Tuesday, March 20, 2012

Wananchi mkoani Kagera Wanufaika na Ranch ya Taifa

Moja ya ngombe jamii ya Kongwa wakiwa katika malisho ndani ya ranch za taifa mkoani kagera hapa ni Ranch ya Kagoma Wilayani Bukoba

Na Antidius kalunde
Kagera


JAMII ya wafugaji wadogowadogo mkoani Kagera,wamepongeza uhamuzi wa mamlaka ya ranchi za taifa zinazojishughulisha na ufugaji wa ng'ombe,kwa kuwanufaisha kwa njia ya kutoa elimu ya ufugaji ulio bora ba wa kisasa.

Wakiongea na waandishi wa habari,wafugaji hao walisema utaratibu unaoendelezwa na kampuni za ranchi za Taifa(NARCO)zilizo Kagoma,Kikurula,Missenyi na Mabare ni mzuri na wenye malengo ya kumuinua mfugaji na mkulima ili kuondokana na umasikini.

Mmoja wa wafugaji hao John Muganyizi(47)mkazi wa wilayani Karagwe,alisema kuwa pamoja na baadhi ya wafugani wengine katika maeneo mbalimbali mkoani Kagera walikuwa na ujuzi wa kujiendeleza kiufugaji lakini utaratibu wa ranchi hizi ni mzuri zaidi kwani ni njia mbadala ya kumuelimisha mwananchi atambue umuhimu wa ufugaji na kilimo.

Muganyizi alisema kuwa awali hali ya ufugaji kwa wakulima ilionekana kukumbwa na changamoto kubwa ususani namna mbalimbali za kukabiliana na magonjwa ya mifugo,kubaini mbegu bora za ng'ombe zinazofaa katika ufugaji,lakini atua za ranchiNARCO kupisha utaratibu huu,ni dalili kuu inayoonesha kuwa serikali bado haijamsahau mfugaji wa taifa hili.

Alisema kwakuwa NARCO imeamua kuwapatia mafunzo wafugaji,ni vyema wakazi wa mkoa wa Kagera kuchangamkia fursa hii kwani ni muhimu na kwa kuelimika juu ya ufugaji janga la umasiki litapungua kwa kiasi kikubwa sana.

Tarsis Mawala ni meneja wa ranchi ya Missenyi,anasema utaratibu wa kutoa elimu ya ufugaji kwa wafugaji ni mojawapo ya majukumu ya NARCO hivyo ni mwendelezo wa mipango ya kampuni na ipo kwa kila mpango mkakati wa ranchi mkoani Kagera.

Mawala amesema pamoja na kutoa elimu pia ranchi hizo za Kagoma,Missenyi na Kikurula utoa mbolea kwa wakulima wa vijijini kwa bei nafuu sana,na kwa kufanya hivyo urahisisha ushughuli za ranchi na kujenga mahusiano kwa wananchi.

Alingeza kuwa hata hivyo kamppuni hizo ukabiliwa na baadhi ya changamoto nyingi mmojwapo ikiwepo uchomaji mbuga hovyo na kuwepo wanyama wakali maeneo ya ranchi kama tembo katika ranchi za Kagoma na Kikurula ambavo uhataarisha maisha ya watumishi wa ranchi na mifugo.

MWISHO


No comments:

Post a Comment