Lissu
apangua hoja za CCM kwa masaa 3 na nusu (3:30) : kauli ya mwisho
anayosema ni kuwa katika tuhuma zote zilizoletwa mahakamani, hakuna
ushahidi hata mmoja wa mawakala wa CCM, au wapiga kura wa CCM
waliolalamika kuwa kulikuwa na vitendo vya uvunjaji wa sheria.
Hakuna
hata wakala mmoja wa CCM aliyejaza fomu namba 14 ya kutoridhika na
upigaji kura. Sheria za uchaguzi zinasema wakala ajaze fomu kuonyesha
kuwa ameridhika au hajaridhika na kulalamikia tuhuma iliyoletwa
mahakamani.
Jambo la pili Hakuna wakala hata moja aliyejaza fomu namba 16 ambaye hakuridhika na zoezi la kuhesabu kura na kutangaza matokeo
Tatu:
Hakuna ushahidi wowote wa nyaraka, kuonyesha kuwa CCM au mgombea wao wa
Ubunge, au diwani, au wakala wao aliyelalamika kwenye kamati ya maadili
ya uchaguzi ya Jimbo la Singida mashariki, au kwa jambo lolote lile.
Na
hakuna ushahidi wowote uliotolewa wa malalamiko yeyote. Ushahidi
uliotolewa wa Bw. Robert Kimanda, anadai kuwa aliwahi kusema kuwa
alijaza. Lakini shahidi aliyefuata alisema kuwa baada yakugundua kuwa
CCM wameshinda katika kituo alichosimamia, aliichana fomu hiyo. Kuna
malalamiko mengi lakini mengi yanatokana na umbumbumbu wa kutojua sheria
za uchaguzi.
Kutokuwepo
kwa malalamiko kunaonyesha kuwa hakukuwepo tatizo, kesi imetengenezwa
baadaye na watu walioshindwa kwenye uchaguzi. Mheshimiwa jaji, Mashahidi
walipingana, wengine walisema walioleta mashataka ni waongo.
Kama
mashahidi wa upande wa walalamikaji wanaitana waongo mheshimiwa jaji,
kuna nini chakuongeza? Shahidi namba 16, alisema waleta maombi ni
waongo.
Kwa hisani ya Josephat Isango
Kwa hisani ya Mjengwa Blog
No comments:
Post a Comment