Thursday, April 26, 2012
Miaka 48 Ya Muungano Tanganyika na Zanzibar
Muungano huu ni muhimu KuudumishaMiaka Yote Hongereni Tanganyika na zanzibar Kwa kuungana na kuzaa Tanazania
Wazo Langu Kwa Leo
Baadhi Ya warembo Wa Tanzania wakiwa Katika Vazi La Kanga Moja Imependeza Saaaaaana
PICHA KWA HISANI YA MJENGWA BLOG
KWAKWELI AKINA MAMA NI MUHIMU SAAAANA
PICHA KWA HISANI YA MJENGWA BLOG
Hivi kama mugu angeliumba wanaume peke yao ingekuwaje? wanaume wangetembea Uchi kwakuwa hakuna jinsia nyingine?Je kungekuwa na umuhimu wakujituma na kufanya kazi?Je watu ambao mungu angewaumba wasingeongezeka kutokana na kutokuwepo akina Mama ambao ndio wanauwezo wa kuzaa/ au mungu angewapa wanaume uwezo wa Kuzaa?
Uvccm Arusha Kasheshe Katibu afungiwa Ofisi
HALI ya Siasa Mkoa wa arusha hususan kwa Umoja wa Vijana (UVCCM) ni
tete baada ya vijana hao kuchukua uamuzi wa kufunga ofisi ya umoja
huo pamoja na kubandika mabango usiku wa kumkia leo .
Mabango hayo yalikuwa yakimshinikiza Katibu wa UVCCM Mkoa wa Arusha,
Abdallah Mpokwa kuondoka na kumfuata aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM
,James Ole Millya ambaye amehamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) na mengine yakimtuhumu Millya kuwa ni fisadi .
Wakizungumza na waandishi wa habari baadhi ya vijana wa umoja huo
mkoani hapa ambao ni Ally Shabani maarufu kwa jina la Majeshi ambaye ni
Katibu wa UVCCM Kata ya Moivo pamoja na Masoud Rajabu ambaye ni
Katibu wa UVCCM kata ya Lemara walisema wamechukizwa na kauli ya
Mpokwa aliyoitoa janajuu ya kumsafisha Millya kwa madai hana ushahidi
wa hela Sh. milioni 2 iliyotolewa kwa ajili ya kuanzishwa kwa saccos
hiyo.
Shabani alisema kauli aliyoitoa juzi Mpokwa kuwa UVCCM haijawahi
kuwa na mradi wa SACCOS na pia kukanusha suala la Millya kutakiwa
kukabidhi ofisi mara alipoondoka na kujiunga na Chama cha Demokrasia
na Maendeleo(Chadema).
Alisema kitendo cha Mpokwa kudai kuwa kisheria Millya hakuwa na
ofisi ila alikuwana kazi ya kufungua mikutano hivyo tuhuma hizo
hazimhusu pia suala la SACCOS halijawahi kuwepo katika kumbukumbu
za ofisi zao na wala hakuna mtu aliyekatiwa risiti wala kuonyesha
mahali popote mtu wa umoja huo kama alipokea.
Alisema kutokana na kujitoa kwake na wengine wanaoendelea kuondoka
katika Umoja huo, Umoja huo haujatetereka na wala hautatetereka na
sasa wanajiandaa na uchaguzi wa ngazi zao zote.
Majeshi alihoji ni kwanini Mpokwa amtetee Millya kuhusu suala la
fedha na mambo mengine hivyo uamuzi wa vijana kufunga ofisi hiyo ni
sahihi kwani tamko alilolitoa halina mashiko na kama vijana hawamtaki
tena kuongoza umoja huo.
Alisema haiwezekani hela za miradi ya UVCCM ziliwe kama mchwa kwenye
kichuguu hivyo hawamtaki Mpokwa na kusisitiza kuwa amfuate Millya huko
aliko
Mpokwa amekiuka taratibu za UVCCM kwakumuunga mkono Millya hivyo
hawamtaki awaongoze vijana hao kwani yeye ni mamluki anayetumiwa na
Millya kuhakikisha anaharibu umoja huo .
