Friday, March 23, 2012

TEMBOTEMBO JAMANI WANAWASUMBUA WANA BUKOBA VIJIJINI

Na.Kibuka Prudence,Bukoba Vijijini

SERIKALI imeombwa kuweka mpango mkakati wa kupambana na wanyama waharibifu na kuwatoa katika mazingira wasipostairi ili kuepusha gharama nyingi za fidia zinazosababishwa na wanyama hao.

Rai imetolewa na baadhi ya wananch wa vijiji vya Ombweya na Kikagati vilivyoko katika kata ya Izimbya wilayani Bukoba vijijini,mara baada ya kufanya maojiano na waandishi wa habari waliofika maeneo hayo yanayodaiwa kukidhiri na kuwepo wanyama aina ya ya Tembo.

Bw.Januari Abdalla(35)mkulima wa maeneo hayo,alisema kuwa wanyama jamii ya Tembo ufanya uharibifu wa mazao ya wananchi kutokana na kutoka katika hifadhi ya Taifa Burigi iliyoko wilaya za Muleba na Buharamulo.

Abdalla alisema kuwa vitendo vya Tembo kuvamia makazi ya wananchi si jambo geni kwa wakazi hao,kwani ni kila mara wanyama hao ufanya uharibifu wa mali za watu na kuvunja vunja makazi yao,jambo ambalo ufanya wakazi husika kuishi kwa mashaka.

Bw. Bonifasi Rwegila ni meneja wa ranchi ya Taifa (NARCO)ya Kagoma iliyoko katika wilaya ya bukoba vijijini,alibainisha kuwepo na kushamili vitendo vinavyotokana na uvamizi wa wanyama hao.

Rwegila alisema kuwa wanyama hao ni hatari kwa maisha ya watu hususani watumishi ndani ya ranchi na wananchi jirani na ranchi hiyo,ambapo Tembo hao ufika mara kwa mara maeneo ya ranchi na kuharibu mazizi ya ng'ombe na majumba ya watumishi wa ranchi.

Alisema kuwa hali hiyo usababisha watumishi katika ranchi hiyo kuishi kwa tahadhari kubwa kwani mbali na kuvunja mazizi ya mifugo,Tembo pia ni hatari kwa maisha ya watu.

Meneja huyo wa Kagoma ranchi,alisema ni vyema serikali kupitia halmashauri za wilaya kuweka mpango maalumu ambao ni kwa ajili ya kufukuza wanyama hao mbali na maeneo ya watu kuliko kuendelea kufanya uharibifu ambao gharama uwa kubwa sana.

Alisema kuwa gharama za uendeshaji shughuli za ranchi ni kubwa mno,ikizingatiwa baadhi ya vitu kupandaa kwa bei madukani hivyo ni hasara kubwa pale inapotokea Tembo kuvunja mazizi ya mifugo wakati hali ya kiuchumi ni duni ambavyo wakati mwingine usababisha hata shughuli za uendeshaji kukwama.

Hata hivyo,pamoja na kusababisha gharama za uendeshaji wa ranchi kuwa kubwa,Meneja huyu alisema hali ya wasiwasi juu ya maisha yao kutokana na kuwepo na Tembo katika mazingira hayto,pia usabnabisha kufanya shughuli za kuvuga kwa roho mkononi,na kusababisha kuzorotesha ufanisi wa malengo yaliyokusudiwa.

Kero ya Tembo imekuwa ikilipotiwa mara kwa mara kwa wananchi wanaoishi maeneo ya kata za Izimbya na Kibirizi ingawa halmashauri ya wilaya Bukoba kupitia kitengo cha mali asili na Uvuvi, imekuwa ifanya utaratibu wa kuwafukuza wanyama hao na kuwasogeza mbali na maeneo wanamoishi wananchi,japo tatizo hilo linadaiwa bado kuwa ni kero kwa wananchi kwani kunauharifu mkubwa unaosabishwa na Tembo hao.

MWISHO

No comments:

Post a Comment