Friday, March 30, 2012

Tunakukumbuka Mzee Mkapa Ulikuwa Jembe

Wakati watanzania walio wengi wanazidi kulia na maisha magumu huku wengine wachache wakila kuku na bata ,lakini tukilinganishha maisha ta serikali ya awamu ya tatu na ya nne ni tofauti ndio maana wananchi walio wengi wanasema bora Mkapa angerudi kuwa rais wa Tanzania Hali ni mbaya kila kukicha Jamaniii  (Picha ni rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mh Benjamini Mkapa akipungia wana CCM Arumeru)

Rais Kikwete Atoa tuzo Kwa wanahabari

Rais Jakaya Kikwete akiongea na Fili Karashani Mwandishi mkongwe naambaye ameshinda  tuzo ya Maisha ya Mafanikio katika Tasnia ya Habari mwaka 2011, katika tuzo za (EJAT) zilizoandaliwa na Baraza la Habari Nchini Tanzania (MCT) na washirika wake, hafla hiyo inafanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jana usiku , katika picha kushoto ni Mwandishi wa siku nyingi Khamis Ben Kiko.
Rais Jakaya Kikwete akimkabidhi Nevil Meena cheti cha ushindi wa jumla kwa katika tuzo hizo mara baada ya kutangazwa rasmi.
 Katibu Mtendaji wa MCT Bw. Kajubi Mukajanga akizungumza katika hafla hiyo.

Tunajadiliana

Rais Jakaya Kikwete akizungumza na Mkurugenzi wa Makampuni ya IPP Bw. Reginald Mengi walipkutana katika hafla hiyo.PICHA KWA HISANI Ya IKULU

Lowasa Atikisa Arumeru Jana

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowasa akihutubia kwenye Mkutano wa Kampeni za CCM Jimbo la Arumeru Mashariki jana kwenye viwanja vya Kikatiti,Wilayani Arumeru.

Karibu

Mh. Edward Lowasa akiwasili katika mkutano wa hadhara tayari kwa kuhutubia wakazi wa Arumeru jana
picha kwa hisani ya Ahmadi Michuzi

Wednesday, March 28, 2012

Kuna Umuhimu wa Kusema Hapa Ni Wapi

Unaweza ukafikiri Bonge la Uwanja fika mwenyerwe Utaniambia Karibu Bukoba Uwanja wa Ndege

Hi Ni Jadi Yetu na Huku Ndo Kwetuuuuuuuuuu

Leo mapema nilipita asubuhi katika soko la mjini Bukoba na hali ilikuwa hivi kama unavyoziona Ndizi zikisubiri wateja

Serikali Yatangaza Waliochaguliwa Kidato cha Tano

Fredy Azzah
WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, imetangaza majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano mwaka huu, huku idadi yao ikishuka kwa asilimia 13.34 ikilinganishwa na mwaka jana.

Akitangaza majina hayo Dar es Salaam jana, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo alisema kutokana na hatua hiyo, shule nyingi hasa zinazochukua wanafunzi wa mikondo ya sanaa na uchumi, zimekosa idadi ya wanafunzi kama ilivyotakiwa.

“Serikali ilikuwa imetenga nafasi 15,000 za wasichana, lakini waliopatikana ni 9,378 tu, nafasi zilizokuwa zimetengwa kwa wavulana ni 26,000, lakini waliopatikana ni 22,138,” alisema.

Alisema wanafunzi 142 waliobakia, ufaulu wao haukuweza kutengeneza maunganisho yoyote ya masomo, kwa hiyo hawakupangwa kuendelea na masomo ya kidato cha tano.

Mwaka 2010, wanafunzi 352,840 walifanya mtihani wa kidato cha nne, huku 40,388, sawa na asilimia 11.5 wakipata daraja la kwanza mpaka la tatu. Waliochaguliwa kuendelea na kidato cha tano na vyuo vya ufundi walikuwa 36,366.

Mulugo alisema mwaka 2011 wanafunzi waliofanya mtihani huo walikuwa 336,301, huku 33,577 sawa na asilimia 9.98 wakipata daraja la kwanza mpaka la tatu.

“Ufaulu huu umepunguza idadi ya waliochaguliwa kidato cha tano na vyuo vya ufundi kutoka wanafunzi 36,366 mwaka 2011 mpaka wanafunzi 31,516 mwaka 2012. Huu ni upungufu wa wanafunzi 4,850 sawa na asilimia 13.34,” alisema Mulugo.

Sayansi wajitutumua

Waziri Mulugo alisema idadi ya wanafunzi waliopangiwa kusoma masomo ya sayansi imeongezeka hadi kufikia asilimia 53.34 ya wanafunzi wote waliopangiwa kidato cha tano mwaka huu.

“Jumla ya wanafunzi waliopangiwa masomo ya sayansi ni 16,493 ambao ni asilimia 53.34 ya wanafunzi wote waliopangiwa kidato cha tano mwaka 2012. Idadi hii ni kubwa kuliko ya waliopangiwa kusoma masomo mengine,” alisema.Soma zaidi www.mwananchi.co.tz

Tuesday, March 27, 2012

Zitto Kugombea Urais 2015

Aidan Mhando
SIKU moja baada ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema) Zitto Kabwe kutangaza nia ya kugombea urais mwaka 2015, kauli hiyo imewachanganya watendaji wakuu wa chama hicho, Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu Mkuu Dk Willibrod Slaa.

Wakati Dk Slaa akikosoa hatua hiyo na kusema sio wakati mwafaka sasa kuzungumzia urais, Mbowe amesema hana tatizo na Zitto kutangaza nia hiyo sasa kwa kuwa ni haki yake, lakini akahoji haraka ya kutangaza dhamira hiyo.

Hata hivyo, kwa nyakati tofauti viongozi hao wamemshauri Zitto kufuata taratibu za chama kama anataka kufikia malengo yake hayo ya kutaka kuwania nafasi hiyo ya juu kabisa ya uongozi wa taifa.

Kauli ya Dk Slaa
Akizungumzia uamuzi huo wa Zitto kutangaza dhamira hiyo, Dk Slaa alisema suala la urais sio muhimu kwa sasa kwani chama kinaangalia ushindi kwenye uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki.

"Naomba niseme hivi, sasa urais sio ‘issue’ (suala). Chama kinaangalia uchaguzi wa Arumeru Mashariki, muda wa kuzungumzia urais ukifika, tutasema," alisema Dk slaa na kuongeza:

“…Naomba mtambue kwamba tunakabiliwa na suala kubwa la uchaguzi huku Arumeru kwa hiyo sasa siwezi kuzungumzia suala la urais, hili sio wakati wake sasa.”

Hata hivyo alimshauri Zitto kufuata taratibu kama ana nia ya kugombea urais na kufafanua kwamba, chama kina utaratibu wake na ndicho chenye uamuzi wa mwisho.

“Chadema ina utaratibu wake kwa kila jambo, kama Zitto ametangaza kugombea urais 2015 huo ni uamuzi wake binafsi. Lakini mimi kama kiongozi wa chama sioni kama urais ni jambo la kujadili wakati huu.

“Ikifika wakati wakujadili masuala ya urais, tutafanya hivyo kwa undani lakini, sio kwa sasa kwani wakati wake haujafika.”

Mbowe
Kwa upande wake Mwenyekiti Mbowe, alisema kila mtu ana busara na haki zake katika kuamua jambo na hii, ni busara yake Zitto.

Lakini, Mbowe alionyesha kushangazwa na Zitto kutangaza nia hiyo sasa wakati ambao chama kinawaza na kufikiria uchaguzi wa Arumeru Mashariki.

