Thursday, August 2, 2012

Picha Na Habari Mbalimbali


Afisa Michezo Mkoa wa Kagera Bw. Kepha Elias Aliyesimama wa Kwanza Kushoto Akiwa Katika Picha ya Pamoja na Timu ya Wasichana Mpira wa Miguu Kibaha Mkoani Pwani.
SERIKALI itakuwa inagawa ng’ombe 1500 kila mwezi kwa wananchi wa wilaya tatu za Mkoa wa Arusha kama kifuta jasho cha kupoteza kiasi cha karibu mifugo 800,000 iliyopotea kutokana na ukame na athari zake mwaka 2008/2009.

Katika uzinduzi huo uliohudhuriwa na viongozi wa Mkoa wa Arusha wakiwemo wakuu wa wilaya na wabunge wa mkoa huo, Rais Kikwete amegawa ng’ombe 500 kwa kundi la kwanza la wananchi ikiwa ni mitamba minne na dume moja la kisasa kwa kaya 16 za mwanzo.

Uzinduzi huo ni wa pili kufanywa na Rais Kikwete chini ya Mradi huo wa kwanza wa aina yake kubuniwa na Serikali katika historia na wenye thamani ya sh. Bilioni 12.9.

Februari 19, mwaka huu, Rais Kikwete alizindua Mradi kama huo katika Wilaya ya Loliondo kwenye sherehe zilizofanyika mjini Loliondo. Kesho Agosti 3, 2012 Rais Kikwete anatarajiwa kuendelea na zoezi hilo katika mji wa Loliondo.

Posted on: 03 Aug 2012Rais Jakaya Kikwete akimkabidhi ngombe mmoja wa wakaazi wa Monduli walioathririka na na ukame mwaka 2008/2009 ambapo walipoteza mifugo yao yote. Hafla hii imefanyika leo Monduli. Picha na IkulRais Jakaya Mrisho kikwete akizindua mpango wa kugawa ngombe 1500 kila mwezi kwa wananchi wa wilaya tatu za Mkoa wa Arusha kama kifuta jashp cha kupoteza kiasi cha mifugo 800,000 kutokana na ukame na athari zake mwaka 2008/2000Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akionyesha kitabu kiitwacho Lighting Fire kilichoandikwa na wanasayansi 31 Mabingwa wa Kitanzania baada ya kukizindua kwenye ukumbi wa Tume ya taifa ya Sayansi na Tekinolojia, Kijitonyama jijini Dar es salaam Agosti 2, 2012. Kushoto ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Makame Mbalawa na Kulia ni Rais wa Tanzania Academy of Science (TAAS), Profesa Esther Mwaikambo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)Mkuu wa Mkoa wa Kagera Alilazimika Kusimamisha Safari yake Sehemu Moja Wilayani Missenyi Kuuzima Moto Uliokuwa Unauunguza Mbuga Ili Kuyalinda Mazingira, Wananchi Tuige Mfano Huu.9Picha na Sylvester Raphael)

No comments:

Post a Comment