Monday, August 6, 2012

Yanga Yapeleka Kombe La Kagame Bungeni

Tanzania Kukagua Hesabu Za UN

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) ambaye pia ni Mkaguzi wa hesabu za Umoja wa Mataifa (UN) Ludovick Utouh akiongea na waandishi wa habari kuhusu Taasisi 10 za UN ambazo zitafanyiwa ukaguzi chini ya usimamizi wake ambapo watumishi 60 kutoka ofisini yake watafanya kazi hiyo. Kwa kipindi cha miaka sita nchi za Tanzania, China na Uingereza zimepewa jukumu la ukaguzi wa hesabu za UN.


Edwin Rweyumamu kutoka ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) akimkaribisha CAG ambaye pia ni Mkaguzi wa Hesabu za Umoja wa Mataifa (UN) Ludovick Utouh ili aweze kuongea na waandishi wa habari kuhusu Tanzania kupata nafasi ya kukagua hesabu za UN kwa kipindi cha miaka sita. Watumishi 60 kutoka ofisi ya CAG watafanya kazi ya kuzikagua taasisi 10 za UN. Chanzo: Picha na Anna Nkinda – Maelezo
Reactions::
Wachezaji wa Yanga wakiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri Mkuu , Fatuma Karume ,wabunge na Kocha wao wakiwa na Kombe lao la Kagame Bungeni mjini Dodoma.


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Mama Fatuma Karume wakishikilia Kombe la Kagame lililotwaliwa na Yanga hivi karibuni lililoletwa na wachezaji wa Yanga na Viongozi wao akiwemo Kocha wao mpya Tom Saintfiet Bungeni mjini Dodoma.


Mke wa Rais, marehemu Abeid Amani Karume Mama Fatuma Karume ambae ni Mfadhiri wa Yanga kwa pamoja wakiingia Bungeni pamoja na Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji kupeleka kombe la Kagame Bungeni.


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Mke wa Rais, Marehemu Abeid Amani Karume Mama Fatuma Karume kwenye Viwanja vya Bunge mjini Dodoma. Chanzo: Anna Nkinda, Maelezo

No comments:

Post a Comment