Mnara wa kumbukumbu ya abiria waliopoteza maisha uliopo eneo la Igoma Jijijini Mwanza.
Kwa Hisani ya Bukoba Pamoja Blogspot
LEO
ikiwa ni kumbukumbu ya miaka kumi na sita tangu kuzama kwa meli ya Mv
Bukoba,baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Kagera wamehoji utekelezaji wa
ahadi ya Rais Kikwete ya ununuzi wa meli mpya.
Meli
ya Mv Bukoba ilizama May 21,1996 na kusababisha vifo vya zaidi ya watu
mia tisa,ambapo wakati wa kampeini za uchaguzi Mkuu mwaka 2010 Rais
Kikwete alihaidi ununuzi wa meli mpya kama mbadala wa meli iliyozama.
Wakihojiwa
kwa nyakati tofauti juu ya kumbukumbu ya tukio hilo baadhi ya wananchi
wamesema hawajaona juhudi zozote za utekelezaji wa ahadi hiyo na kuwa
tangu wakati huo usafiri wa majini umezorota.
Mmoja
wa wananchi hao Selestine Mwebesa mkazi wa kijiji cha Ruhunga wilaya ya
Bukoba alisema mbali na kupoteza ndugu mmoja katika ajali hiyo,hakuna
jitihada zozote zinazoonekana katika utekelezaji wa ahadi ya rais
Kikwete.
Alisema
utekelezaji wa ahadi hiyo haupashwi kuchelewa kwani kuzama kwa meli ya
Mv Bukoba iliongeza pengo la usafiri kati ya wananchi wa Mkoa wa Kagera
na Mkoa wa Mwanza.
Pia
mwananchi mwingine Pontian Kaiza mkazi wa Kijiji cha Kibeta nje kidogo
ya mji wa Bukoba alisema pamoja na ahadi ya meli mpya kuonekana imewekwa
kando,pia alidai kuna malalamiko mengi ya wananchi ambao hawakupata
kifuta machozi kama kilivyodaiwa kutolewa na serikali.
Alisema
mmoja wa jamaa zake aliyemtaja kwa jina la Joseph Peter ambaye
alimpoteza mke wake katika ajali hiyo ni miongoni mwa wananchi wengi
ambao hawakupata kifuta machozi kilichotolewa huku wengine wakilalamikia
kiwango kidogo walichopewa.
Mmoja
wa wananchi waliopona katika ajali hiyo David Mtensa mkazi wa mjini
Bukoba wakati wa kumbukumbu ya tukio hilo mwaka jana alinukuliwa
akiilalamikia Serikali juu ya kiwango kidogo cha fedha zilizotolewa kwa
waathirika wa ajali hiyo.
Alidai
kiasi cha shilingi laki moja kilichotolewa kwa abiria aliyenusurika na
laki tano waliopoteza ndugu hakikulingana na madhara waliyopata kwa
kuzingatia kuwa baadhi yao walikuwa wafanyabiashara waliolazimika kuanza
upya.
Miongoni
mwa ahadi nyingi alizozitoa Rais Jakaya Kikwete wakati akitafuta muhura
wa pili wa uongozi ni ununuzi wa meli mpya,ambapo mpaka sasa hakuna
jitihada za wazi zinazoonekana juu ya utekelezaji wa ahadi hiyo.
No comments:
Post a Comment