Naye Rajab aliongeza kuwa wanamhitaji mlezi wa Chama hicho Mkoani
hapa, Steven wassira aje kurekebisha kasoro zilizopo kwa vijana kwani
awali Wassira alifika kutatua makundi yenye mgogoro kwenye vikao na
kupokea taarifa zisizo sahihi hivyo safari hii kama atakuja
awakutanishe vijana wote ili kutatua migogoro mbalimbali ya umoja huo
ikiwemo ulaji wa fedha za miradi mbalimbali ya UVCCM.
Hata hivyo vijana wa umoja huo walionekana wakiwa makundi makundi kila
mmoja akimvizia mwenzie kuona ni nani atavunja ofisi hiyo huku wengine
wakidai mtu akisogea kufungua makufuli hayo waliyoweka watahakikisha
wanapigana na kusisitiza Mpokwa kuondoka kwani hawamhitaji tena.
Vijana hao walichukua hatua hiyo baada ya Mpokwa kumsafisha Millya kwa
madai kuwa alihama chama kwa matakwa yake na pia hakukuwa na saccos
kama ilivyodaiwa hapo awali .
Na Ashura Mohamed

Tusikilize Hukumu ya Taylor Leo
Majaji katika mahakama maalum kuhusu
vita nchini Sierra Leone, leo watatoa hukumu dhidi ya aliyekuwa Rais wa
Liberia Charles Taylor kwa kuhusika na vita hivyo vilivyodumu miaka
10.
Taylor anakabiliwa na mashtaka 11 ikiwemo ubakaji na mauaji ya raia wa Sierra Leone.
Ikiwa atapatikana na hatia atakuwa rais mstaafu wa kwanza kuhukumiwa na mahakama ya kimataifa.
Kiongozi huyo wa zamani anadaiwa kufadhili waasi wa RUF.
Zaidi
ya mashaidi 100 wamefika mbele ya mahakama hiyo lakini Bw Taylor
amekanusha kuhusika na uhalifu huo wakivita na anadai kuwa kesi hiyo ni
njama ya kummaliza kisiasa.
Hukumu
ya majaji hao inasubiriwa kwa hamu sana na raia nchini Sierra Leone
ambao jamaa zao waliathirika sana wakati wa vita hivyo.
Inakadiriwa
kuwa zaidi wa watu elfu 50 waliuawa na wengine wakiwemo wanawake na
watoto walibakwa na kukatwa mikono au miguu na waasi wa RUF ambao
upande wa mashtaka unasema walipata usaidizi wa silaha kutoka kwa Bw
Taylor.
Wakati
wa vita hivyo, mwendesha mashtaka anasema kuwa Taylor alikuwa kiungo
muhimu katika biashara haramu ya almasi kutoka Sierra Leone.
Kesi
hii iliodumu miaka mitatu na nusu, hata hivyo huenda isi kamilike leo
kwani pande zote wanauhuru wa kukata rufaa ikiwa hukumu hiyo
haitawaridhisha.
chanzo:BBC
chanzo:BBC
Sunday, April 22, 2012
RTO Kagera na watumishi Wa Lake Zone Driving School
Walimu wa Chuo cha udereva akiwemo mkurugenzi wa chuo hicho Winstoni Kabantega akiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoani kagera Malisoni Mwakyoma na baadhi ya askari wa usalama barabarani
Mkurugenzi wa Lake Zone driving School Winstoni Kabantega akiwa na baadhi ya walimu wa chuo hicho akiwapa maelekezo juu ya ufundishaji wa madereva hivi karibuni
PC Fadhili akiwa na Coplo Safari(mwenye sale ya Polisi) wakikagua moja ya gari ambalo linatumika kufundishia mafundi makenika wakiwemo madereva katika chuo cha Lake zone Driving School

Mkaguzi wa magari mkoani Kagera akikagua katika chuo Cha Lake Zone
Mkaguzi wa Magari kutoka kikosi cha usalama barabarani mkoani Kagera PC Samweli akikagua magari yanayotumika kufundishia madereva katika chuo cha Lake zone Driving School mjini Bukoba nyuma ni moja wa Mkufunzi wa chu hicho.
Baaddi ya walimu wa Chuo cha Lake Zone Driving School wakiwa katika picha ya pamoja na mkaguzi wa magari katikati yao PC Samweli
Saturday, April 21, 2012
Mkuu Wa Trafiki Kagera Atembelea Chuo Cha Mafunzo Ya Udereva
Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Malisoni Mwakyoma akiwasili katika chuo cha mafunzo ya udereva cha Lake Zone Driving School akipokelewa na Mkurugenzi wa Chuo hicho Winstoni Kabantega
Mkurugenzi wa chuo hicho Winsoni Kabantega akitoa maelezo kwa Mwakyoma juu ya ufundishaji kwa mafundi wa magari akionyesha gari linalotumika kuwafundishia.
Mkurugenzi wa chuo hicho Winsoni Kabantega akitoa maelezo kwa Mwakyoma juu ya ufundishaji kwa mafundi wa magari akionyesha gari linalotumika kuwafundishia.
Wanafunzi Wa Chuo Cha Udreva Cha Lake Zone
Wanafunzi wa chuo Cha Lake Zone kilichopo Mjini Bukoba wakiwa wanapata maelezo juu ya usalama barabarani kutoka kwa mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoani Kagera
Mkuu wa Kikosi Cha Usalama Barabara Mkoani Kagera Malisoni Mwakyoma akikagua wanafunzi wa Lake Zone Driving School na nyuma yake ni mkurugenzi wa chuo hicho Winstoni Kabantega
Mwakyoma (RTO )akiwa na Mkurugenzi wa Lake Zone pamoja na askari wa kikosi cha usalama barabarani mkoani Kagera wakiangalia jinsi ya uendeshaji na ubebaji wa pikipiki za abilia

Kilimo Cha Migomba Kuboreshwa Kagera
Mratibu wa Mradi wa migomba unaofadhiliwa na Serikali ya Tanzania na
Ubeligiji Mgenzi Byabachwezi akitoa maelezo ya jinsi ya kudhibiti
magonjwa yanayoshambulia migomba kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali
Mstaafu Fabian Massawe alipotembelea shamba la kikundi cha Mshikamano
Kata ya Magoma Wilayani Ngara wiki hii. PICHA NA PHINIAS BASHAYA
Na.Kibuka Prudence,Ngara
Shirika la Maendeleo la Ubeligiji(BTC)kwa kushirikiana na Serikali
ya Tanzania limetumia zaidi ya shilingi bilioni 120 kwa ajili ya mradi
wa migomba unatekelezwa katika wilaya zote za Mkoa wa Kagera na Wilaya
ya Kibondo Mkoani Kigoma.
Hayo yamebainishwa na Afisa Miradi shirika hilo hapa nchini Cranme
Chiduo, wakati wa maadhimisho ya siku ya zao la ndizi yaliyofanyika
katika kijiji cha Rusumo wilayani Ngara ambayo yamefunguliwa rasmi na
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Massaawe.
Amesema tangu Mradi wa BTC yaani (Belgium Technical Corporation)
uanzishwe miaka minne iliyopita mbali na kutumia kiasi hicho cha fedha
pia umepata mafanikio makubwa katika usambazaji wa mbegu bora za migomba
na kuwasaidia wasindikaji na wasambazaji kuongeza thamani ya zao la
ndizi.
Katika maadhimishisho hayo Mratibu wa Mradi wa Migomba Mkoani
Kagera Mgenzi Byabachwezi alisema hadi Desemba mwaka jana zaidi ya miche
bora ya migomba milioni mbili imesambazwa kwa wakulima 46,000 katika
maeneo unapotekelezwa mradi huo.
Pia alisema mradi huo unaogharamiwa na Serikali za Ufalme wa
Ubeljiji naTanzania,ulianza kutekelezwa tangu mwaka 2009 kwa sambaza
miche ya migomba ambao umeweka mwamko endelevu wa kusindika mazao ya
migomba na utaalamu wa masoko.