Mbowe alisema haoni tatizo Zitto kutangaza sasa nia ya kuutaka urais kwa kuwa ni uamuzi na haki yake kwasababu kila mwanachama wa Chadema ana haki ya kuamua jambo analolitaka ili mradi afuate taratibu.

“Sioni kama Zitto ana tatizo lolote la kutangaza sasa kwamba mwaka 2015 anataka kugombea urais kwani ni haki ya kila mtu kugombea nafasi hiyo,” alisema Mbowe

Hata hivyo, alifafanua kwamba pamoja na Zitto kutangaza nia, wakati wa kuwania nafasi hiyo ndani ya chama ukifika wanachama wa Chadema ndio watakaotoa uamuzi wa nani anafaa.Soma zaidi www.mwananchi.co.tz

MENEJA WA RANCHI YA KAGOMA NDANI YA MTANDAO

Bw Boniface  Rwegila ambaye ni meneja wa Ranchi ya Kagoma akiwa katika tabasamu kalii mara baada ya kuzungumza nae juu ya maendeleo ya Ranchi husika,akiwa katika ofisi yake iliyopo Bukoba Vijijini

CHAKULA CHA N'GOMBE HUTUMIKA KWENYE KIANGAZI


Moja ya hifadi ya nyasi ambazo ni akiba ya chakula cha n'gombe kinachotumika wakati wa kiangazi katika Ranchi ya Taifa ya Kagoma wilayani Bukoba mkoani Kagera

UMEIPATA HIYO YA TAKUKURU KAGERA

Na Mwandishi Wetu
Karagwe

OFISA mkuu  wa taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa (TAKUKURU) wilayani Karagwe mkoani Kagera anatuhumiwa  kwa kujihusisha na kudhohofisha  kesi ambayo inawakabili watu ambao ni raia wa nchi jirani ya Rwanda ambao wanabiliwa na kesi ya  wizi wa ngombe  36 walioibiwa mwezi september 2 mwaka 2010 kata Ihembe  wilayani Karagwe.

Akizungumza na waandishi wa habari wilayani Karagwe Gozibath Blandes ambaye ni mfugaji wa kata ya Ihembe na ndie aliyeibiwa ngombe hao alisema kuwa ofisa huyo ambaye anaitwa Onesphor Ajinasi anajihusisha na kesi ambayo haimuhusu kwa kuwatishia wapelelezi wa kesi hiyo wakiwemo mashahidi kwa upande wa mashtaka.

Blandes ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Karagwe (CCM) alisema kuwa hadi hivi sasa kesi hiyo inayoendelea katika mahakama ya wilaya ya Kayanga inaedelea kusikilizwa na mashahidi wanne kwa upande wa mashtaka wametoa ushahidi wao, lakini alisikitishwa na vitendo vya ofisa wa Takukuru kutaka kuingilia uhuru wa mahakama.

Aliongeza kuwa watuhumiwa ambao wanahisika na wizi wa ngombe zake sio Watanzania ni wanyarwanda na aliwataja kwa majina ya Rusagara Geofrey(33) mfanyakazi katika mamlaka ya mapato nchini Rwanda,Joramu Sebatwale(47) na Ndamaji Anacleth (66) ambao wote wanahusika na vitendo vya wizi.

Aidha aliongeza kuwa ngombe hao walikamatwa mnamo tarehe 5/4/2011 katika eneo la Kasulo wilayani Ngara eneo ambalo walikuwa wamefichwa mara baada ya kuibiwa na raia hao wa Rwanda.

"Kwakweli bado inasikitisha kuona mtumishi wa serikali tena kitengo muhimu anaigilia sehemu ambayo hausiki nayo ili kuharibu kesi ambayo ahusiki nayo tena kibaya zaidi anaweka kesi za kubumba kwa wale wote wanasaidia wakiwemo wapelelezi kutoka jeshi la Polisi ambao siwezi kuwataja inabidi mamlaka husika kumuangalia huyo mtumishi wao"alisema Blandesi.

Aliongeza kuwa wananchi wa wilaya hiyo wanakabiliwa na tatizo la wizi wa ngombe kutoka kwa wavamizi wa nchi jirani jambo ambalo linawaathiri wafugaji wadogowadogo.

Aidha taarifa ambazo ziliwafikia waadishi wa habari zinasema kuwa ofisa huyo wa Takukuru wilaya amekuwa akiwaambia baadhi ya wananchi kuwa atahakikisha anawafuatilia wale wote wanajihusisha na kesi hiyo na ikiwezekana anawawekea mitego ya rushwa ya kutegeshea.

Jitihada za kumtafuta ofisa huyo zilishindikana kwa kuambiwa kuwa akuwepo katika eneo la kazi na kwamba yuko mbali na wilaya hiyo nakuambiwa kuwa suala hilo anaweza kulizungumzia kamanda wa Takukuru mkoa.

Akizungumzia suala hilo Kamanda wa Takukuru Mkoani Kagera Domina Mkama alisema kuwa taarifa ambazo zinatolewa juu ya mtumishi wake azina ukweli ndani yake bali ni kikundi kidogo cha watu ambao wanachunguzwa au waliwahi kuchunguzwa na taasisi hiyo na wanataka kuijengea chuki Takukuru.

Alisema suala la kesi ya wizi wa Ngombe analifahamu kwani iko mahakamani kwa hiyo kesi kama sio ya Takukuru ni vigumu ofisa yoyote kuingilia kwaiyo huyu ofisa wake hana mamlaka ya kuingilia kesi isiyo muhusu,hizo ni chuki za baadhi ya watu na jambo hili halipo.

Mwisho

Saturday, March 24, 2012

POLISI AUWAWA KINYAMA NA KUPORWA BUNDUKI

Kamanda wa polisi mkoani kagera Henry Salewi akizungumza kuhusiana na matukio mbalimbali




Bukoba

WATU wasijulikana wamemuuwa askari polisi kwa kumpiga kichwani na moko ambacho ni kifaa cha kuchimbia madini kwa wachimbaji wadogowadogo  kisha wakatoweka na bunduki aliyokuwa nayo aaskari huyo aina ya SMG katika mgodi wa Tulawaka wilayani Biharamulo mkoani Kagera.

Kwa mujibu wa kamanda wa Polisi mkoani Kagera Henry Salewi amewaambia waandishi wa habari kuwa tukio hilo lilitokea jana majira ya saa kumi na moja jioni ambako askari huyo akiwa na wenzake watatu walikuwa katika doria ya kulinda eneo la mgodi huo.

Kamanda Salewi Alimtaja kwa jina ni Namba G.2626 PC Diksoni mwenye umri wa miaka 29 mzaliwa wa Sumbawanga mkoani Katavi.

Aliongeza kuwa wauwaji hao walikuwa na nia ya kupora bunduki kwa ajili ya kufanya uharifu na inasadikiwa ni wachimbaji wadogo wadogo ambao upenda kuindia katika mgodi wa Tulawaka kufanya vitendo vya uharifu.

Aidha alisema kuwa askari wengine watatu ambao walikuwa na marehemu wakiwa doria walishangaa kuona mwenzao haonekani ndipo walianza kumtafuta na kumkuta tayari amekufa na akiwa hana bunduki aina ya SMG kwa kila askari anakuwa na eneo lake la kulinda katika pori lililozunguka mgodi.

Mwili wa marehemu umesafirishwa kuelekea mkoani Katavi wilaya ya Sumbawanga ili kuweza kufanyika taratibu za mazishi na ameacha mjane..


Kamanda Salewi alisema kuwa juhudi za kuitafuta bunduki zinaendelea katika eneo la Tulawaka ikiwemo maeneo ya karibu na eneo hilo na ametoa wito kwa wananchi wa wilaya ya Buharamulo kutoa taarifa endapo watabaini kuiona bunduki hiyo ya kivita.

