aibu Waziri wa Ujenzi Dk. Harrison
Mwakyembe, akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es
Salaam jana, muda mfupi baada ya kuingia ofisini humo kuanza kazi,
kutokana na afya yake kuimarika. Mwakyembe amekuwa akitibiwa nchini
India kwa muda mrefu. Picha na Zacharia Osanga
BAADA ya utata wa muda mrefu wa ama Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison
Mwakyembe amelishwa sumu au la, jana Mbunge huyo wa Kyela, aliweka
hadharani ugonjwa wake akisema unafahamika kitaalamu kwa jina la Popular
Scleroderma huku akisisitiza: “Sasa nimepona kabisa.”Dk Mwakyembe
amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya ngozi ambayo mwaka jana yalizidi
kumtikisa na Oktoba 9, Serikali iliamua kumpeleka Hospitali ya Appolo,
India kwa ajili ya matibabu na uchunguzi zaidi.Akizungumza na waandishi
wa habari ofisini kwake Dar es Salaam jana, Dk Mwakyembe akiwa
amevalia kofia ya pama alisema: “Si kwamba sijambo, bali nimepona
kabisa baada ya kugundulika na maradhi hayo na kutibiwa.”“Nimerudi juzi
kutoka India na daktari wangu ameniambia nimepona, nilikuwa
nasumbuliwa na maradhi ya ‘Popular Scleroderma’ iliyosababisha ‘skin
disorder’ (ngozi kutokuwa katika hali ya kawaida), lakini kwa nguvu za
Mungu nimepona, namshukuru Mungu.”Kuhusu sumu
Alipoulizwa kuhusu tuhuma za kulishwa sumu, Dk Mwakyembe alikataa
kuzungumzia hilo akisema anasubiri uchunguzi ulioagizwa na Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha.Hata hivyo, Dk Mwakyembe
alisema angependa kuona uchunguzi huo unakamilika haraka na ripoti yake
inatangazwa kwa umma.Alisema yuko tayari na anasubiri tume hiyo ya
uchunguzi iliyoundwa na Waziri Nahodha imhoji ili atoa kile kilichomo
katika ripoti ya daktari wake.Dk Mwakyembe alisema anachoshukuru hadi
sasa ni kwamba afya yake imeimarika kutokana na shinikizo la Rais
Jakaya Kikwete ambaye aliagiza Serikali kumpa kipaumbele wakati wote
akiwa nchini na India hatua ambayo imemwezesha kufika hapo
alipo.Kutokana na hali hiyo, Dk Mwakyembe aliwataka wananchi wote
wakiwemo wa jimboni kwake Kyela kuondoa wasiwasi akisema sasa yupo
imara kwa ajili ya ujenzi wa majukumu ya taifa.“Ninaomba wapiga kura
wangu wa Kyela waache jazba, wawe na subira juu ya matatizo yangu. Wiki
ijayo nitakwenda kuzungumza nao ili niweze kuwaeleza matatizo
yaliyokuwa yananisumbua, lakini sasa hivi niko fit,” alisema.
SOMA ZAIDI:http://www.mwananchi.co.tz/habari/-/21277-dk-mwakyembe-aweka-hadharani-ugonjwa-wake
No comments:
Post a Comment