Tarehe Mkoa Viwanja
30/06/2012 KAGERA
Kaitaba
07/07/2012 MWANZA Ccm Kirumba
14/07/2012
TABORA Chipukizi
21/07/2012
SHINYANGA Shycom
21/07/2012
MUSOMA Bwalo la Magereza
28/07/2012.
FINALS MWANZA Ccm Kirumba
Akielezea juu ya zawadi za mwaka huu, bi. Edith Bebwa alisema; kama ilivyo ada ya Bia ya Balimi, kila mwaka tumekuwa tukiongeza zawadi ili kuongeza chachu ya ushindani na kuleta tija kwa washindani. Kwa mwaka huu tumeongeza zawadi kwa takribani asilimia 20 ukilinganisha na mwaka jana. Hii yote inaonesha jinsi gani bia ya Balimi inatambua, inajali na kuthamini utamaduni wa kanda yetu. Zawadi kwa washindi ni kama ifuatavyo;
Ngazi ya mkoa Finali
Mshindi wa kwanza 600,000 1,100,000
Mshindi wa pili 500,000 850,000
Mshindi wa tatu 400,000 600,000
Mshindi wa nne 300,000 500,000
Mshindi wa tano hadi wa kumi kila kikundi 150,000 250,000
Pamoja na zawadi hizi nono, pia Balimi Extra Lager itaendelea kutoa huduma muhimu kwa vikundi shiriki kama vile chakula na malazi. Tunaamini kabisa mambo yote haya yataongeza hamasa na msisimko katika mshindano ya mwaka huu. Na kauli mbiu yetu kwa mwaka 2012 “Balimi Extra Lager, twajivunia utamaduni wetu”.

Akizungumzia maandalizi ya fainali hizo, Meneja Masoko wa Tbl Fimbo Buttalah alisema; Maandalizi yote kwa upande wetu sisi wadhamini yameshakamilika, hivyo niwaombe tu washiriki wote ambao nimepata taarifa kuwa wamekuwa mazoezini kwa muda sasa, waendelee na mazoezi ili kuonesha uwezo wa juu utakaoleta ushindani na kutoa burudani yenye kiwango cha juu.

Kwa niaba ya bia ya Balimi Extra Lager, tunapenda kuwakaribisha watu wote kuhudhuria mashindano haya ambayo tarehe na mahali yatakapofanyikia zitakuwa zikitangazwa redioni ili waweze kushuhudia burudani hii na kuuenzi utamaduni wetu. Pia wananchi wasisahau kuwa katika burudani hizi pia wataburudika na Bia yao waipendayo ya Balimi Extra lager baridi, na kushinda zawadi mbali mbali katika promosheni za Balimi zitakazoambatana na Mashindano haya ya Ngoma za asili ya Balimi Extra Lager.
Kwa Maelezo zaidi wasiliana na:
Edith Bebwa, Brand Manager, +255767266410, edith.bebwa@tz.sabmiller.com
Fimbo Butallah, Marketing Manager, +255767266567, fimbo.butallah@tz.sabmiller.com
Editha Mushi, Communications & Media Manager, +255767266420, editha.mushi@tz.sabmiller.com

Kuhusu TBL
Tanzania Breweries Limited (TBL) inatengeneza, kuuza na kusambaza bia, vinywaji vyenye ladha ya matunda vilivyo na kilevi na vinywaji visivyo na kilevi hapa Tanzania. TBL pia ndiyo kampuni mama ya Tanzania Distilleries Limited pamoja na kampuni shiriki ya Mountainside Farms Limited.

Bia zinazotengenezwa na kampuni ya TBL ni pamoja na Safari Lager, Kilimanjaro Premium Lager, Ndovu Special Malt, Castle Lager, Vinywaji vingine vinavyotengenezwa na kundi la makampuni ya TBL ni Konyagi Gin, Amarula Cream, Redd’s Premium Cold na Grand Malt.

Kundi la makampuni ya TBL limeorodheshwa kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam, limeajiri watu wapatao 1,300 na linawakilishwa nchi nzima na viwanda vinne vya bia, kiwanda kimoja cha kutoneshea, kimoja cha kutengenezea kimea pamoja na bohari nane za kusambazia bia.