Friday, March 23, 2012

TEMBOTEMBO JAMANI WANAWASUMBUA WANA BUKOBA VIJIJINI

Na.Kibuka Prudence,Bukoba Vijijini

SERIKALI imeombwa kuweka mpango mkakati wa kupambana na wanyama waharibifu na kuwatoa katika mazingira wasipostairi ili kuepusha gharama nyingi za fidia zinazosababishwa na wanyama hao.

Rai imetolewa na baadhi ya wananch wa vijiji vya Ombweya na Kikagati vilivyoko katika kata ya Izimbya wilayani Bukoba vijijini,mara baada ya kufanya maojiano na waandishi wa habari waliofika maeneo hayo yanayodaiwa kukidhiri na kuwepo wanyama aina ya ya Tembo.

Bw.Januari Abdalla(35)mkulima wa maeneo hayo,alisema kuwa wanyama jamii ya Tembo ufanya uharibifu wa mazao ya wananchi kutokana na kutoka katika hifadhi ya Taifa Burigi iliyoko wilaya za Muleba na Buharamulo.

Abdalla alisema kuwa vitendo vya Tembo kuvamia makazi ya wananchi si jambo geni kwa wakazi hao,kwani ni kila mara wanyama hao ufanya uharibifu wa mali za watu na kuvunja vunja makazi yao,jambo ambalo ufanya wakazi husika kuishi kwa mashaka.

Bw. Bonifasi Rwegila ni meneja wa ranchi ya Taifa (NARCO)ya Kagoma iliyoko katika wilaya ya bukoba vijijini,alibainisha kuwepo na kushamili vitendo vinavyotokana na uvamizi wa wanyama hao.

Rwegila alisema kuwa wanyama hao ni hatari kwa maisha ya watu hususani watumishi ndani ya ranchi na wananchi jirani na ranchi hiyo,ambapo Tembo hao ufika mara kwa mara maeneo ya ranchi na kuharibu mazizi ya ng'ombe na majumba ya watumishi wa ranchi.

Alisema kuwa hali hiyo usababisha watumishi katika ranchi hiyo kuishi kwa tahadhari kubwa kwani mbali na kuvunja mazizi ya mifugo,Tembo pia ni hatari kwa maisha ya watu.

Meneja huyo wa Kagoma ranchi,alisema ni vyema serikali kupitia halmashauri za wilaya kuweka mpango maalumu ambao ni kwa ajili ya kufukuza wanyama hao mbali na maeneo ya watu kuliko kuendelea kufanya uharibifu ambao gharama uwa kubwa sana.

Alisema kuwa gharama za uendeshaji shughuli za ranchi ni kubwa mno,ikizingatiwa baadhi ya vitu kupandaa kwa bei madukani hivyo ni hasara kubwa pale inapotokea Tembo kuvunja mazizi ya mifugo wakati hali ya kiuchumi ni duni ambavyo wakati mwingine usababisha hata shughuli za uendeshaji kukwama.

Hata hivyo,pamoja na kusababisha gharama za uendeshaji wa ranchi kuwa kubwa,Meneja huyu alisema hali ya wasiwasi juu ya maisha yao kutokana na kuwepo na Tembo katika mazingira hayto,pia usabnabisha kufanya shughuli za kuvuga kwa roho mkononi,na kusababisha kuzorotesha ufanisi wa malengo yaliyokusudiwa.

Kero ya Tembo imekuwa ikilipotiwa mara kwa mara kwa wananchi wanaoishi maeneo ya kata za Izimbya na Kibirizi ingawa halmashauri ya wilaya Bukoba kupitia kitengo cha mali asili na Uvuvi, imekuwa ifanya utaratibu wa kuwafukuza wanyama hao na kuwasogeza mbali na maeneo wanamoishi wananchi,japo tatizo hilo linadaiwa bado kuwa ni kero kwa wananchi kwani kunauharifu mkubwa unaosabishwa na Tembo hao.

MWISHO

Tido Mhando Bosi Mpya Mwananchi

BODI ya Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), imemteua Mwandishi wa Habari Mkongwe barani Afrika, Tido Mhando kuwa Mkurugenzi mpya wa kampuni hiyo kuanzia jana.

Waziri Mponda Azungumza Siku ya Kifua Kikuu Duniani

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hadji Hussein Mponda Kushoto akiongea na Waandishi wa Habari kuhusu kuadhimisha siku ya Kifua Kikuu Kitaifa, ambapo sherehe zitafanyika Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara hivi karibuni kwenye ukumbi wa wizara ya Afya Jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hadji Hussein Mponda akiongea na Waandishi wa Habari ambao hawapo kwenye Picha kuhusu siku ya Kifua Kikuu kitaifa ambapo sherehe zitafanyika Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara hivi karibuni kwenye Ukumbi wa Wizara ya Afya Jijini Dar es Salaam leo.

Picha na Anna Itenda -Maelezo.

Thursday, March 22, 2012

Iringa Mpo Tayari Kumpokea Mh Rais Wetu

Rais Akishuka Kwenye Ndege alipowasili katika uwanja Mkoani Iringa

Rais Karibu Mkoani Iringa

Rais Jakaya Kikwete akiongozana na Mkuu wa mkoa wa Iringa Dk. Christine Ishengoma kushoto mara baada ya kuwasili mjini Iringa , kulia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Grayson Rwenge.

Rais Kikwete azindua Mradi wa Maji Pawaga Iringa

Rais Jakaya Kikwete akifungua maji ya bomba kuashiria uzinduzi rasmi wa mradi wa maji katika kijiji cha Itunundu kata ya Pawaga Iringa uliogharimiwa na kanisa la Anglican Dayosisi ya Luaha Mkoani Iringa kwa zaidi shilingi bilioni mbili, Huku wakuu wa kanisal hilo wakishuhudia, kutoka kulia ni Askofu mstaafu wa Dayosisi ya Luaha Dornald Mtetemela, Martha Mgomi Mratibu wa mradi huo na Askofu Joseph Mgomi wa Daayosisi ya Luaha. FULLSHANGWE ilikuwepo katika msafara huo na kukuletea taswira mbalimbali za kuwasili kwa Mh. Rais Jakaya Kikwete pamoja na shughuli yake ya kuzindua mradi wa maji katika kijiji cha Itunundu kata ya Pawaga mkoani Iringa.

Wednesday, March 21, 2012

DUH: Maradhi Ya Mwakyembe ni Ya Kawaida Kwa Tanzania

The Citizen Reporter
Dar es Salaam. The disease that deputy minister for Works Dr Harrison Mwakyembe has been battling for almost six months, is fairly widespread in Tanzania, but is only now becoming a subject of public discussion.

Medical experts say that on average, between two and five people seek treatment for scleroderma at clinics in Dar es Salaam Region at three-weekly intervals, which they suggest represents a countrywide prevalence trend .

Up to last Monday when Dr Mwakyembe disclosed that he was suffering from scleroderma ‑ a chronic condition that causes inflammation and thickening of the skin – knowledge or awareness of the disease was confined to a relatively small circle of doctors, medical students, patients and their relatives.

It has now become a subject of wider public interest in the wake of the controversy that has marked the deputy minister’s health status, triggered, primarily, by allegations that he had been poisoned by individuals that neither he nor political allies who support the theory, have named.

The controversy persists, because simultaneous to telling journalists at a briefing session in the city that doctors at Apollo Hospital in India had diagnosed ‘popular scleroderma’ as the ailment that was troubling him, he called on the government team investigating the issue to speed it up. Medical doctors who spoke to The Citizen yesterday confirmed that the disease was fairly common in the country, but noted that its effects spread slowly.

Dr Isaac Maro of the Infectious Diseases Centre in Dar es Salaam confirmed that many Tanzanian are suffering from the disease, whose causes health experts had not established.“If you open a skin clinic in this city, for example, at least three people will seek treatment for scleroderma within two to three weeks,” he said.

The disease is an autoimmune, rheumatic, and chronic affliction that affects the body by hardening connective tissues. Literally, “scleroderma” means “hard skin”.

It is classified as an autoimmune disease, which means that a person’s immune system works against itself. Its severity varies from person to person: it can be a mild annoyance or it can cause significant clinical problems.

For others, it can become life threatening. Dr Maro cited the case of a scleroderma patient he had attended over the past two years, but whose condition didn’t seem serious. Doctors say treatment of the disease takes a long time, and that, if it is not administered at early stages, the disease affects internal body organs like lungs.

Another skin consultant doctor volunteered to comment on the disease but on condition of remaining anonymous, as a safeguard against being associated with the controversial dimension to Dr Mwakyembe’s illness.
He said several people suffering from the disease attended his clinic in Dar es Salaam, adding that, it was afflicting many others all over the country, but very few of whom sought treatment, especially those living in villages. Scleroderma starts by affecting hands and face, but seldom affects hair; and sometimes penetrates internal organs at advanced stages.

Hii habari imetoka leo Jumatano kwenye gazeti la The Citizen baada ya waandishi kuwahoji madaktari mabingwa wa magonjwa ya ngozi wanaowatibu watu wenye tatizo hili - Scleroderma - hapa nchini. Jamani miye mjumbe tu, kwa kawaida mjumbe hauawi. Tunahitaji kufahamu kinachoendelea kama alivyoshauri mwenyewe Dkt. Mwakyembe na hata kuomba serikali iwe wazi.

Matinyi.

Karibu Dkt. Slaa

[Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa]Picha kwa hisani ya mjengwablogspot

LASEMA KAMA ANAO USHAHIDI WA WIZI WA FEDHA ZA PAPA AUTOE, WANASIASA WANAOCHAFUA WENZAO WAMEFILISIKA, NEC YAVIONYA CCM, CHADEMA
Na Waandishi Wetu
KANISA Katoliki nchini limemtaka Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Uhusiano wa Jamii), Stephen Wassira kutoa ushahidi kuthibitisha kama Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alifukuzwa upadre baada ya kuiba fedha za ujio wa Papa John Paul II, alipokuja nchini mwaka 1991.Akizungumza kwa simu jana, Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (Tec), Yuda Thadeus Ruwaichi alimtaka Wassira athibitishe tuhuma zake akisema kanisa hilo halijawahi kumtuhumu Dk Slaa kwa tuhuma za wizi.

Akizungumza katika kampeni za CCM Jimbo la Arumeru Machi 19, mwaka huu, Wassira alimtupia kombora Dk Slaa akidai si mwaminifu kwa kuwa alifukuzwa ukasisi wa kanisa hilo baada ya kufanya ufisadi kwenye fedha za mapokezi ya Papa huyo ambaye sasa ni marehemu.

Hata hivyo, Wassira jana alipotakiwa kuzungumzia kauli hiyo ya Askofu Ruwaichi alijibu kwa kifupi: “Mimi nilishazungumza na yakaandikwa kwenye vyombo vya habari, hii leo siyo habari.”
Ruwaichi ambaye pia ni Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Mwanza alisema madai hayo ya Wassira hayana msingi.

“Kanisa halijawahi kumshutumu Dk Slaa kuhusu madai hayo (ya Wassira). Kama Wassira ameyatoa kwenye mkutano wa hadhara, njia sahihi ya kupata ukweli ni yeye kutupa ushahidi wa vielelezo kuthibitisha madai yake,” alisema Ruwaichi.

Askofu Ruwaichi amewaonya wanasiasa wanaofanya kampeni za kuchafuana akiwataka waache na waanze kufanya siasa za kistaarabu.

“Ukiona mwanasiasa anakurupuka na kuanza kumchafua mwenzake ujue amefilisika, vitendo hivyo vinaonyesha udhaifu kwa nchi katika nyanja za siasa,” alisema.

Askofu Ruwaichi alisema wanasiasa waliokomaa hawapaswi kufanya kampeni za kuchafuana... “Watajishughulisha katika kujadili hoja zinazozingatia mahitaji ya jamii. Kitendo cha wanasiasa wetu kufanya kampeni za kuchafuana kinaonyesha dhahiri kuwa bado tuko dhaifu katika siasa na hatuna vipaumbele.”

Askofu Ruwaichi aliwataka wanasiasa hao kuachana na kampeni chafu na badala yake wajikite katika kujadili hoja zinazotoa vipaumbele katika matatizo yanayoikabili jamii na namna ya kuyatatua ili kuwawezesha wananchi kuchagua viongozi bora.

Kauli hiyo ya Askofu Ruwaichi, imekuja siku chache baada ya Dk Slaa kuzungumza katika mkutano wa hadhara kwenye kampeni za uchaguzi mdogo Jimbo la Arumeru na kusema Wassira ni mwongo na hajui asemalo.

“Kama tangu mwaka 1991 nipo, basi kitendo cha Serikali kushindwa kunifungulia mashtaka ya wizi wa hizo fedha basi ni Serikali dhaifu na ijiuzulu,” alisema Dk Slaa.Soma zaidi www.mwananchi.co.tz

Tuesday, March 20, 2012

MCHUNGAJI ANYANGANYWA WANAFUNZI BUKOBA VIJIJINI

Na.Kibuka Prudence,Bukoba Vijijini

HALMASHAURI ya wilaya Bukoba mkoani Kagera,imefikia uamuzi wa kutoa watoto waliokuwa wakipata malezi kutoka kwa mchungaji kutokana na kudaiwa kukiukwa na baadhi ya mashariti ya malezi.

Hatua hiyo iliyochukuliwa na halmashauri Machi 17 chini ya idara ya maendeleo ya jamii,imekuja baada ya madai kuwa mlezi aliyekuwa akiwajibika kuwalea watoto hao 37 wakiwa wa kike 12 na kiume 25 alishindwa kufuata baadhi ya masharti yanayopaswa kufuatwa wakati wa malezi ya mtoto.

Mmoja wa maafisa wa idara hiyo waliohusika katika kuamisha watoto hao kutoka kituo cha malezi cha Kaagya Ophans Care Center na kuwaamisha kituo cha Kabilizi kilicho chini ya idara hiyo kata Rubale,bi.Renatha Mshwaili,alisema halmashauri imefikia maamuzi hayo ili kuepusha mtoto na matatizo mengine yanayoweza kumsababishia madhara ya kiafya.

Mshwaili alisema kuwa awali walibaini kuwepo matatizo mbalimbali yaliyokuwa baiona ya  mlezi wa kituo hicho ambaye ni mchungaji wa kanisa la Christian Life Church Cleoper Kaijage na mfadhili wa kituo hicho ambao ni shirika la The Mighty Fortress lenye makazi yake nchini Uholanzi.

Alisema baada ya mfadhili kudai kuwa hakubaliana na utawala uliopo na kuomba halmashauri kuchukua maamuzi juu ya walengwa(watoto)idara yake ilifikia maamuzi ya kuwanusuru watoto kwa mpango maalumu wa kujali usalama wa mtoto huku atua nyingine zikifuatwa.

Hata hivyo,kwa upande wake mlezi wa kituo hicho,mchungaji Kaijage,alikiri kutokubaliana na mfadhili wake kwa kile alichodai kuwepo baadhi ya wajumbe waliwai kufukuzwa ndani ya bodi ya kituo kumchonganisha mfadhili dhidi yake kwa maslahi ya kutaka utawala.

