Wednesday, April 4, 2012

Mmeisoma Hii Ma Bloggers?

Tanzania Blog Awards: Nominations Are Accepted!

Hi Tanzanian Bloggers!

Natumaini wote hamjambo. Ninataka kuwaambia kuwa tumeanza kupokea majina ya mapendekezo ya blogs ambazo zinataka kushiriki katika shindano letu la mwaka huu. Form zimewekwa kwenye blog yetu toka tarehe 1 mwezi wa 4 na tutapokea mapendekezo hayo mpaka tarehe 31 mwezi wa 5. Hatutaengeza muda kama mwaka jana.

Sasa hivi ninavyoandika form hii imeshajanzwa mara 206. Inaelekea mwaka huu watu wengi watashiriki hivyo tafadhali ombi letu ni hili kama unataka blog yake ishiriki please do your part. Sisi tuna emal za bloggers kama 120 hivi. Nitawatumia wote lakini kwa wale wanaowafahamu wengine naomba waeleze. Mambo ya kulalamikiwa kama mwaka jana kweli hatutayaweza. Tuko hapa kwa kupromot blogs zote bila kujali hii ni blog ya nani au ile ni blog ya nani.

Sasa kama hao wachache watajishughulisha kuwatangazia wasomaji wao usitegemee miracles kuwa blog yako itashirikiswhwa tu bila kupendekezwa. Sisi tutachukua kama tunavyoona zinavyopendekezwa. Mambo ya kusema blog yangu ni maarufu sana huku niliko nashangaa kwanini hamkuishirikiswa sis hatuna saying katika jambo lolote hapa.

Tuanawasikiliza wasomaji wanaopendekeza majina haya. Halitakua kosa letu kwa blog yako kutoshirikishwa hapa.. Tunajitahidi kadiri ya uwezo wetu kutangaza kwenye sehemu mbali mbali. Na ndio maana tumeweka muda huo ili kila anayetaka kushiri na ashiriki

Hivyo tafadhali sana kama unataka ksuhiriki watangazie wasomaji wa blog yako wakupendekeze. Kama mnavyojua blogs ziitazopendekezwa kwa wingi ndio zitaingia kwenye shindano letu

No comments:

Post a Comment