Friday, March 2, 2012

WANANCHI WAMTAKA MBUNGE WAO WA ZAMANI KUACHIA ARDHI

Na Mwandishi wetu Muleba.
WANANCHI wa kata ya Katoke tarafa Izigo wilayani Muleba mkoani Kagera wamemtaka mbunge wa zamani wa jimbo la muleba Kaskazini Ruth Msafiri CCM, kuachia eneo la ardhi lenye hekari 40 ikiwemo jengo la shule ya sekondari ya kata hiyo ambalo mbunge huyo wazamani analimiliki kinyume cha sheria.

Wananchi wamesema hayo katika mkutano wa kijiji ambao ulifanyika kijiji cha Katoke na kutoa maazimio kwamba mbunge huyo wa zamani amejimilikisha eneo ambalo ni la kijiji na kudai kuwa aliuziwa na uogozi wa serikali ya kijiji iliyopita.

Akizungumza katika mkutano huo mmoja ya wananchi hao ambaye kipindi cha nyuma alikuwa mwenyekiti wa kijiji cha Katoke Andesoni Ngililea alisema kuwa mnamo tarehe 18 mwezi wa 3 mwaka 2009 Ruth Msafiri akiwa mbunge wa jimbo hilo alikutana na uongozi wa serikali ya kijiji na kuwapa wazo la kuazisha shule ya sekondari ya serikali ya wazichana.

"Tulimkubalia na kutenga ardhi ya kijiji kwakuwa tuliona itasaidia kupunguza tatizo la mimba kwa wasichana ambao wanasomea shule za mbali kwani shule hiyo ingekuwa ya bweni na ikimilikiwa na wananchi wa kata Katoke "alisema Ngililea

Aliongeza kuwa kwa wakati ule michango mbalmbali ilikusanywa wananchi walichangia kwa harambee,michango mingine walipewa na rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete,vile vile Benki ya NMB tawi la Muleba nayo ilitoa mchango wake na fedha ya mfuko wa jimbo ilikuja kwenye kijiji ili kufanikisha shule ya wananchi.

Aliongeza kuwa baada ya muda wa uchaguzi wa kura za maoni kufika wa Chama Cha Mapinduzi wa mwaka 2010,mbunge huyo alishindwa katika uchaguzi huo mara baada ya kushindwa aliendelea ujenzi kwa kushirikianana wananchi baada ya muda aliwageuka wananchi wa Kijiji hicho na kudai kuwa shule hiyo ni mali yake na sio ya serikali ya kijiji.

Kwa upande wake mwenyekiti wa mkutano huo Eliasi Juma aliwataka wananchi kutokubali kuchukuliwa shule yao likiwemo eneo husika kutokana na kata hiyo kutokuwa na shule ya sekondari ya kata na kuwataka wananchi wasichangie ujenzi wa shule kwakuwa shule yao ipo lakini mtu mmoja ndio anaikatalia.

Alisema pia Mbunge huyo wa zamani anae katalia eneo hilo amesema wananchi hawana shule eneo lile na shule hiyo inaitwa Ruth Blasio Msafiri Girls Sekondari School wala sio Katoke Sekondari School kama wananchi wanavyodai.

No comments:

Post a Comment