Tuesday, March 20, 2012

MCHUNGAJI ANYANGANYWA WANAFUNZI BUKOBA VIJIJINI

Na.Kibuka Prudence,Bukoba Vijijini

HALMASHAURI ya wilaya Bukoba mkoani Kagera,imefikia uamuzi wa kutoa watoto waliokuwa wakipata malezi kutoka kwa mchungaji kutokana na kudaiwa kukiukwa na baadhi ya mashariti ya malezi.

Hatua hiyo iliyochukuliwa na halmashauri Machi 17 chini ya idara ya maendeleo ya jamii,imekuja baada ya madai kuwa mlezi aliyekuwa akiwajibika kuwalea watoto hao 37 wakiwa wa kike 12 na kiume 25 alishindwa kufuata baadhi ya masharti yanayopaswa kufuatwa wakati wa malezi ya mtoto.

Mmoja wa maafisa wa idara hiyo waliohusika katika kuamisha watoto hao kutoka kituo cha malezi cha Kaagya Ophans Care Center na kuwaamisha kituo cha Kabilizi kilicho chini ya idara hiyo kata Rubale,bi.Renatha Mshwaili,alisema halmashauri imefikia maamuzi hayo ili kuepusha mtoto na matatizo mengine yanayoweza kumsababishia madhara ya kiafya.

Mshwaili alisema kuwa awali walibaini kuwepo matatizo mbalimbali yaliyokuwa baiona ya  mlezi wa kituo hicho ambaye ni mchungaji wa kanisa la Christian Life Church Cleoper Kaijage na mfadhili wa kituo hicho ambao ni shirika la The Mighty Fortress lenye makazi yake nchini Uholanzi.

Alisema baada ya mfadhili kudai kuwa hakubaliana na utawala uliopo na kuomba halmashauri kuchukua maamuzi juu ya walengwa(watoto)idara yake ilifikia maamuzi ya kuwanusuru watoto kwa mpango maalumu wa kujali usalama wa mtoto huku atua nyingine zikifuatwa.

Hata hivyo,kwa upande wake mlezi wa kituo hicho,mchungaji Kaijage,alikiri kutokubaliana na mfadhili wake kwa kile alichodai kuwepo baadhi ya wajumbe waliwai kufukuzwa ndani ya bodi ya kituo kumchonganisha mfadhili dhidi yake kwa maslahi ya kutaka utawala.

Mchungaji Kaijage aliswema kuwa japo kituo hicho kilikuwa kikipata ufadhili kutoka kwa shirika husika,lakini ufadhili ulimkuta tayari ameanza kutoa msaada kwa walengwa hao.Ambapo wazo la kuanzishwa kituo hicho lilianza tangu mwaka 2004 na mwaka 2005 alianza kutoa msaada wa malezi kwa watoto 12.

Alisema malezi hayo yaliendelea kutolewa kituoni hapo mpaka 2008 hini ya bodi ya kituo hicho,na tayari alikuwa amejenga majumba mawili japo yalikuwa ya udongo lakini lengo kuu lilikuwa ni kuwanusuru watoto wanaoishi katika mazingira magumu,ambao walickuliwa kutoka maeneo ya mwalo wa Igabilo na sehenmu nyingine.

Alisema msaada wa shirika ulianza kutolewa mnamo mwaka 2008 wakiwa na watoto 15,ambapo mfadhili alikubali kuwafadhili watoto kwa kuboresha nyumba na kutoa dola 20 kwa ajili ya chakula na matumizi mengine,jambo ambalo uongozi uliamua kulima ili kujipatia chakula na fedha hizo zikagharamikie huduma za kuwapatia elimu katika mashule mbalimbali.

Aidha,mchungaji huyo anadai kuwa anashangazwa na uamuzi wa halmashauri kumwamulisha ahame kituoni hapo kwa kuelekezwa na wafadhili,kwani yeye aende wapi wakati hapio alipo ndiyo kwake na kuiomba serikali kuchunguza kwanza na kubaini ukweli ulivyo kabla ya maamuzi mengine.

Alibainisha kuwa tayari ameanza kuchafuliwa kwa maneno ya kashifa kuwa anawanyanyasa watoto jambo ambalo ni la kupandikizwa na alishakamatwa na kukaa rumande kwa siku 15,japo tayari kesi dhidi ya madai yote yanayo muguza ipo mahakamani.

MWISHO

No comments:

Post a Comment