Friday, March 2, 2012

CCM WATAKIWA KURUDISHA HESHIMA KWA WANANCHI WAKE


Na Mwandishi Wetu
Bukoba

VIONGOZI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Kagera wametakiwa kuhakikisha wanarudisha heshima ya chama hicho kama kilivyokuwa kinaheshimika chama cha TANU, kutokana chama hicho kinachoshikilia serikali  kuingiliwa na watu ambao hawana sifa za kuwa wanachama.

Akizungumza katika kata ya Bilele mjini Bukoba na wanachama  wa CCM mlezi wa chama hicho mkoani Kagera ambae pia ni mbunge wa jimbo la Peramiho Jenesitha Mhagama alisema kuwa kadili siku zinavyokwenda wananchi wanakosa imani na CCM kutokana na kuingiliwa na watu wasiokuwa waaminifu.

Alisema kuwa kwa hivi sasa viongozi wa CCM wajitahidi kufichua watu ambao wanaonekana kuwa hawana uwezo wa kuongoza na wale ambao wanaonekana kutanguliza maslahi yao mbele tofauti na chama.

"Chama kinazidi kuyumba kila kukicha kutokana na watu wachache lakini tukumbuke kuwa wakati wa TANU watu walikuwa na imani na viongozi wake waliokuwa wanaiongoza lakini hivi sasa kuna tatizo la watu wachache kuendelea kutuvuruga inabidi hawa watu tuwakatae na tusiwape nafasi kwenye chama chetu"alisema Mhagama.

Katika hatua nyingine aliwashauri wazazi kuwapa elimu vijana juu ya kulinda amani ya Tanzania kwani wao ndio wanaweza kusababisha machafuko kwenye nchi kutokana kuwa na kundi kubwa la vijana na wengi wao hawako katika ajira rasmi.

Alisema kuwa ni haki ya kila mtu kudai haki yake ya msingi kutokana na ugumu wa maisha lakini kuna haja ya kuangalia na ni jinsi gani unadai haki kwani vijana wengi wanadai kwa kuonyesha uvunjifu wa amani.

Alisema pia amani ambayo iliachwa na viongozi waasisi wa nchi hii inabidi ilindwe ili kuweza kujihepusha n machafuko yanayoweza kutokea endapo amani ikivulugwa na kushauri wananchi wasikubali kurubuniwa na baadhi ya wanasiasa wachache.

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoani Kagera Costansia Buhie ambaye pia ni mjumbe wa kamati kuu ya chama cha mapinduzi CC alimhakikishia mlezi huyo kuwa watahakikisha wanarudisha imani kwa wananchi ambao wanakata tama na chama hicho.

Aliongeza kuwa wale ambao wanataka uongozi kwa maslai yao chama hakitawafumbia macho na kuhakikisha wanawatoa katika nafasi watakazo kuwa nazo kiuongozi

MWISHO

No comments:

Post a Comment