Kuhusu SABMiller
SABMiller plc moja kati ya makampuni makubwa ya bia duniani ikiwa na mikataba ya kutengeneza na kusambaza bia kwenye nchi zaidi ya 60 katika mabara matano. Bia zake ni pamoja na zile za kimataifa kama Miller Genuine Draft, Peroni Nastro Azzurro na Pilsner Urquell vilevile na bia nyingine zinazoongoza kwenye masoko ya ndani ya nchi mbalimbali. Nje ya Marekani, SABMiller ni moja ya kati ya makampuni makubwa yanayotengeneza vinywaji vya Coca-Cola duniani. Hivi karibuni SABMiller plc ilinunua kampuni ya bia ya Foster’s pamoja na shughuli zake za uzalishaji nchini India.SABMiller imeorodheshwa kwenye masoko ya hisa ya London na Johannesburg.

Thursday, June 21, 2012

Bei Ya Kahawa Mkoani Kagera Yashuka

Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Kagera John Binushu anaye andika akijadiri jambo na Mrajisi wa Vyama Vya Ushirika Mkoani Kagera Rwenkiko Shorosi


 Na Mwandishi Wetu Bukoba
 
CHAMA kikuu cha ushirika mkoani Kagera(KCU 1990 LTD)kimefikia maamuzi ya kushusha bei ya Kahawa,kwa kile kilichodaiwa kusababishwa na kushuka kwa bei hiyo katika soko la Dunia.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa chama hicho John Binunshu,kushuka kwa bei hiyo ni kutokana na bei ya mnadani kuporomoka kwa siku za hivi karibuni hivyo kulazimu KCU kubadirisha bei ya manunuzi tofauti kama ilivyokuwa hapo awali.

Binunshu alisema kuwa hata hivyo pamoja na kushuka bei hiyo,wakulima wa Kahawa mkoani hapa wasiwe na wasiwasi juu ya taarifa hizi kwani wataendelea kupatiwa taarifa za bei kadili hali ya soko itakavyokuwa inabadirika.

Katika taarifa ya Meneja mkuu wa KCU Vedasto Ngaiza,na nakusambazwa kwa mameneja wote wa  vyama vyamsingi vipatavyo 129 ambavyo vinaendelea na ununuzi wa Kahawa kwa msimu huu ambao umefunguliwa rasmi mwezi Mei mwaka huu,bei ya kahawa imeteremka kutoka shilingi 1350/=hadi kufikia shilingi 1100/=kwa Kahawa aina ya robusta maganda,huku robusta safi itakuwa ikinunuliwa kwa shilingi 2,200/= kwa kilo.


Aidha,Ngaiza alibainisha kuwa Kahawa nyingine aina ya Arabika maganda imeshuka kutoka shilingi 1550/=na kufikia shilingi 1300/=huku safi ikinunuliwa shilingi 2600/=.

Hata hivyo,Ngaiza amesisitiza kuwa wakulima wa zao hili wanapaswa kupokea mabadiliko ya bei hiyo,ila endapo bei itaongezeka mnadani uongozi wa KCU hautachelewa kurekebisha bei hiyo kwa mkulima.

Awali mabadiriko ya bei hizi,yalionekana kuanza kuleta wasiwasi juu kwa wakulima huku baadhi yao wakihushutumu uongozi wa KCU umeamua kutelemsha bei mara baada ya kubaini kuwepo wingi za kahawa kwa wakulima.

MWISHO

Wazee Kata Ya Kahororo Manispaa Ya Bukoba Wazindua Tawi La Saidia Jamii Ya Wazee Kagera (SAJAWAKA)

 Moja ya kitambulisho walivyopatiwa wazee wa kata ya Kahororo Katika Manispaa ya Bukoba ambavyo vitawasaidia kupata huduma ya Matibabu Bure pamoja namambo mengine ya wazee
 Wazee wa kata ya kahororo wakiwa wanasubiri kufunguliwa kwa tawi lao la SAJAWAKA
 Mwenyekiti wa tawi la saidia Jamii Ya wazee Kagera tawi la Kahororo Silivandi Muyoza akitoa utambulisho kwa wazee
 Wakisoma hotuba yao kwa wageni waliofika katika ufunguzi wa tawi la SAJAWAKA
 Anajulikana kama Mrisho Juma ambaye ni afisa maendeleo ya jamii katika Manspaa ya Bukoba hapa yupo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa
 Vitambulisho vikigawiwa kwa wazee wa kata ya Kahororo katika ufunguzi huo

 Mwenyekiti wa Saidia Jamii Ya Wazee Kagera (SAJAWAKA) Mchungaji Temalirwa akitoa ufafanuzi kwa wazee wa kata Kahororo Manispaa ya Bukoba
 Wakionyesha Vitambulisho vyao kwa mpiga picha wetu

 Hatimae burudani ilianza ama kweli wazee walisakata mziki hadi nilishangaa nilidhani ni vijana kumbe wazee




Bukoba

WAZEE wamashauriwa kutojihusisha na masuala ya siasa na badala yake watafute mbinu mbadala ya kujikwamua kimaisha ili kukabiliana na hari ya ugumu wa maisha ili kuhepuka na suala la kuwa ombaomba katika maisha yao ya kila siku.

