Tuesday, August 28, 2012

Matukio Mbalimbali


Baadhi ya viongozi wa LAVLAC wakiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa mashirika yaliyofadhili ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka wa LAVLAC.
Mkurugenzi wa mipango na mikakati wa benki ya Posta Tanzania, Bernadethe Gogadi akiwasalimia wajumbe walioudhuria ufunguzi wa mkutano wa LAVLAC uliofanyika kwenye ukumbi wa hoteli ya Bukoba Coop. iliyoko katika manispaa ya Bukoba, mkutano huo unazishirikisha halmashauri za wilaya na manispaa zinazoko kwenye ukanda ziwa victoria 130 toka katika nchi za Uganda, Kenya na Tanzania.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Misenyi, William Katunzi (kushoto) na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Karagwe, Kashunju Runyogote (kulia).
Baadhi ya viongozi mkoani Kagera walioudhuria ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa LAVLAC kutoka kulia ni diwani wa viti maalumu, Mulungi Kichwabuta (CCM), mbunge wa viti maalumu CHADEMA Conchester Lwamlaza, na mwisho kushoto ni Diwani wa viti maalumu wa manispaa ya Bukoba CHADEMA, Mama Mkono.
Bango linaloonyesha wadhamini wa mkutano wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa LAVLAC ulioandaliwa na halmashauri ya manispaa ya Bukoba ambao ni pamoja na Benki ya posta Tanzania (TPB) na mradi wa uwekezaji (UTT).Baadhi ya wajumbe walioudhuria mkutano wa LAVLAC.
Mkusanyiko wa waumini wa dhehebu la kiislamu wakiwa nje ya mahakama ya mkoa ya Kagera, walikusanyika kwa lengo la kusikiliza tuhuma zinazowakabili wenzao walikamatwa na jeshi la polisi kwa tuhuma ya kupinga kuhesabiwaBaadhi ya wiaslamu wengine waliokutwa kwenye viwanja vya mahakama kuwatetea waislamu wenzao waliokamatwa kwa tuhuma ya kupinga zoezi la sensa ya watu na makazi.
Baadhi ya waislamu wengine.
Waislamu wa wengine waliokuwa miongoni mwa walioukutwa kwenye viwanja vya mahakama.
Peter Mushi, katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) akifungua mkutano wa uchaguzi wa jumuia ya wazazi ya chama hicho uliofanyika kwenye viwanja vya mtakatifu Francis.

No comments:

Post a Comment