Akizindua maonyesho hayo Mkuu wa Mkoa wa Kagera aliwataka wakulima
wa migomba kuachana na kilimo cha mazoea na kuelekeza nguvu kwenye
kilimo cha biashara.
Aidha,Massawe alitaka wakulima wapewe elimu ya ujasiliamali ili
kujipatia ujuzi ambao pia utawasaidia kupeleka mazao yao kwenye masoko
wao wenyewe bila kutegemea walanguzi wa mazao yao.
Hata hivyo Mkuu huyo wa Mkoa wa Kagera aliwaomba wafadhili wa Mradi
huo kuanzisha pia maadhimisho ya zao la mgomba katika mikoa mingine
nchini inayolima zao hilo.
Katika maadhimisho hayo Massawe pia aliiasa jamii kuachana na tabia
ya utegemezi wa wafadhili na kuwa baada ya kusaidiwa katika hatua za
awali tunalazimika kujitegemea wenyewe.
Mwisho
Friday, April 20, 2012
Ngeleja Nakusikiliza Ndugu Mwakilishi UN
Waziri wa Nishati na Madini Mh. William Ngeleja (kulia) amekutana na Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania Bw. Alberic Kacou ofisini kwake jijini Dar es Salaam muda mfupi kabla ya kuelekea Dodoma ambapo vikao vya Bunge vinaendelea.
Mh. Ngeleja amekutana na Mwakilishi huyo baada ya kuwasili kutoka katika mkutano wa kimataifa ulioandaliwa na Umoja wa Mataifa unaohusu Nishati uliofanyika nchini Ubelgiji.
Mh. Ngeleja aliiwakilisha Tanzania katika sekta ya Nishati ambapo Umoja wa Mataifa unategemea Nishati kuwafikia watu wote ifikapo Mwaka 2030.
Mh. Ngeleja amesema kuwa pamoja na changamoto zilizopo haswa upatikanaji wa fedha, Serikali ya Tanzania imedhamiria kusambaza nishati nchini Tanzania (yenye watu zaidi ya milioni 45) kutoka asilimia 18.5 hadi asilimia 30 ifikapo mwaka 2015.
Naye Mwakilishi wa Umoja wa Matifa amemshukuru Waziri kwa jitihada zake kupitia wizara hiyo na akasisitiza kuwa Nishati kwa kila mtu ni haki ya msingi hivyo uharakishwaji wa mpango huo wa nishati kwa wote upewe umakini mkubwa.
Pia ameahidi kufikisha maombi ya Waziri wa Nishati ikiwa ni pamoja na kuondolewa vikwazo vya upataji wa fedha kwa nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki Moon.
Kusoma zaidi: http://tz.one.un.org
Imetolewa na Ofisi ya Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa – Afisa Mawasiliano.
Viongozi Wa Dini Wafanya Semina Ya Sensa
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi Ramadhani Khijjah akizungumza na viongozi mbalimbali wa dini kuelezea umuhimu na ushiriki wao katika kufanikisha sensa ya watu na makazi itakayofanyika kitaifa mwezi Agosti mwaka huu wakati wa mkutano wa viongozi wa dini unaoendelea jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi Ramadhani Khijjah (kushoto) akiandika maswali yaliyoulizwa na viongozi wa dini kuhusu namna serikali ilivyojipanga kukamilisha sensa ya watu na makazi itakayofanyika mwezi Agosti 2012. Wengine ni mkurugenzi mkuu wa ofisi ya taifa ya takwimu Dkt. Albina Chuwa (katikati) na kamishna wa sensa Bi. Hajjat Amina Mrisho.