Mchungaji Kaijage aliswema kuwa japo kituo hicho kilikuwa kikipata ufadhili kutoka kwa shirika husika,lakini ufadhili ulimkuta tayari ameanza kutoa msaada kwa walengwa hao.Ambapo wazo la kuanzishwa kituo hicho lilianza tangu mwaka 2004 na mwaka 2005 alianza kutoa msaada wa malezi kwa watoto 12.

Alisema malezi hayo yaliendelea kutolewa kituoni hapo mpaka 2008 hini ya bodi ya kituo hicho,na tayari alikuwa amejenga majumba mawili japo yalikuwa ya udongo lakini lengo kuu lilikuwa ni kuwanusuru watoto wanaoishi katika mazingira magumu,ambao walickuliwa kutoka maeneo ya mwalo wa Igabilo na sehenmu nyingine.

Alisema msaada wa shirika ulianza kutolewa mnamo mwaka 2008 wakiwa na watoto 15,ambapo mfadhili alikubali kuwafadhili watoto kwa kuboresha nyumba na kutoa dola 20 kwa ajili ya chakula na matumizi mengine,jambo ambalo uongozi uliamua kulima ili kujipatia chakula na fedha hizo zikagharamikie huduma za kuwapatia elimu katika mashule mbalimbali.

Aidha,mchungaji huyo anadai kuwa anashangazwa na uamuzi wa halmashauri kumwamulisha ahame kituoni hapo kwa kuelekezwa na wafadhili,kwani yeye aende wapi wakati hapio alipo ndiyo kwake na kuiomba serikali kuchunguza kwanza na kubaini ukweli ulivyo kabla ya maamuzi mengine.

Alibainisha kuwa tayari ameanza kuchafuliwa kwa maneno ya kashifa kuwa anawanyanyasa watoto jambo ambalo ni la kupandikizwa na alishakamatwa na kukaa rumande kwa siku 15,japo tayari kesi dhidi ya madai yote yanayo muguza ipo mahakamani.

MWISHO

NG OMBE WA NYAMA JAMII YA KONGWA DODOMA

Moja ya bonge la N gombe jamii ya KONGWA ambaye ni kwa ajili ya nyama akiwa kwenye malisho katika Ranch ya Kagoma Wilayani Bukoba

Wananchi mkoani Kagera Wanufaika na Ranch ya Taifa

Moja ya ngombe jamii ya Kongwa wakiwa katika malisho ndani ya ranch za taifa mkoani kagera hapa ni Ranch ya Kagoma Wilayani Bukoba

Na Antidius kalunde
Kagera


JAMII ya wafugaji wadogowadogo mkoani Kagera,wamepongeza uhamuzi wa mamlaka ya ranchi za taifa zinazojishughulisha na ufugaji wa ng'ombe,kwa kuwanufaisha kwa njia ya kutoa elimu ya ufugaji ulio bora ba wa kisasa.

Wakiongea na waandishi wa habari,wafugaji hao walisema utaratibu unaoendelezwa na kampuni za ranchi za Taifa(NARCO)zilizo Kagoma,Kikurula,Missenyi na Mabare ni mzuri na wenye malengo ya kumuinua mfugaji na mkulima ili kuondokana na umasikini.

Mmoja wa wafugaji hao John Muganyizi(47)mkazi wa wilayani Karagwe,alisema kuwa pamoja na baadhi ya wafugani wengine katika maeneo mbalimbali mkoani Kagera walikuwa na ujuzi wa kujiendeleza kiufugaji lakini utaratibu wa ranchi hizi ni mzuri zaidi kwani ni njia mbadala ya kumuelimisha mwananchi atambue umuhimu wa ufugaji na kilimo.

Muganyizi alisema kuwa awali hali ya ufugaji kwa wakulima ilionekana kukumbwa na changamoto kubwa ususani namna mbalimbali za kukabiliana na magonjwa ya mifugo,kubaini mbegu bora za ng'ombe zinazofaa katika ufugaji,lakini atua za ranchiNARCO kupisha utaratibu huu,ni dalili kuu inayoonesha kuwa serikali bado haijamsahau mfugaji wa taifa hili.

Alisema kwakuwa NARCO imeamua kuwapatia mafunzo wafugaji,ni vyema wakazi wa mkoa wa Kagera kuchangamkia fursa hii kwani ni muhimu na kwa kuelimika juu ya ufugaji janga la umasiki litapungua kwa kiasi kikubwa sana.

Tarsis Mawala ni meneja wa ranchi ya Missenyi,anasema utaratibu wa kutoa elimu ya ufugaji kwa wafugaji ni mojawapo ya majukumu ya NARCO hivyo ni mwendelezo wa mipango ya kampuni na ipo kwa kila mpango mkakati wa ranchi mkoani Kagera.

Mawala amesema pamoja na kutoa elimu pia ranchi hizo za Kagoma,Missenyi na Kikurula utoa mbolea kwa wakulima wa vijijini kwa bei nafuu sana,na kwa kufanya hivyo urahisisha ushughuli za ranchi na kujenga mahusiano kwa wananchi.

Alingeza kuwa hata hivyo kamppuni hizo ukabiliwa na baadhi ya changamoto nyingi mmojwapo ikiwepo uchomaji mbuga hovyo na kuwepo wanyama wakali maeneo ya ranchi kama tembo katika ranchi za Kagoma na Kikurula ambavo uhataarisha maisha ya watumishi wa ranchi na mifugo.

MWISHO


Dk Mwakyembe Akizungumza na Vyombo Vya Habari Jana

aibu Waziri wa Ujenzi Dk. Harrison Mwakyembe, akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam jana, muda mfupi baada ya kuingia ofisini humo kuanza kazi, kutokana na afya yake kuimarika. Mwakyembe amekuwa akitibiwa nchini India kwa muda mrefu. Picha na Zacharia Osanga




 BAADA ya utata wa muda mrefu wa ama Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe amelishwa sumu au la, jana Mbunge huyo wa Kyela, aliweka hadharani ugonjwa wake akisema unafahamika kitaalamu kwa jina la Popular Scleroderma huku akisisitiza: “Sasa nimepona kabisa.”Dk Mwakyembe amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya ngozi ambayo mwaka jana yalizidi kumtikisa na Oktoba 9, Serikali iliamua kumpeleka Hospitali ya Appolo, India kwa ajili ya matibabu na uchunguzi zaidi.Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam jana, Dk Mwakyembe akiwa amevalia kofia ya pama alisema: “Si kwamba sijambo, bali nimepona kabisa baada ya kugundulika na maradhi hayo na kutibiwa.”“Nimerudi juzi kutoka India na daktari wangu ameniambia nimepona, nilikuwa nasumbuliwa na maradhi ya ‘Popular Scleroderma’ iliyosababisha ‘skin disorder’ (ngozi kutokuwa katika hali ya kawaida), lakini kwa nguvu za Mungu nimepona, namshukuru Mungu.”Kuhusu sumu
Alipoulizwa kuhusu tuhuma za kulishwa sumu, Dk Mwakyembe alikataa kuzungumzia hilo akisema anasubiri uchunguzi ulioagizwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha.Hata hivyo, Dk Mwakyembe alisema angependa kuona uchunguzi huo unakamilika haraka na ripoti yake inatangazwa kwa umma.Alisema yuko tayari na anasubiri tume hiyo ya uchunguzi iliyoundwa na Waziri Nahodha imhoji ili atoa kile kilichomo katika ripoti ya daktari wake.Dk Mwakyembe alisema anachoshukuru hadi sasa ni kwamba afya yake imeimarika kutokana na shinikizo la Rais Jakaya Kikwete ambaye aliagiza Serikali kumpa kipaumbele wakati wote akiwa nchini na India hatua ambayo imemwezesha kufika hapo alipo.Kutokana na hali hiyo, Dk Mwakyembe aliwataka wananchi wote wakiwemo wa jimboni kwake Kyela kuondoa wasiwasi akisema sasa yupo imara kwa ajili ya ujenzi wa majukumu ya taifa.“Ninaomba wapiga kura wangu wa Kyela waache jazba, wawe na subira juu ya matatizo yangu. Wiki ijayo nitakwenda kuzungumza nao ili niweze kuwaeleza matatizo yaliyokuwa yananisumbua, lakini sasa hivi niko fit,” alisema.
SOMA ZAIDI:http://www.mwananchi.co.tz/habari/-/21277-dk-mwakyembe-aweka-hadharani-ugonjwa-wake

Monday, March 19, 2012

Bado tuko Pori mda mwingine hari inakuwa hivi

Hapa ni mdau Prudence Kibuka Mmiliki wa Mtandao wa bukobaFamaly akiwa katikati ya pori Kagoma Runch lakini mda mwingine barabara balaa hapa unaweza kukutana na Tembo Pori balaa

Unaweza Ukafikiri ni Mjini hapa Lakini Katikati ya Pori

Nikiwa katika michakato yangu na mdau wa pori  hapa ni katikati ya pori la Kagoma Runch wilayani Bukoba hili ni eneo la Ranch za Taifa na hapa ni moja ya majosho ya kuoshea ngombe wanaofugwa Kagoma Runch..................BORA MAISHA YA PORI KULIKO MJINI NJAA TUPU

Jamani Mapambano yakuingia mjengoni Bado yanaendelea Arumeru


Dk Slaa Akihutubia Arumeru Jana

Picha Kwa hisani ya Mjengwablogspot

Saturday, March 17, 2012

MWAKYEMBE KUTOA TAMKO KESHO KUTWA

Fidelis Butahe
NAIBU Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe amerejea nchini akitokea India alikokwenda kwa matibabu na kueleza kuwa atazungumzia, pamoja na mambo mengine, afya yake keshokutwa atakapoingia ofisini.

Hata hivyo, mara baada ya kuwasili jana alasiri kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam Mbunge huyo wa Kyela (CCM), hakutaka kuzungumza na waandishi wa habari na badala yake alitoa ujumbe wake huo kupitia kwa Mbunge wa Lupa (CCM), Victor Mwambalaswa ambaye pia ni msemaji wa familia ya Dk Mwakyembe.

Mwambalaswa alisema Dk Mwakyembe aliona ni vyema apate muda wa kutosha kujiandaa kabla ya kukutana na waandishi wa habari Jumatatu.

“Afya yake imeimarika na anaendelea vizuri, ila ameomba msamaha kuwa hataweza kuzungumza na nyinyi (waandishi), amesema yeyote anayetaka kuzungumza naye, aende ofisini kwake Jumatatu,” alisema Mwambalaswa.

Dk Mwakyembe alifika katika viwanja hivyo saa 9:47 alasiri, lakini kabla ya kuingia katika vyumba vya abiria wanaowasili, alituma ujumbe kwa waandishi wa habari kuwa hatakuwa tayari kuzungumza jambo lolote.
Dk Mwakyembe amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya ngozi ambayo Oktoba 9, mwaka jana yalimlazimu kupelekwa katika Hospitali ya Appolo, India kwa matibabu zaidi.

Maradhi hayo yamezua utata mkubwa baada ya kudaiwa kuwa yametokana na kuwekewa sumu huku kukiwa na kauli mbalimbali zinazotofautiana kutoka kwake na baadhi ya watendaji wengine wa Serikali.

Kauli tata zaidi ziliibuka baada baadhi ya viongozi akiwamo Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta kudai kuwa maradhi yanayomsumbua Dk Mwakyembe yametokana na kulishwa sumu.

Hata hivyo, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Kamishna Robert Manumba alijibu madai hayo aliposema kuwa uchunguzi wa polisi umebaini kuwa Dk Mwakyembe hajaugua kwa sababu ya kulishwa sumu na kutishia kuwachukulia hatua walitoa kauli hizo.

Ripoti ya uchunguzi aliyoisoma Manumba katika mkutano wake na waandishi wa habari Februari 16, mwaka huu Dar es Salaam, inaonyesha kuwa Dk Mwakyembe hakulishwa sumu huku akisema kwamba pia ulijumuisha taarifa kutoka hospitalini India ambako alikuwa anatibiwa.

Alisema uchunguzi huo unalipa Jeshi la Polisi picha kuwa waliotoa taarifa hizo hadharani wanapaswa kuchukuliwa hatua za kisheria.

Baada ya kauli hiyo, Dk Mwakyembe aliibuka na kutoa kauli nzito iliyoonekana kumjibu Kamishna Manumba akielezea kushangazwa kwake na majibu hayo huku akisisitiza kuwa madaktari waliokuwa wakimtibu walithibitisha kuwa ugonjwa alionao unatokana na kulishwa sumu.

Mbali ya Dk Mwakyembe, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hadji Mponda na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha, kwa nyakati tofauti walikana kuijua ripoti hiyo ya Kamishna Manumba.

Hata hivyo, katika kile kilichoonekana kudhamiria kuchukua hatua, inadaiwa kuwa Kamishna Manumba aliwasilisha jalada la mashtaka kwa watu hao kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Eliezer Feleshi ambaye alithibitisha kulipokea lakini akasema ni vigumu kufahamu ni lini atakapopeleka mahakamani jalada la kesi kwa watu hao.


“Ni vigumu kusema ni lini kesi itapelekwa mahakamani... bado tunalifanyia kazi,” alisema Feleshi akisisitiza kuwa uamuzi wa kupeleka suala hilo mahakamani utategemea uchunguzi unaofanywa na ofisi yake. Chanzo: Gazeti Mwananchi.

Friday, March 16, 2012

BAADA YA KAZI NI MAPUMZIKO KITAKACHOFUATA NI KWENDA HOME

Wamiliki wa  mitandao ya kijamii mjini Bukoba wakiwa na wadau wengine wakiwa wametuliiia baada ya kazi za siku nzima lakini hiki kijiwe kinapatikana katika ofisi za Bohari kuu ya Mkoa wa Kagera mjini BUKOBAAA(Kutoka Kushoto ni Mathias Byabato Mmiliki wa Bukoba Forum,Ivani Ndyamukama Mdau wa mitandao,Ustaadhi alieangalia nyuma nae ni mdau wa mitandao na Kibuka Prudence mmiliki wa Bukoba Family kwa nyumaaa Dada Angela Batuli

KATIKA MPAKA WA TANZANIA NA UGANDA MAGARI YAMIZIGO YAZIDI KUKWAMA


MAGARI YAKIWA YANATAKA KUVUKA

Msongamano wa magari makubwa umezidi kuwepo katika eneo la mpaka wa Tanzania na Uganda hasa magari makubwa ya mizigo tatizo hili linatokana na kusuasua kwa mtandao wa mamlaka ya mapato Tanzania(TRA)katika eneo la Mtukula

MASOKO MENGINE NI HATARI

Soko la Africa Mashariki jamani hebu liangalie
Hili ni eneo la soko ambalo ndilo soko kuu Wilayani Missenyi na linatumiwa na watu wengi sana linailtwa SOKO LA BUNAZI ila halina usalama wowote kutokana na vibanda kuezekwa kwa nyasi

JAMANIII WATU WA UJENZI WA BARABARA MBONA KIMYAA

Hiki ni kibao kinachoonyesha ofisi ya Mkuu wa wilaya Missenyi ilipo katika mji wa Bunazi mkoani Kagera lakini Kibao hiki ni moja ya vitu vinavyoonyesha taswira mbaya katika mji huo mkoani Kagera

Monday, March 12, 2012

Mashine ya kuinua matiti ya wakina mama yaingia Tanzania

WANAWAKE WAFURIKA KUPATA HUDUMA
Na Julieth Kulangwa
BIASHARA huria imezua mengi. Hali kadhalika Sayansi na Tekenolojia nayo, imeleta mengi. Katika kuwaondolea kero wanawake wenye matiti yaliyosinyaa hapa nchini, wataalamu kutoka China wameanza kutoa huduma ya kunyanyua matiti hayo kwa kutumia mashine maalumu.

