Thursday, August 2, 2012

Matukio Mbalimbali Katika picha


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama mzinga wa asili wa nyuki wadogo wakati alipotembelea banda la Magereza kwenye maonyesho ya Wakulima Nanenane Mjini Morogo Agosti Mosi, 2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)




Waziri mkuu, Mizengo Pinda akikagua mkungu wa ndizi katika maonyesho ya wakulima Nanenane Mjini Morogoro Agosti Mosi 2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)




Mstahiki meya wa halmashauri ya manispaa ya Bukoba Anatory Amani akifungua kikao cha baraza la madiwani wa manispaa hiyo leo.




Baadhi ya wakuu wa idara wa halmashauri ya manispaa ya Bukoba.




Mstahiki meya wa zamani wa manispaa ya Bukoba, Samweli Ruangisa na makamu wake kulia.




Baadhi wa wageni waalikwa toka kwenye mashirika mbalimbali walioko kwenye safu ya nyuma.




Baadhi ya wasikilizaji wa kikao cha baraza la midiwani.




Huyu mzungu alikuwa ni mmoja wa wataalamu wa manispaa waliohudhuria kikao hicho.




Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Sumve, Richard Ndassa kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Julai 31,2012.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)




Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Lushoto, Henry Shekifu (katikati) na Mbunge wa Viti Maalum, Leticia Nyerere kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Julai 31,2012.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu



Nyumba ya asili ya wahaya iliyokuwa inatengenezwa kwa nyasi maarufu kwa jina la Mshonge inapatikana maeneo ya Kamachumu, wilayani Muleba.




Vivutio vya utalii vilivyoko mkoani Kagera, hapa ni mapango ambayo utembelewa sana na watalii yako Maruku.




Maporomoko ya Kyamnene yaliyoko mkoani Kagera




Mihogo inayopatikana mkoani Kagera.




Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana viongozi wa madhehebu mengine ya dini walioalikwa kula futali aliyoiandaa mkoani Lindi.



Waalikwa wakipakua futari



Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishiriki katika swala ya Magharibi na waumini wengine wa Mkoa wa Lindi aliowakaribisha katika futari Ikulu ndogo ya Mkoani Lindi leo Julai 30,



Mkuu wa mkoa wa Mwanza mhandisi Evarist Ndikilo akifungua semina ya siku mbili iliyohudhuriwa na waandishi zaidi ya 160 toka kwenye mikoa minane, semina hiyo ilifanyika katika ukumbi wa hoteli ya Annox iliyoko katika jiji la Mwanza.




Baadhi ya waandishi wa habari walioshiriki kwenye semina ya siku mbili iliyokuwa inahusu masuala ya sensa na makazi iliyofanyika kwenye ukumbi wa Annox ulioko mkoani Mwanza.



Washiriki wengine wa semina ya sensa na makazi.




Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera akifunga mafunzo ya udereva yaliyotolewa na chuo cha udereva cha lake zone kwa kushirikiana na jeshi la polisi, mafunzo hayo yalitolewa eneo la Kaagya lililoko katika wilaya ya Bukoba mkoani Kagera.




Kalangi akiwa katika picha ya pamoja na mmoja wa wahitimu wa mafunzo ya udereva.




Mkurugenzi mkuu wa chuo cha udereva cha Lake zone Winston Kabantega akipewa zawadi ya kuku na wahitimu wa mafunzo ya udereva.




Baadhi ya wahitimu wa mafunzo ya udereva wakila kiapo.




Mafundi wakijenga daraja katika barabara za eneo la Kisasa kwenye Manispaa ya Dodoma Julai 29,2012. (Picha na Ofisi yaWaziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment