Tuesday, August 7, 2012

Polisi Kagera Yahimiza Madereva Wa Pikipiki Kujifunza Mafunzo Maalum



Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera akifunga mafunzo ya udereva yaliyotolewa na chuo cha udereva cha lake zone kwa kushirikiana na jeshi la polisi, mafunzo hayo yalitolewa eneo la Kaagya lililoko katika wilaya ya Bukoba mkoani Kagera,kushoto kwake ni Mkuu wa Trafik Kagera William Mkonda na kulia ni Mkurugenzi wa Lake Zone Winstoni Kabantega.
 
 
Na Mwandishi Wetu
Bukoba

JESHI la polisi kupitia kikosi cha usalama barabarani mkoani Kagera limewataka watumiaji wa vyombo vya moto hasa waendesha  pikipiki kuhakikisha wanapitia mafunzo maalum ya udareva ili kuweza kuhepusha ajali za kila mara ambazo kwa sasa zinawakumba watumiaji wa vyombo hivyo.

Wito huo umetolewa na mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoani Kagera mrakibu wa polisi William Mkonda wakati wa kufunga mafunzo maalumu ya udereva katika kata  Kaagya wilaya ya Bukoba na Kata Bunazi wilayani Missenyi yaliyoendeshwa na chuo cha Lake Zone Driving School cha mjini Bukoba.

Alisema kuwa kwa hivi sasa ajali nyingi ni za pikipiki zinasababishwa na baadhi ya madereva wazembe ambao hawataki kujifunza sheria za usalama barabarani ambazo kwa hivi sasa nyingine zinabadilika kila mara.

Mkoda alisema kuwa kuna madereva wengine wanazo leseni lakini wao ndio chanzo cha ajali za barabarani kwanbi hawapendi kujifunza mabadiriko ya baadhi ya sheria na kuongeza kuwa kwa hivi sasa jeshi hilo litahakikisha linawachulilia hatua kali au kuwafutia leseni watakaukuwa wazembe.

"Sisi tunajua hakuna anayeomba kupata ajali lakini kuna ajali nyingine ukiziangalia ni kutokana na uzembe wa dereva mwenyewe sasa mtu kama huyo ambaye hataki kujifunza kwanini usimchukulia hatua kali au ikiwezekan kumfutia leseni"alisema Mkonda.

Katika hatua nyingine kamanda mkonda amewataka wahitimu hao hasa madereva wa pikipiki kutokubali kutumika katika suala la uhalifu kwani waliowengi wamekuwa wakiwaendesha watu asmbao ni majambazi hasa usiku.

Alisema kuwa waendesha pikipiki wakiona mtu ambaye wanahisi ni mharifu watoe taarifa katika vyombo vya usalama ili kuweza kuwabaini na kuwataatharisha kuwa watu hao wanaweza kuwadhuru waendesha pikipiki wenyewe na kuwanyanganya vyombo hivyo.

Kwa upande wake  Mkurugenzi wa chuo cha udereva cha Lake Zone kilichoendesha mafunzoWinstoni Kabantega alisema jumla ya wahitimu 129 wamepatiwa mafunzo hayo maalumu ambao ni madereva wa pikipiki na magari wamejifunza sheria za usalama barabarani na watakuwa mabarozi wazuri kwa wale ambao hawajajifunza.

Mwisho


 
 
 
 
 

No comments:

Post a Comment