Wachina wamejipatia umaarufu katika kuleta bidhaa mbalimbali hapa nchini, zikiwamo za kuongeza nguvu za kiume, kupunguza uzito, kuotesha nywele, kujichubua (kumfanya mtu mweusi awe mweupe), kuongeza makalio nk.

Huduma hiyo ya kusimamisha matiti yaliyolala, imeanza kutolewa katika Saluni ya Blue Palace, iliyopo nyuma ya Shule ya Mapambano, Sinza jijini Dar es Salaam.

Haikuwa rahisi kuweza kuamini kuwa vitu kama hivi vinaweza kupatikana Tanzania. Mwananchi Jumapili lilifunga safari mpaka kwenye saluni hiyo inayomilikiwa na Sarafina Mtweve, kujionea jinsi teknolojia hiyo inavyofanya kazi.
Mbali na meneja wa saluni hiyo, Trust Mwembe, pia alikuwepo mtaalamu kutoka China aitwaye, Ciisy Pang, ni binti wa miaka 23 tu, lakini anasema kwa miaka minne amefanya kazi hiyo na kuwasaidia wanawake mbalimbali waliokuwa wakikerwa na matiti yaliyolegea au kuanguka.

Pang na kundi lake wanatoa huduma hii kwa gharama ya Sh150,000 kwa kuanzia, ingawa wanahisi gharama hizo zitapanda katika siku chache zijazo.

Jinsi matiti yanavyosimamishwa
Mashine hiyo inayoitwa ‘Beauty Machine’ ina uwezo wa kusimamisha matiti ya kila saizi kwa kuwa huambatanishwa na vibakuli (cups) kama unavyoona pichani.

Kazi kubwa ya mashine hiyo ni kuamsha misuli ambayo hushikilia nyama za matiti.
Pang anasema, zoezi la kusimamisha matiti huchukua wiki tatu mpaka sita, inategemea aina ya mteja na wakati mwingine juhudi zake.

Mtaalamu huyo ambaye anazungumza Kichina na kutafsiriwa na meneja wa saluni hiyo, anaelezea namna anavyofanya kazi ya kuyarudisha matiti kwa muda huo.

“Kwanza unapaswa ujue kuwa hatutumii dawa yoyote katika zoezi hili, mteja wetu akifika hapa, kinachotumika ni mashine tu ambayo hutumia umeme kama zilivyo dryer za nywele,
“Baada ya kumlaza katika kitanda kile, tunachukua kitu mfano wa bakuli (cups) mbili kulingana na ukubwa wa matiti yake, tunayatumbukiza humo, kisha tunawasha mashine,” anasema Pang.

Mtaalamu huyo anasema mashine hiyo ikiwashwa inavuta kama ‘vacuum’, na inaweza kuongezwa kasi au kupunguzwa kama inavyofanyika kwenye mashine za kufanyia mazoezi.

“Tunaiwasha mashine kwa muda wa dakika 45, mteja atachagua siku mbili katika wiki za kufanya zoezi hili mpaka litakapokamilika,”anasema Pang.

Tangu mashine hiyo iwasili nchini, takribani mwezi mmoja uliopita, Pang anasema ana wateja wanane anaowahudumia kwa nyakati tofauti ambao wamekiri kuwa maendeleo yanatia moyo.

Ni kweli mashine hii inasaidia?
Akizungumza kwa njia ya simu, mmoja wa wateja anayepata huduma hiyo ambaye alijitambulisha kwa jina moja tu Irene anasema, ni wiki ya tatu sasa tangu aanze kupata huduma hiyo, anakiri kuwa matiti yake sasa yameanza kuwa magumu tofauti na mwanzo.

“Kusema kweli nilikuwa na matiti yaliyosinyaa wala si kulala tu kama ulivyouliza, ila naona sasa yameanza kuwa magumu na kurudi juu kidogo,” anasema Irene.

Akizungumzia ugumu anaoupata katika zoezi hilo, anasema safari za kila wiki saluni na zile dakika 45 za kukaa kwenye mashine zinamchosha, lakini kwa kuwa amedhamiria, amejitoa mpaka zoezi hilo litakapokamilika.
Matiti yanaweza kulegea tena?

Pang anasema kama matiti yanalegea kwa sababu fulani mfano uzazi wa watoto wengi, basi yanaweza kulegea tena kama mtu atajifungua na kunyonyesha kwa muda huo.Aidha anasema wanawake wenye matiti makubwa, ni rahisi kuanguka kama hawatayavalisha sidiria kwa muda mrefu.

“Wanawake wenye matiti makubwa huwa nawashauri kuvaa sidiria hasa wakati wa mchana na usiku wanaweza kuacha kuzivaa, hii inasaidia kuimarisha misuli inayoyabeba matiti,” anasema Pang.

Jamii inazungumziaje jambo hili
Baada ya kusikia kuwepo kwa mashine hii nchini, wanawake mbalimbali wamesema wanatamani kupata huduma hiyo lakini wengine, walionyesha woga juu ya matokeo yake.

“Ni kweli baada ya kunyonyesha watoto wawili sasa matiti yamelegea kabisa, natamani yarudi kama wakati ule wa usichana wangu, lakini nahofia huenda mbele ya safari nikapata madhara,” anasema Linda Masatu.

Linda anaongeza kusema kuwa ni vizuri mwanamke akawa na matiti yaliyojaa vizuri, lakini anahofia njia zinaweza kuwa na madhara, huku akisema kama ingetokea njia nyingine ya asili asingesita kuifuata.

Naye Batuli Famau, anasema mwanamke anapokuwa na matiti yaliyosinyaa mvuto wake hupungua, hata anapovaa sidiria anakuwa amebadili mwonekano wa nje tu, lakini ndani bado anakuwa vilevile.

“Mwanamke mrembo ni yule mwenye matiti mazuri, sasa inapobidi kutumia njia fulani ili yarudi kama tulipokuwa vigoli, tutafanya tu ili mradi kama njia hizo hazitatuangamiza,” anasema
Wanaume nao wameonekana kuunga mkono zoezi la kusimamisha matiti ingawa wengine hawaungi mkono utumiaji wa mashine hii.

Augustino Magara anasema: “Ni kweli mwanamke mwenye matiti magumu anavutia kuliko yaliolegea na kulala, lakini sasa tuwe makini kabla wake zetu hawajaumia katika mashine, hizi”Soma zaidi www.mwananchi.co.tz

Saturday, March 10, 2012

Tanzania inapongezwa

TIMU ya wataalam wa mpango wa tathimini ya utendaji kazi kwa nchi za Afrika (APRM) imeisifia Tanzania kwamba ni hazina kubwa katika suala zima la utawala bora katika nchi za Afrika na duniani kote.

Profesa Aderic Nade kutoka nchini Nigeria ambaye pia ni mmoja wa wajumbe wa timu hiyo kati ya 21 wanaounda timu hiyo alibainisha  hayo jana katika  mkutano wa siku moja uliofanyika mjini Bukoba kati ya wadau wa utawala bora na tume hiyo ya APRM kutoka makao makuu.

