Thursday, August 23, 2012

Taarifa Kwa Umma                      JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
                    WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

                          TAARIFA KWA UMMA
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Khamis Sued Kagasheki amebadili taratibu za kuwapata wajumbe wa Bodi mbali mbali zilozoko chini ya Wizara. Kuanzia sasa Wajumbe wa Bodi hizo watapatikana kwa njia ya ushindani badala ya kuteuliwa moja kwa moja na Waziri.
Kwa sasa kuna Bodi nane (8) ambazo muda wake umeisha au unakaribia kuisha.Bodi hizo ni za za Taasisis/Mashirika yafuatayo;-
I. Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro
II. Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI)
III. Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI)
IV. Makumbusho ya Taifa
V. Chuo cha Mafunzo na Usimamizi wa Wanyamapori (MWEKA)
VI. Chuo cha Mafunzo ya Wanyamapori Pasiansi
VII. Wakala wa Mbegu za Miti (TTSA)
VIII. Bodi ya Leseni za Utalii (TTLB)
Watanzania wenye sifa za kuwa Wajumbe wa Bodi hizo wanatakiwa kupeleka maombi kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii.
Maelezo zaidi ya namna ya kupeka maombi yataweka kwenye magazeti na tovuti ya Wizara, www.mnrt.go.tz 

NB: BOFYA HAPA KAMA UNAHITAJI KUOMBA NAFAZI ZA UJUMBE WA BODI http://www.mnrt.go.tz
Reactions::

Mkurungenzi Wa Mashtaka (DPP)Afungua Semina Ya Wapelelezi.Polisi,Mahakimu,Na Majaji Jijini Dar es salaam

Mkurungenzi wa mashtaka (DPP)Dk.Ellezer Feleshi (kulia) akiongea na waandishi wa habari baada ya kufungua semina ya wapelelezi.polisi,mahakimu,na majaji,Dr Ellezer alisema mafunzo hayo yanahusu mbinu za kisasa za kukabiliana na uhalifu wa utakatishaji wa fedha,biashara madawa ya kulevya,utaifishaji wa mali zilizopatikana kwa njia ya haramu na masuala ya ugaidi,semina hiyo ilifanyika katika hotel ya Kunduchi Beach nje kidogo ya jiji la Dar es salaam jana.

Dkt. Mwakyembe Amsimamisha Kazi Mkurugenzi Mkuu wa BandariWaziri wa Uchukuzi Dkt. Harisson Mwakyembe amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari-TPA-Ndugu Ephrahim Mgawe pamoja na wasaidizi wake wawili ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili.

Wengine waliosimamishwa ni Meneja wa Mafuta ya Ndege Kurasini, Meneja wa JET na Meneja wa Oil Terminal kutokana na tuhuma za kupotea kwa mafuta na kuidanganya serikali kuhusu mafuta masafi na machafu.

Kutokana na kuwasimamisha kazi Wakurugenzi hao Dkt. Harisson Mwakyembe amemteua Injinia Madeni Kipange kukaimu nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA.

Kufuatia tuhuma hizo zinazofanywa Bandarini Dkt. Mwakyembe ameunda Tume wa ya watu saba kufanya uchunguzi kwa wiki mbili na kumpelekea taarifa ofisini kwake ili kubaini ukweli wa tuhuma hizo zikiwemo za wizi.

Pia ameagiaza kufikia Septemba Mosi mwaka huu malipo yote yafanyike benki ili kuondoa rushwa na wizi unaofanyika ndani ya Mamlaka hiyo.

Waziri Mwakyembe anachukua hatua hizo kutokana na wwadao wengi sasa hawaitumii Bandari ya Dar es salaam kupitisha mizigo yao kutokana na kutokuwa na imani na watumishi wake hatua inayoifanya serikali kukosa mapato.

Pia ameagiza kusimamishwa mara moja kwa Kampuni ya Singilimo ambayo inajihusisha na kazi ya kubeba mafuta machafu na badala yake itafutwe Kampuni nyingine.

No comments:

Post a Comment