Friday, April 20, 2012

Usalama Barabarani

Moja ya Arama za Barabarani ambazo ni muhimu kuzijua

Na Antidius Kalunde
Bukoba
 
WAMILIKI wa vyuo vya ufundishaji wa madereva wametakiwa kuacha kutanguliza maslahi yao binafsi kwa kutanguliza suala la biashara huku wakiwa hawatoi elimu bora kwa madeleva wanaowafundisha jambo ambalo linaendelea kusababisha ajali nyingi hapa nchini kutokana na vyuo kutokuwana sifa bora.
 
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa kamati ya usalama Barabarani mkoani Kagera Winstoni Kabantega wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya baadhi ya vyuo vinavyotoa elimu kwa madeleva kutokuwa na sifa za ufundishaji.
 
Alisema kuwa kwa hivi sasa vyuo vingi vinatoa madereva ambao hawana sifa za kutosha kutokana na wamiliki kutanguliza pesa bila kujali matatizo yanayoweza kutokeza badae mara baada ya madeleva hao kumaliza masomo.
 
Aidha ameiomba serikali kupitia wizara ya mambo ya ndani ya nchi chini ya jeshi la polisi kuhakikisha inapitia kila chuo na kuangalia kama kina sifa za kutosha katika ufundishaji kwani bila kufanya hivyo tatizo la madereva wazembe haliwezi kumalizika huku wananchi wakiendelea kupoteza maisha ya vilema visivyotarajia.
 
Katika hatua nyingine Kabantega amezungumzia suala la kuhepuka ajali ni lakila Mtanzania kwani wananchi inawabidi kushirikiana na jeshi la polisi kuhakikisha taarifa za wamiliki wa vyuo visivyokuwa na sifa ya kutosha katika kuzalisha madeleva vinafungwa.
 
Akielezea wiki ya nenda kwa usalama barabarani ambayo kitaifa ilifanyika mkoani kagera kuanzia tarehe 3 october hadi tarehe 8 mwaka jana, alisema kuwa wananchi wa mkoa wamejifunza mengi kutokana na maadhimisho hayo na kujua sheria jambo ambalo litaendelea kuounguza ajali kwa mkoa huo.
 
Aliongeza kuwa katika takwimu  za hivi karibuni zimeonyesha kuwa mkoa wa Kagera ni mmoja ya mikoa minne ambayo imepunguza tatizo la ajali za barabarani kutokana na elimu inayotolewa na kikosi cha usalama barabarani cha polisi kwa kushirikiana na vyuo vya madeleva ambavyo vina sifa ya kutosha.
 
Katika hatua nyingine Kabantega alilitaka jeshi la Polisi kupitia kikosi cha usalama barabarani kufuata sheria sahihi kuliko kuendelea kuendekeza vitendo vya rushwa ambavyo vikiendelea udhibiti wa madeleva wazembe utakuwa mgumu.
 
MWISHO

No comments:

Post a Comment