Prof. Nade ambaye pia ni mhadhiri katika chuo kikuu cha Lagos kilicho nchini Nigeria,alisema kuwa pamoja na changamoto mbalimbali zinazoikabili Tanzania lakini imekuwa ni kisiwa cha nchi nyingine kuja kujifunzia jinsi gani wanavyoilinda amani yake ikiwa ni sambamba na misingi ya utawala bora inayodumishwa kwa wananchi wake.

Alisema lengo la mkutano huo na dhamila kubwa ya tume ni kuangalia mchakato mzima wa utawala bora katika nchi hii,historia   na masuala mazima yanayopelekea utawala bora ulioko Tanzania ulivyoimalika leo na hata kabla ya uhuru.

Alieleza kwamba umuhimu wa kuwepo APRM ni kuhakikisha Afrika inarudi katika mustakabali wa utawara bora ambapo hari hiyo itajenga misingi mipya ambayo itaegemea katika kujadiri mkataba wa kijamii kati ya Serikali na wadau,Serikali na Raia pia kuweka misingi mipya ya mahusiano kati ya Watu wa Afrika.

Alisema kuhusu suala la demokrasia  katika nchi za Kiafrika ni jambo muhimu ambalo ni ndoto ya nchi za kiafrika wanayohitaji kuipata kwahiyo ni haki ya Raia kuuliza Serikali ni mambo gani inapswa kufanya na kama imefanya imefikia malengo yapi.

Alisema malengo mengine ni kuhakikisha pale jambo linapotokea katika nchi moja wapo katika Afrika lionekane kuwagusa Waafrika wote ambapo aliongeza kwamba hari hiyo haikuanza leo bali ilianzishwa na waasisi wa Afrika ambao ni baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambalage Nyerere,Kwame Nkuruma na Keneth Kaunda.

Alisema kuwa tathimini hii ni endelevu ambapo kila baada ya miezi sita wadau watatakiwa kukaa na kutathimini ambapo kila nchi itatakiwa kutoa taarifa jinsi gani imetekeleza mawazo ambayo yaliibuliwa na wadau na kila baada ya miaka mine timu itafanya tathimini juu ya utawala bora pamoja na uendelevu katika nchi za Afrika.

Kwa upande wa mgeni rasmi katika mkutano huo ambaye pia ni katibu tawala wa mkoa wa Kagera Nassor Mnambila kwa niaba ya mkuu wa mkoa huo kanal mstaafua Fabiania Massawe alisema kuwa pamoja na mafanikio hayo ya Tanzania kuwa hazina katika utawala bora bali zipo changamoto zinazowakabili kama Serikali.

Mnambila alisema kuwa changamoto hizo ni mauaji ya vikongwe na walemavu wa ngozi (albino) kwa sababu ya imani za kishirikina,ukeketaji kwa watoto wa kike,ujambazi,ukatili wa kijinsia kwa wanawake na ukatili kwa watoto hawajapata uwakilishi wa kutosha katika masuala ya kisheria ambapo amesema kuwa hayo ni baadhi ya changamoto ambazo Serikali inaendelea kupambana nazo.

mwisho

WATU WAKO BUZY

Wakazi wa Manispaa ya Bukoba wakionekana kupiga mishe mishe yao katika kumalizia siku ya leo hili ni eneo la mjini kati karibu na BIG STAND mjini BUKOBA

KARIBUNII BUKOBA ILA KUNA BARIIIDI

Hii ni moja ya barabara za mjini Bukoba barabara hii ndio ya kuingilia ndani ya mji wa Bukoba kama unatoka eneo lolote nchini Tanzania na nje ya nchi ni eneo maarufu kwa jina la Kanoni karibu na sheli ya TOTAL

JAMANI HAPA TUNAIGIA STAND YA MABASI BUKOBAA

Hiki ni kibao cha kuonyesha jinsi ya kuingia ndani ya stand mjini Bukoba lakini kwa mbele yake kuna kibao Cha SUMATRA CCC ambacho kimeziba kibao cha kuonyesha kuingia BUKOBA STAND


Manispaa ya BUKOBAAA MPOOOO!

Thursday, March 8, 2012

TV SHOW:Ongea na Janeth

JANET MWENDA TALAWA KATIKA POOOZI
JANA  KIMEIBUKA KIPINDI KIPYA CHA TV CHA ‘ONGEA NA JANET’

*AITAKA JAMII KUACHA WOGA NA KUJITOKEZA KUONYESHA VIPAJI.

MO BLOG: Nini Theme ya kipindi cha ‘ONGEA NA JANET’..?

JANET: Aah…!! Theme ya “ONGEA NA JANET’ ni kipindi ambacho kinatoa fursa kwa mtu yeyote kuja kuongea ili mradi awe na kitu ambacho kinaweza kuilemisha jamii. Kipindi hiki kinazungumza na watu wa rika zote. Na katika kipindi hiki kwa kweli mimi nazungumzia kila kitu sijajiwekea limitations. Lengo ili tufike mahali tuweze kuzungumza hata yale mambo ambayo watu wanaogopa kuyazungumza hadharani.

Japo watu wengi wanapenda nizungumzie mambo ambayo yapo current, lakini kwa mfano yakitokea mafuriko, ukifungua TV zote taarifa za habari zinazungumzia mafuriko, radio zote ni mafuriko, ukisoma kila gazeti ni mafuriko na hata misemo mitaani inakuwa kuhusu mafuriko. Sikuona tena umuhimu wa kuongelea kitu ambacho kinaongelewa kila mahali, nataka kutoa nafasi ya kuzungumzia mambo ambayo hatupati nafasi ya kuyazungumzia.

Kwa mfano huwezi kukuta, gazeti au TV ikizungumzia kuwa wanawake walioko katika ndoa wanapata taabu kwa sababu ya nyumba ndogo, na hata kama itaandikwa basi inapewa nafasi ndoogo.

Na sifikirii kipindi changu kiishe leo au kesho  hiki kitaendelea siku zote.

MO BLOG: Watazamaji watarajie nini kutoka kwako katika siku zijazo..?

JANET: Watarajie mambo mengi mazuri na kuwa kila siku kipindi kitakuwa na kitu kipya. Nitakuwa na season 4, hivyo kila season itakuwa tofauti na nyingine. Mfumo nitakaotumia katika season 1 utakuwa tofauti na nitakaoutumia katika season 2 na kuendelea.

Akifanya mambo yake

Janeth akiwa ndani ya TV SHOW JANA

SIKU YA WANAWAKE DUNIANI NI LEO


Wakati wanawake wanasherehekea siku yao Duniani hawa ni wanawake ambao hawatambui kuwa kuna siku ya wanawake,Wanawake hawa kama walivyokutwa na mpiga picha wakiwa wanachambua kahawa leo mapema katika kiwanda cha kusaga kahawa cha AMIR HAMZA mjini Bukoba

Tuesday, March 6, 2012

KARIBU KARAGWE TUNALIMA NDIZI KUBWAAAAAA

Hizi ni ndizi ambazo zinalimwa katika mkoa wa Kagera lakini hii inapatikana katika shamba moja la mkulima hodari ambye ni mkuu wa mkoa wa Kagera kanali Mstaafu Fabiani Massawe liko katika kijiji cha Kayanga wilayani Karagwe mkoani hapa

Nakagua Shamba Langu Kanali Masawe

Mkuu wa mkoa wa Kagera kanali mstaafu Fabiani Massawe wa kwanza kulia akiangalia moja ya ndizi ambayo inapatikana katika shamba lake ambalo lina migomba yakutosha lililopo Kayanga wilayani Karagwe m,koani hapa

Shamba hilo alilianzisha wakati alipokuwa wilayani hapo akiwa ni mkuu wa wilaya hiyo lakini kwa sasa kanali Massawe ni mkuu wa mkoa wa Kagera, kilimo kwanza Baaaaana