Sunday, August 5, 2012

Matukio Mbalimbali Mjini Bukoba


Maofisa wa benki ya posta tawi la Bukoba wakimfungua akaunti mmoja wa wakazi wa manispaa ya Bukoba waliofungua akaunti katika benki hiyo, benki hiyo inashiriki kwenye maonyesho ya nanenane yanayoendelea kwenye viwanja vya Kyakailabwa vilivyoko katika manispaa ya Bukoba.
Baadhi ya wakazi mkoani Kagera wakiwa kwenye banda la benki ya posta lililoko kwenye viwanja vya maonyesho ya nane vya Kyakailabwa wwakisubili kufungua akiba.
Mkuu wa wilaya ya Bukoba Bi. Zeporah Pangania akiongea na wafanyabiashara wa soko kuu la Bukoba, alikuwa akiwaelezea wafanyabiashara hao wakubali mpango wa halmashauri wa kuvunja soko la sasa na kujenga soko jipya.
Timu ya wafanyabiashara wa soko kuu la Bukoba iliyoteuliwa kuwasimamia wafanyabiashara walioko ndani ya soko hilo baada ya kuvunjwa kupisha ujenzi wa soko kuu la Bukoba jipya.

No comments:

Post a Comment