JANA KIMEIBUKA KIPINDI KIPYA CHA TV CHA ‘ONGEA NA JANET’
*AITAKA JAMII KUACHA WOGA NA KUJITOKEZA KUONYESHA VIPAJI.
MO BLOG: Nini Theme ya kipindi cha ‘ONGEA NA JANET’..?
JANET: Aah…!!
Theme ya “ONGEA NA JANET’ ni kipindi ambacho kinatoa fursa kwa mtu
yeyote kuja kuongea ili mradi awe na kitu ambacho kinaweza kuilemisha
jamii. Kipindi hiki kinazungumza na watu wa rika zote. Na katika kipindi
hiki kwa kweli mimi nazungumzia kila kitu sijajiwekea limitations.
Lengo ili tufike mahali tuweze kuzungumza hata yale mambo ambayo watu
wanaogopa kuyazungumza hadharani.
Japo
watu wengi wanapenda nizungumzie mambo ambayo yapo current, lakini kwa
mfano yakitokea mafuriko, ukifungua TV zote taarifa za habari
zinazungumzia mafuriko, radio zote ni mafuriko, ukisoma kila gazeti ni
mafuriko na hata misemo mitaani inakuwa kuhusu mafuriko. Sikuona tena
umuhimu wa kuongelea kitu ambacho kinaongelewa kila mahali, nataka kutoa
nafasi ya kuzungumzia mambo ambayo hatupati nafasi ya kuyazungumzia.
Kwa
mfano huwezi kukuta, gazeti au TV ikizungumzia kuwa wanawake walioko
katika ndoa wanapata taabu kwa sababu ya nyumba ndogo, na hata kama
itaandikwa basi inapewa nafasi ndoogo.
Na sifikirii kipindi changu kiishe leo au kesho hiki kitaendelea siku zote.
MO BLOG: Watazamaji watarajie nini kutoka kwako katika siku zijazo..?
JANET: Watarajie
mambo mengi mazuri na kuwa kila siku kipindi kitakuwa na kitu kipya.
Nitakuwa na season 4, hivyo kila season itakuwa tofauti na nyingine.
Mfumo nitakaotumia katika season 1 utakuwa tofauti na nitakaoutumia
katika season 2 na kuendelea.
No comments:
Post a Comment