Baadhi ya viongozi wa dini wanaoendelea na mkutano wao jijini Dar es salaam wakipitia vitabu na vipeperushi vyenye jumbe mbalimbali kuhusu zoezi la sensa ya watu na makazi litakalofanyika nchi nzima mwezi Agosti mwaka huu baada ya wataalam kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu kutoa semina fupi kuhusu ushiriki wa viongozi hao katika kufanikisha sensa hiyo
Na Aron Msigwa MAELEZO
Usalama Barabarani
Moja ya Arama za Barabarani ambazo ni muhimu kuzijua
Na Antidius Kalunde
Bukoba
WAMILIKI wa vyuo vya ufundishaji wa madereva wametakiwa kuacha kutanguliza maslahi yao binafsi kwa kutanguliza suala la biashara huku wakiwa hawatoi elimu bora kwa madeleva wanaowafundisha jambo ambalo linaendelea kusababisha ajali nyingi hapa nchini kutokana na vyuo kutokuwana sifa bora.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa kamati ya usalama Barabarani mkoani Kagera Winstoni Kabantega wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya baadhi ya vyuo vinavyotoa elimu kwa madeleva kutokuwa na sifa za ufundishaji.
Alisema kuwa kwa hivi sasa vyuo vingi vinatoa madereva ambao hawana sifa za kutosha kutokana na wamiliki kutanguliza pesa bila kujali matatizo yanayoweza kutokeza badae mara baada ya madeleva hao kumaliza masomo.
Aidha ameiomba serikali kupitia wizara ya mambo ya ndani ya nchi chini ya jeshi la polisi kuhakikisha inapitia kila chuo na kuangalia kama kina sifa za kutosha katika ufundishaji kwani bila kufanya hivyo tatizo la madereva wazembe haliwezi kumalizika huku wananchi wakiendelea kupoteza maisha ya vilema visivyotarajia.
Katika hatua nyingine Kabantega amezungumzia suala la kuhepuka ajali ni lakila Mtanzania kwani wananchi inawabidi kushirikiana na jeshi la polisi kuhakikisha taarifa za wamiliki wa vyuo visivyokuwa na sifa ya kutosha katika kuzalisha madeleva vinafungwa.
Akielezea wiki ya nenda kwa usalama barabarani ambayo kitaifa ilifanyika mkoani kagera kuanzia tarehe 3 october hadi tarehe 8 mwaka jana, alisema kuwa wananchi wa mkoa wamejifunza mengi kutokana na maadhimisho hayo na kujua sheria jambo ambalo litaendelea kuounguza ajali kwa mkoa huo.
Aliongeza kuwa katika takwimu za hivi karibuni zimeonyesha kuwa mkoa wa Kagera ni mmoja ya mikoa minne ambayo imepunguza tatizo la ajali za barabarani kutokana na elimu inayotolewa na kikosi cha usalama barabarani cha polisi kwa kushirikiana na vyuo vya madeleva ambavyo vina sifa ya kutosha.
Katika hatua nyingine Kabantega alilitaka jeshi la Polisi kupitia kikosi cha usalama barabarani kufuata sheria sahihi kuliko kuendelea kuendekeza vitendo vya rushwa ambavyo vikiendelea udhibiti wa madeleva wazembe utakuwa mgumu.
MWISHO
Rais Kikwete Amaliza Ziara Brazil
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na wajumbe wa chama cha wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa wa nchi ya Brazil alipokutana nao katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kikazi jijini Sao Paulo April 19, 2012.PICHA NA IKULU
Thursday, April 19, 2012
Wabunge Ambao Wanaanza Inawabidi kuwasikiliza Wakubwa
Waziri Mkuu Mizengo Pinda Akizungumza na mbunge Mpya wa Jimbo La Arumeru Mashariki Joshua Nassari(CHADEMA) kabla ya kuanza Kikao cha Bunge Leo Mjini Dodoma hapa kama walivyokutwa na Mpiga picha wetu katika viwanja vya Bunge
Wednesday, April 18, 2012
Mkutano Wa Viongozi wa Waislamu Na Wakristo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya viongozi wa dini alipowasili kwenye Hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam,kwa ajili ya kufungua Kongamano la Dini la Waislam na Wakristo, lililoanza jana Aprili 18, 2012
Kaka Mjengwa Hata mimi Nimeipenda Hii Sheria
Sheria ya Uasalama barabarani hairuhusu pipiki za abilia kupakia watu watatu kwa upande wa raia ila Polisi Ruksa kupakiwa wawili akiwemo dreva wao. MTUNGA SHERIA NDIE..................................
PICHA KWA HISANI YA MJENGWA
PICHA KWA HISANI YA MJENGWA
Msitu Mnene Lakini Ni Hifadhi Ya Taifa Je Tunailinda?
Hapa ni Msitu wa pori la Kikulula Ranchi lililoko Katika wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera na ni moja ya eneo ambalo linatumika kulishia mifugo aina mbalimbali zikiwemo N'GOMBE aina ya Kongwa BEEF Lakini kama kawaida ya Mtu mzima kutembelea maeneo kama haya.
Hili Nalo Ni Daraja Wananchi Wanalitumia Kupita
Moja ya Daraja ambalo linaonekana halifai kwa matumizi ya wananchi hasa kupita na kuvuka kwani halina usalama wowote ule na halieleweki,hapa ni wilayani Karagwe mkoani Kagera katika kata ya Kihanga barabara ya kuelekea Kikulula ranchi.
MADIWANI MULEBA WAPITISHA BAJETI YA MWAKA WA FEDHA 2012/13
Na Antidius Kalunde
Muleba
MADIWANI wa halmashauri ya wilaya ya Muleba mkoa wa Kagera Wamepitisha bajeti ya mwaka 2012/13, ambapo zaidi ya shilingi Bilioni 41.1 zinatarajia kukusanywa kutoka vyanzo mbalimbali ikiwemo ruzuku ya serikali.
Bajeti hiyo iliyowasilishwa na mwenyekiti wa halmashauri hiyo , George Katomero iliridhiwa na baraza baada ya kujadiliwa kwa siku mbili April 14/15 na hivyo kutoa nafasi kwa wajumbe wa baraza hilo kuifanyia marekebisho katika masuala kadhaa, ikiwemo matumizi ya mapato yanayotokana na nyanzo vya ndani.
Awali akiwasilisha makadirio ya bajeti hiyo Bw. Katomero alisema kati ya fedha hizo zinazotarajiwa kukusanywa huo, zaidi ya bilioni 3.2 zinatokana na vyanzo vya ndani, huku nyingine zikitarajiwa kupatikana kupitia ruzuku ya serikali kuu na wahisani.
Hata hivyo madiwani hao wamekubaliana kwamba kiasi cha shilingi bilioni moja zitumike katika miradi ya maendeleo badala ya milioni 527.1 zilizotengwa awali kwa miradi lengo likiwa kuboresha maisha wa wakazi wa wilaya hiyo.
Mmoja wa madiwani hao, Justus Magongo wa kata ya Muhutwe alisema hakuna sababu ya halmashauri kutegemea kwa kiasi kikubwa fedha za ruzuku zinazotewa na serikali kuu kwa madai kuwa sio za uhakika katika upatikanaji wake, na kuwa wakati mwingine uletwa kwa kuchelewa.
Aidha madiwani hao waliitaka halmashauri kuongeza nguvu katika ukusanyaji wa mapato ili kufikia lengo hasa kutokana na bajeti ya mwaka huu kuwa na ongezeko la takribani shilingi bilioni 15 kutoka shilingi 26,236,096,906 kwa mwaka 2011/12 hadi kufikia shilingi 41,118,283,893 mwaka 2012/13.
Mwisho
WANA JANGWANI WENZANGU
Kwanza nawapa pole wana Yanga wenzangu kwa kushindwa kufanya vizuri katika mechi za misho wa ligi kuu Tanzania Bala lakini siku za hivi karibuni katika kanda ya ziwa mmepoteza michezo yote miwili mechi ya kwanza timu ya toto African ya Mwanza aliwachapa kwa magolo 3 kwa 2 na siku ya jana timu ya Kagera sugar ya mjini Bukoba iliwapiga goli Moja kwa bila pamoja na kuonyesha mpira mzuri lakini matokeo yakawa vile
Cha msingi ni kuweka jitihada zaidi na kujiandaa upya katika michuano ijayo imekuwa ni mara ya Kwanza kwa timu yetu hii nzuri kufanya vibaya katika kipindi cha mwisho wa ligi kuu ya Tanzania bala.