Ushauri huo umetolewa na afisa maendeleo ya Jamii Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera Mrisho Issa kwaniaba ya Mkurugenzi wa Manispaa hiyo wakati wa kufungua tawi la Saidia Jamii ya wazee Kagera(SAJAWAKA)  tawi la kata ya Kahororo katika manispaa hiyo ambalo limeanzishwa kwa ajili ya kusaidia wazee.

Alisema kuwa wazee wanapofungua vikundi kama cha (SAJAWAKA) wajue malengo yake na wala wasijihusishe na masuala ya siasa kwani wakati  wa kushabikia  mambo ya siasa uwe nje ya vikundi ambavyo vinatambulika kisheria.

Aliongeza kuwa vipo vikundi vingi vinaanzishwa lakini malengo ambayo wanakuwa wamakusudia luyafanya hawayafanyi na badala yake wanajikuta wameanza kushabikia mambo ya kisiasa nalengowanalokuwa wamekusudia kulifanya halifanyiki.

Katika hatua nyingine alisema kuwa pamoja na kufungua tawi la wazee bado kuna changamoto kwa wazee kutopata huduma ya afya bure hasa wale wanao anzia umri wa miaka 60 na kuendelea kama sera ya wizara husika inavyosema.

Aliongeza kuwa Hospitari nyingi bado jambo hilo hawalitilii maanani na kusababisha usumbufu kwa wazee ambao uwezo wao ni mdogo na kujikuta hawapati huduma ya matibabu bure .

Nae Mwenyekiti wa tawi la Saidia jamii ya wazee Kagera tawi la kata kahororo Silivandi Muyoza alisema kuwa kikundi hicho kina jumla ya wazee 104 na wanatarajia wapewe matibabu bila kudaiwa changizo za tiba kama sra ya wizara ya afya inavyosema na wamepatiwa vitambulisho maalumu vya Chama cha wazeeTanzania (CHAWATA).

Aliongeza kuwa wazee wanatarajia pia kutolipa kodi za viwanja na nyumba zao zisizozalisha biashara kama mwanzo ambapo waliwa wakilipa kodi hizo huku wengine wakiwa na uwezao mdogo.

Aidha alisema kuwa kikundi hicho hakikuanzishwa kwa lengo la siasa na badala yake ni kwa ajili ya kusaidia wazee kimaendelea kwa kubuni mirani mbalimbali ya kuwasaidia katika umri wao wa uzeeni.

Mwisho


Wednesday, June 20, 2012

Rais Kikwete akutana na Viongozi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na shirika la nyumba mjini Dodma


Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mkutano na viongozi wa mifuko ya hifadhi ya Jamii na Shirika la Nyumba la taifa ikulu mjini Dodoma leo.Katika kikao hicho Mheshimiwa Rais aliwapa changamoto viongozi hao  kuunganisha nguvu na kubuni mikakati itakayowezesha kuwapatia watumishi wa umma nyumba za kuishi. PICHA NA FREDDY MARO
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisisitiza jambo wakati akiongea na mkurugenzi mkuu wa PPF Bwana William Eriyo mjini Dodoma leo baada ya kikao maalumu na viongozi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na shirika la Nyumba .
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na shirika la Nyumba la Taifa mara baada ya kikao maalumu kilichofanyika ikulu mjini Dodoma leo. viongozi Wengine waandamizi w aliohudhuria kikao hicho Naibu Waziri wa Ardhi Goodluck ole Medeye(watatu kushoto),Katibu Mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue(Wanne kushoto),Gavana wa Benki Kuu Professa Beno Ndulu(kulia) na naibu katibu Mkuu Hazina Dr.Servacius Likwelile(kushoto). Katika kikao hicho Mheshimiwa Rais aliwapa changamoto viongozi hao  kuunganisha nguvu na kubuni mikakati itakayowezesha kuwapatia watumishi wa umma nyumba za kuishi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC Bwana Nehemiah  Mchechu mara baada ya kikao maalumu kilichofanyika ikulu mjini Dodoma leo(picha na Freddy Maro)
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dr.Ramadhani Dau akiteta Jambo na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu mjini Dodoma jana.

Magazeti Magazeti
















Reactions::