Thursday, August 23, 2012

U.W.T Bukoba Wafanya Mkutano Wa UchaguziMkuu wa mkoa wa Kagera Bi Ziporah Pangani, akiongea na wajumbe wa jumuia ya wanawake (UWT) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)wakati wa mkutano mkuu wa jumuia hiyo wa kuwachagua viongozi wapya uliofanyika kwenye ukumbi wa amtakatifu Francis, ulioko katika manispaa ya Bukoba.
Mwenyekiti wa UWT wa mkoa wa Kagera ambaye amestaafu nafasi hiyo akitoa hotuba wakati wa mkutano mkuu wa jumuia hiyo uliofanyika kwenye ukumbi wa mtakatifu FrancisMkuu wa wilaya ya Bukoba Bi. Ziporah Pangani na mkuu wa mwenyekiti wa jumuia ya wazazi wa mkoa wa Kagera walikuwa miongoni mwa walioudhuria mkutano mkuu wa jumuia hiyo.
Hali hii inaonyesha jinsi gani wanawake wanavyoithamini CCM.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa wazazi wa CCM wa wilaya ya Bukoba.
Makada wa CCM.Mama stella (kulia) na Mama Kyaishozi.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu wa jumuia ya wanawake ya wilaya ya Bukoba ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakifurahia jambo nje ya ukumbi wa mtakatifu Francis uliko katika manispaa ya Bukoba wakijadili jambo kabla ya kufanyika mkutano mkuu wa chama hicho wa kuwachagua viongozi wapya wa jumuia hiyo.
Mulungi Kichwabuta, diwani wa viti maalumu wa chama cha mapinduzi (CCM) akiwa na baadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu wa jumuia ya wanawake wa wilaya ya bukoba mjini, walioudhuria mkutano mkuu wa jumuia hiyo wa kiwachagua viongozi wapya.
Baadhi ya waandishi wa habari mkoani Kagera wanaohudhuria mafunzo ya uchokonozi yanayotolewa na mwandishi mkongwe Fili Karashani wakiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari toka mkoani Singida.

No comments:

Post a Comment