Msikate tamaa bado wapenzi wenu tuko pamoja haya ni matoeke katika michezo wala hakuna haja ya kuwa na hasira ya aina yoyote ile bado twawapenda wana jangwani
By Kalunde
Friday, April 13, 2012
NILIPOKUTANA NA GAZETI HILI LEO NIMEOGOPA AJINYONGA......
NIPASHE:LEMA APEWA CHOPA KIJENGA CHADEMA
Na Sharon Sauwa
12th April 2012
Aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema
Hayo yalisemwa jana na Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe, alipokuwa akihutubia umati wa watu uliofurika katika uwanja wa Barafu mjini hapa.
Mbowe alisema Lema amevuliwa ubunge katika hali ya kutatanisha, lakini wanaamini kuwa haki itatendeka kutoka kwa majaji wa Mahakama ya Rufaa watakapoisikiliza rufaa yao.
Alisema iwapo Mahakama ya Rufaa itabariki maamuzi ya Mahakama Kuu, watakwenda katika uchaguzi na wanaamini kuwa watashinda kwa kishindo.
“Ninajua mna hamu ya kusikia kuhusiana na mbunge wenu Lema, (wananchi wanaitikia ndiyo), tumempatia kazi maalum kwa kumpa helikopta, muziki mkubwa na matarumbeta,” alisema.
“Anakwenda kuamsha ari ya mageuzi nchini, hakuna kulala hadi kieleweke. Wangejua ni balaa kwa hili walilolifanya wangemuacha bungeni,” aliongeza Mbowe huku akishangiliwa na umati wa watu.
Aidha, Mbowe alisema mara baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Saba wa Bunge, wabunge wote wa chama chake watakwenda mjini Mwanza kuandaa maandamano makubwa ambayo yatalenga kupinga unyanyasaji unaodaiwa kufanywa na polisi kwa wabunge wao wawili.
Wabunge hao ni Mbunge wa Ukerewe, Salvatory Machemli na Mbunge wa Ilemela, Highness Kiwia walipigwa mapanga usiku wa kuamkia Aprili Mosi mwaka huu, wakati walipokuwa wakisambaza mawakala wa chama hicho katika uchaguzi wa udiwani Kata ya Kirumba.
Kwa upande wake, Mbunge mteule wa Arumeru Mashariiki, Joshua Nassari, alifananisha kitendo cha kumuengua ubunge wa Lema na kuchaguliwa kwake kuwa ni sawa na kuzuia mkuki bungeni na kuingiza bunduki aina ya SMG.
Alisema wabunge wa Chadema ambao yeye ameongeza nguvu, wamedhamiria kuirudisha nchi mahali ambapo Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, aliiacha na kuwataka wananchi kuwaombea ujasiri ili waweze kutekeleza majukumu yao.
Alisema hawezi kuingia bungeni na kupiga makofi wakati akinamama wanajifungulia katika mazingira mabaya na wanafunzi wanaendelea kukaa chini.
“Arumeru ina shida, CCM wanaleta magari manne yamejaa maji ya kuwasha, Arumeru wanashida ya magari ya kubebea wagonjwa wao wanaleta magari, wananiapisha kesho (leo) ngoma inaanza, hivyo hakuna kulala mpaka kieleweke,” alisema Nassari huku akishangiliwa na wananchi kwa kumuita ‘dogo janja’.
Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, alisema hawako tayari kuuziwa mbuzi katika gunia katika suala la uandaji wa katiba mpya.
Alisema kuwa chama chake kitachambua wasifu wa wajumbe wa Tume ya Kuandaa katiba Mpya na kuuweka hadharani ili watu waweze kufahamu.
Mkurugenzi wa Mambo ya Bunge wa chama hicho, John Mrema, alisema iwapo ripoti ya ukaguzi wa hesabu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), haitawekwa wazi bungeni katika mkutano huu, wao wataiweka hadharani ili umma uweze kufahamu kilichomo ndani ya ripoti hiyo.
Subscribe to:
Posts (Atom)