Na Mwandishi Wetu
Karagwe
OFISA mkuu wa taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa (TAKUKURU) wilayani Karagwe
mkoani Kagera anatuhumiwa kwa kujihusisha na kudhohofisha kesi ambayo
inawakabili watu ambao ni raia wa nchi jirani ya Rwanda ambao
wanabiliwa na kesi ya wizi wa ngombe 36 walioibiwa mwezi
september 2 mwaka 2010 kata Ihembe wilayani Karagwe.
Akizungumza
na waandishi wa habari wilayani Karagwe Gozibath Blandes ambaye ni
mfugaji wa kata ya Ihembe na ndie aliyeibiwa ngombe hao alisema kuwa
ofisa huyo ambaye anaitwa Onesphor Ajinasi anajihusisha na kesi ambayo
haimuhusu kwa kuwatishia wapelelezi wa kesi hiyo wakiwemo mashahidi kwa
upande wa mashtaka.
Blandes ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Karagwe (CCM) alisema kuwa hadi hivi sasa kesi hiyo
inayoendelea katika mahakama ya wilaya ya Kayanga inaedelea kusikilizwa
na mashahidi wanne kwa upande wa mashtaka wametoa
ushahidi wao, lakini alisikitishwa na vitendo vya ofisa wa Takukuru
kutaka kuingilia uhuru wa mahakama.
Aliongeza kuwa watuhumiwa
ambao wanahisika na wizi wa ngombe zake sio Watanzania ni wanyarwanda na
aliwataja kwa majina ya Rusagara Geofrey(33) mfanyakazi katika mamlaka
ya mapato nchini Rwanda,Joramu Sebatwale(47) na Ndamaji Anacleth (66)
ambao wote wanahusika na vitendo vya wizi.
Aidha aliongeza kuwa
ngombe hao walikamatwa mnamo tarehe 5/4/2011 katika eneo la Kasulo
wilayani Ngara eneo ambalo walikuwa wamefichwa mara baada ya kuibiwa na
raia hao wa Rwanda.
"Kwakweli bado inasikitisha kuona mtumishi wa
serikali tena kitengo muhimu anaigilia sehemu ambayo hausiki nayo ili
kuharibu kesi ambayo ahusiki nayo tena kibaya zaidi anaweka kesi za
kubumba kwa wale wote wanasaidia wakiwemo wapelelezi kutoka jeshi la
Polisi ambao siwezi kuwataja inabidi mamlaka husika kumuangalia huyo
mtumishi wao"alisema Blandesi.
Aliongeza kuwa
wananchi wa wilaya hiyo wanakabiliwa na tatizo la wizi wa ngombe kutoka
kwa wavamizi wa nchi jirani jambo ambalo linawaathiri wafugaji
wadogowadogo.
Aidha taarifa ambazo ziliwafikia waadishi wa habari
zinasema kuwa ofisa huyo wa Takukuru wilaya amekuwa akiwaambia baadhi
ya wananchi kuwa atahakikisha anawafuatilia wale wote wanajihusisha na
kesi hiyo na ikiwezekana anawawekea mitego ya rushwa ya kutegeshea.
Jitihada
za kumtafuta ofisa huyo zilishindikana kwa kuambiwa kuwa akuwepo katika
eneo la kazi na kwamba yuko mbali na wilaya hiyo nakuambiwa kuwa suala
hilo anaweza kulizungumzia kamanda wa Takukuru mkoa.
Akizungumzia
suala hilo Kamanda wa Takukuru Mkoani Kagera Domina Mkama alisema kuwa
taarifa ambazo zinatolewa juu ya mtumishi wake azina ukweli ndani yake
bali ni kikundi kidogo cha watu ambao wanachunguzwa au waliwahi
kuchunguzwa na taasisi hiyo na wanataka kuijengea chuki Takukuru.
Alisema suala
la kesi ya wizi wa Ngombe analifahamu kwani iko mahakamani kwa hiyo kesi kama sio ya Takukuru ni
vigumu ofisa yoyote kuingilia kwaiyo huyu ofisa wake hana mamlaka ya
kuingilia kesi isiyo muhusu,hizo ni chuki za baadhi ya watu na jambo
hili halipo.
Mwisho
No comments:
Post a Comment