TIMU ya
wataalam wa mpango wa tathimini ya utendaji kazi kwa nchi za Afrika (APRM)
imeisifia Tanzania
kwamba ni hazina kubwa katika suala zima la utawala bora katika nchi za Afrika
na duniani kote.
Profesa
Aderic Nade kutoka nchini Nigeria ambaye pia ni mmoja wa wajumbe wa timu hiyo
kati ya 21 wanaounda timu hiyo alibainisha
hayo jana katika mkutano wa siku
moja uliofanyika mjini Bukoba kati ya wadau wa utawala bora na tume hiyo ya
APRM kutoka makao makuu.
Prof.
Nade
ambaye pia ni mhadhiri katika chuo kikuu cha Lagos kilicho nchini
Nigeria,alisema kuwa pamoja na changamoto mbalimbali zinazoikabili
Tanzania lakini
imekuwa ni kisiwa cha nchi nyingine kuja kujifunzia jinsi gani
wanavyoilinda
amani yake ikiwa ni sambamba na misingi ya utawala bora inayodumishwa
kwa wananchi
wake.
Alisema
lengo la mkutano huo na dhamila kubwa ya tume ni kuangalia mchakato mzima wa
utawala bora katika nchi hii,historia
na masuala mazima yanayopelekea utawala bora ulioko Tanzania ulivyoimalika
leo na hata kabla ya uhuru.
Alieleza
kwamba umuhimu wa kuwepo APRM ni kuhakikisha Afrika inarudi katika mustakabali
wa utawara bora ambapo hari hiyo itajenga misingi mipya ambayo itaegemea katika
kujadiri mkataba wa kijamii kati ya Serikali na wadau,Serikali na Raia pia
kuweka misingi mipya ya mahusiano kati ya Watu wa Afrika.
Alisema
kuhusu suala la demokrasia katika nchi
za Kiafrika ni jambo muhimu ambalo ni ndoto ya nchi za kiafrika wanayohitaji
kuipata kwahiyo ni haki ya Raia kuuliza Serikali ni mambo gani inapswa kufanya
na kama imefanya imefikia malengo yapi.
Alisema malengo
mengine ni kuhakikisha pale jambo linapotokea katika nchi moja wapo katika
Afrika lionekane kuwagusa Waafrika wote ambapo aliongeza kwamba hari hiyo
haikuanza leo bali ilianzishwa na waasisi wa Afrika ambao ni baba wa Taifa
Mwalimu Julius Kambalage Nyerere,Kwame Nkuruma na Keneth Kaunda.
Alisema
kuwa tathimini hii ni endelevu ambapo kila baada ya miezi sita wadau watatakiwa
kukaa na kutathimini ambapo kila nchi itatakiwa kutoa taarifa jinsi gani
imetekeleza mawazo ambayo yaliibuliwa na wadau na kila baada ya miaka mine timu
itafanya tathimini juu ya utawala bora pamoja na uendelevu katika nchi za
Afrika.
Kwa upande
wa mgeni rasmi katika mkutano huo ambaye pia ni katibu tawala wa mkoa wa Kagera
Nassor Mnambila kwa niaba ya mkuu wa mkoa huo kanal mstaafua Fabiania Massawe
alisema kuwa pamoja na mafanikio hayo ya Tanzania kuwa hazina katika utawala
bora bali zipo changamoto zinazowakabili kama Serikali.
Mnambila
alisema kuwa changamoto hizo ni mauaji ya vikongwe na walemavu wa ngozi
(albino) kwa sababu ya imani za kishirikina,ukeketaji kwa watoto wa kike,ujambazi,ukatili
wa kijinsia kwa wanawake na ukatili kwa watoto hawajapata uwakilishi wa kutosha
katika masuala ya kisheria ambapo amesema kuwa hayo ni baadhi ya changamoto
ambazo Serikali inaendelea kupambana nazo.
mwisho
No comments:
Post a Comment