Saturday, March 24, 2012

POLISI AUWAWA KINYAMA NA KUPORWA BUNDUKI

Kamanda wa polisi mkoani kagera Henry Salewi akizungumza kuhusiana na matukio mbalimbali




Bukoba

WATU wasijulikana wamemuuwa askari polisi kwa kumpiga kichwani na moko ambacho ni kifaa cha kuchimbia madini kwa wachimbaji wadogowadogo  kisha wakatoweka na bunduki aliyokuwa nayo aaskari huyo aina ya SMG katika mgodi wa Tulawaka wilayani Biharamulo mkoani Kagera.

Kwa mujibu wa kamanda wa Polisi mkoani Kagera Henry Salewi amewaambia waandishi wa habari kuwa tukio hilo lilitokea jana majira ya saa kumi na moja jioni ambako askari huyo akiwa na wenzake watatu walikuwa katika doria ya kulinda eneo la mgodi huo.

Kamanda Salewi Alimtaja kwa jina ni Namba G.2626 PC Diksoni mwenye umri wa miaka 29 mzaliwa wa Sumbawanga mkoani Katavi.

Aliongeza kuwa wauwaji hao walikuwa na nia ya kupora bunduki kwa ajili ya kufanya uharifu na inasadikiwa ni wachimbaji wadogo wadogo ambao upenda kuindia katika mgodi wa Tulawaka kufanya vitendo vya uharifu.

Aidha alisema kuwa askari wengine watatu ambao walikuwa na marehemu wakiwa doria walishangaa kuona mwenzao haonekani ndipo walianza kumtafuta na kumkuta tayari amekufa na akiwa hana bunduki aina ya SMG kwa kila askari anakuwa na eneo lake la kulinda katika pori lililozunguka mgodi.

Mwili wa marehemu umesafirishwa kuelekea mkoani Katavi wilaya ya Sumbawanga ili kuweza kufanyika taratibu za mazishi na ameacha mjane..


Kamanda Salewi alisema kuwa juhudi za kuitafuta bunduki zinaendelea katika eneo la Tulawaka ikiwemo maeneo ya karibu na eneo hilo na ametoa wito kwa wananchi wa wilaya ya Buharamulo kutoa taarifa endapo watabaini kuiona bunduki hiyo ya kivita.

No comments:

Post a Comment