Tuesday, August 21, 2012

Picha Mbalimbali


Baadhi ya wakati wa manispaa ya Bukoba wakiadhimisha sikukuu ya Idd El Fitri kwenye hoteli ya kimataifa ya Bukoba Coop Hoteli inayomilikiwa na chama cha ushirika Kagera (KCU) iliyoko kwenye ufukwe wa ziwa Victoria.
Baadhi ya wakazi wa manispaa ya Bukoba wakila vitu ndani ya hoteli ya Paradise wakati wa sikukuu ya Idd El Fitri.
Vijana wakibembea kwenye mabebea ya manispaa ya Bukoba yaliyojengwa kwa hisani ya Rotary club ya Bukoba.
Mambo hayo! hii sio foleni ya jambo lolote bali ni baadhi ya vijana wakijimwaga kwenye ukumbi wa disco wa stone hoteli ulioko kwenye ufukwe wa ziwa victoria.
Baadhi ya wakazi wa manispaa ya Bukoba wakijivinjali kwenye ufukwe wa hoteli ya kimataifa ya Spice wakati wa sikukuu ya Idd.
Viburudisho mbalimbali vilivyokutwa kwenye ufukwe wa hoteli ya spice wakati wa maadhimisho ya sikukuu ya Idd el Fitri.
Na hawa walikutwa wakivinjali kwenye ufukwe wa hoteli ya Spice.
Mmoja wa wamiliki wa tovuti hii Margareth Mwesiga akijadili masuala ya arusi ya Edius Njunwa na Dr. Buberwa na mkewe kulia kwenye viwanja vya Bukoba Club vilivyoko katika manispaa ya Bukoba.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Askofu Mstaafu wa Jimbo la Dodoma Mhashamu Mathias Isuja katika sherehe za kuadhimisha miaka 10 ya Kijiji cha Matumaini cha Dodoma kinacholea watoto yatima, Agust 18, 2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Jengo la hospitali ya mkoa wa Kagera litakalotumiwa kutoa huduma ya tiba ya daraja la kwanza, linatoa matibabu kwa waginjwa wa nje na wanaolazwa, lina vyumba vya kulaza wagonjwa vyenye huduma zote vikiwemo viyoyozi, gharama ya chumba ni kati ya shilingi 30,000 hadi 75,000 kwa siku.
Mandhari ya jengo la hospitali huu ya mkoa linalotumika kutoa huduma ya tiba ya daraja la kwanza.
Mabasi haya hufanya safari zake kati ya mikoa mingine na mkoa wa kagera yalikuwa maeneo ya kituo kikuu cha polisi inadaiwa yalikiuka kanuni za sheria za usalama barabarani.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizindua kampeni ya uhamasishaji wa sensa ya watu na makazi kwenye viwanja vya mnazimmoja jijini Dar es salaam Agust 17,2012.Watatu kushoto ni Makamu wa Pili wa rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd na kulia kwake ni Kamishina wa Sensa, Hajati Amina Mrisho(Picha na Ofisi ya Waziri MkuuRais Jakaya Mrisho Kikwete akishiriki katika swala ya Magharibi kabla ya kushiriki katika futari aliyoandaliwa na wananchi wa Tanga jana Agosti 15, 2012 jijini TangaRais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea hati za utambulisho toka kwa balozi mpya wa Spain hapa nchini Mhe Luis Manuel Cuesta Civis leo Agosti 16, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na balozi mpya wa India hapa nchini Mhe Debnath Shaw baada ya kupokea hati zake za utambulisho leo Agosti 16, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam.
Mkuu wa mkoa wa Kagera Kanali mstaafu Fabian Massawe akiongea na waumini wa dhehebu la kiisilamu aliowaandalia futari kwenye viwanja vya Ikulu ndogo iliyoko katika manispaa ya Bukoba, alikwa akiwaeleza waapuuze waislamu wachache wanaotaka kukwamisha zoezi la sensa ya watu na makazi, alikuwa akiwaambia kuwa mungu ni mmoja.
Mmiliki wa Cable inayosambaza mawasiliano katika manispaa ya Bukoba, Mohamed akiagana na mkuu wa mkoa baada ya kula futari.
Askofu Buberwa wa kanisa la kiinjiri la kirutheri diosisi ya kaskazini Magharibi alikuwa ni miongoni wmwa wageni walioalikwa kushiriki kwenye futari iliyoandaliwa na mkuu wa mkoa, kulia kwake ni sheikh Haruna Kichwabuta.
Baadhi ya viongozi walioungana na mkuu wa mkoa kula futari aliyoiandaa kwa ajili ya waumini wa dini ya kiislamu.
Massawe katikati, kulia kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera Philip Kalangi na kushoto afisa wa ofosi ya mkuu wa mkoa, Mrisho.
Waumini wa dini ya Kiislamu na wageni waalikwa wakila futari iliyoandaliwa na Massawe kwenye viwanja vya Ikulu ndogo ya Bukoba.
Baadhi ya wageni walialikwa kula futari.
Baadhi ya wageni waalikwa wakila Futari, kulia ni anajulikana kwa jina maarufu la China na anayefuata anajulikana kwa jina la Cheyo.Mjumbe wa sekretarieti ya mkoa wa Kagera Fikir Kisimba (kulia) akiwa na wakuu wa wilaya nje ya viwanja vya ukulu ndogo ya Bukoba.

No comments:

Post a Comment