Na.Kibuka Prudence,Ngara
Shirika la Maendeleo la Ubeligiji(BTC)kwa kushirikiana na Serikali
ya Tanzania limetumia zaidi ya shilingi bilioni 120 kwa ajili ya mradi
wa migomba unatekelezwa katika wilaya zote za Mkoa wa Kagera na Wilaya
ya Kibondo Mkoani Kigoma.
Hayo yamebainishwa na Afisa Miradi shirika hilo hapa nchini Cranme
Chiduo, wakati wa maadhimisho ya siku ya zao la ndizi yaliyofanyika
katika kijiji cha Rusumo wilayani Ngara ambayo yamefunguliwa rasmi na
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Massaawe.
Amesema tangu Mradi wa BTC yaani (Belgium Technical Corporation)
uanzishwe miaka minne iliyopita mbali na kutumia kiasi hicho cha fedha
pia umepata mafanikio makubwa katika usambazaji wa mbegu bora za migomba
na kuwasaidia wasindikaji na wasambazaji kuongeza thamani ya zao la
ndizi.
Katika maadhimishisho hayo Mratibu wa Mradi wa Migomba Mkoani
Kagera Mgenzi Byabachwezi alisema hadi Desemba mwaka jana zaidi ya miche
bora ya migomba milioni mbili imesambazwa kwa wakulima 46,000 katika
maeneo unapotekelezwa mradi huo.
Pia alisema mradi huo unaogharamiwa na Serikali za Ufalme wa
Ubeljiji naTanzania,ulianza kutekelezwa tangu mwaka 2009 kwa sambaza
miche ya migomba ambao umeweka mwamko endelevu wa kusindika mazao ya
migomba na utaalamu wa masoko.
Akizindua maonyesho hayo Mkuu wa Mkoa wa Kagera aliwataka wakulima
wa migomba kuachana na kilimo cha mazoea na kuelekeza nguvu kwenye
kilimo cha biashara.
Aidha,Massawe alitaka wakulima wapewe elimu ya ujasiliamali ili
kujipatia ujuzi ambao pia utawasaidia kupeleka mazao yao kwenye masoko
wao wenyewe bila kutegemea walanguzi wa mazao yao.
Hata hivyo Mkuu huyo wa Mkoa wa Kagera aliwaomba wafadhili wa Mradi
huo kuanzisha pia maadhimisho ya zao la mgomba katika mikoa mingine
nchini inayolima zao hilo.
Katika maadhimisho hayo Massawe pia aliiasa jamii kuachana na tabia
ya utegemezi wa wafadhili na kuwa baada ya kusaidiwa katika hatua za
awali tunalazimika kujitegemea wenyewe.
Mwisho
No comments:
Post a Comment