Tuesday, August 28, 2012

Mgomo Wa Madereva Mjini Bukoba wazidi Kuwatesa Wasafiri

 Ndani ya stendi ya Bukoba hamna gari dogo hata moja
 Makundi ya watu wanaosemekana ni madereva wakiwa wanajadili juu ya mgomo huo,
 Baadhi ya watu wanaofanya biashara ndani ya stendi wakiwa wamekaa bila kazi kwani hamna abilia wa kuwauzia bidhaa zao.
 Ni kundi kubwa la madreva lilijitokeza kufanya maojiano na mwandishi wetu
 Dereva akitoa kile alichonacho moyoni (Bora kufa njaa kuliko kuwafanyia kazi wazabuni wa standi hii)
 Dereva akiongea kwa uchungu mkubwa  mara baada ya kupewa majibu ya kuumizwa na mzabuni wa standi  ya kuwa wanajiangisha bure hamna kitakachofanyika juu ya hilo watarudi tu (aalisema dreva mmoja)
Na Mwandishi Maalum Bukoba

MADERVA wa magari ya kusafirisha abilia mjini Bukoba wameitaka halmashauri ya manispaa hiyo kusikiliza matakwa yao ili waweze kusitisha mgomo wa kusafirisha abilia ambao ukiwa umedumu takilibani siku tatu
 :-
Wanashinikiza serikali kutimiza matakwa yao na kusema kuwa kiwango cha ela wanachotozwa kama ushuru wa standi ni kikubwa ukilinganisha na kiwango cha  standi haini vigezo maalum vya kuwa standi ya kulipia kiwango cha ushuru huo.


Inasemekana kuwa kwa siku gari moja aina ya haice,tax,pikipiki,mkokoteni  na hata gari binafsi linapoingia ndani ya stand  inaweza kulipa ushuru mpaka 4000/= kiasi ambacho ki kingi kwa maisha ya kaiwaida na ukilinganisha na athi ya standi yenyewe.

Walisema kuwa  wako tayari kufanya kazi na kukaa kwa mazungumzo na Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba kama alivyodai kuwa atakutana nao siku ya tarehe 01/09/2012.


Waliongeza kuwa mpaka siku yenyewe ya tarehe 01/09/2012 watakuwa tayari kuendelea kufanya kazi kama ungozi wa manispaa watatoa hamri kuwa kwa siku hizo tatu magari yote yasilipe ushuru ndani ya stendi au yasingie ndani ya stendi ila yaendelee kutoa huduma mtaani kwa kudaka abiria.

Matukio Mbalimbali


Baadhi ya viongozi wa LAVLAC wakiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa mashirika yaliyofadhili ufunguzi wa mkutano mkuu wa mwaka wa LAVLAC.




Mkurugenzi wa mipango na mikakati wa benki ya Posta Tanzania, Bernadethe Gogadi akiwasalimia wajumbe walioudhuria ufunguzi wa mkutano wa LAVLAC uliofanyika kwenye ukumbi wa hoteli ya Bukoba Coop. iliyoko katika manispaa ya Bukoba, mkutano huo unazishirikisha halmashauri za wilaya na manispaa zinazoko kwenye ukanda ziwa victoria 130 toka katika nchi za Uganda, Kenya na Tanzania.




Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Misenyi, William Katunzi (kushoto) na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Karagwe, Kashunju Runyogote (kulia).




Baadhi ya viongozi mkoani Kagera walioudhuria ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa LAVLAC kutoka kulia ni diwani wa viti maalumu, Mulungi Kichwabuta (CCM), mbunge wa viti maalumu CHADEMA Conchester Lwamlaza, na mwisho kushoto ni Diwani wa viti maalumu wa manispaa ya Bukoba CHADEMA, Mama Mkono.




Bango linaloonyesha wadhamini wa mkutano wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa LAVLAC ulioandaliwa na halmashauri ya manispaa ya Bukoba ambao ni pamoja na Benki ya posta Tanzania (TPB) na mradi wa uwekezaji (UTT).



Baadhi ya wajumbe walioudhuria mkutano wa LAVLAC.




Mkusanyiko wa waumini wa dhehebu la kiislamu wakiwa nje ya mahakama ya mkoa ya Kagera, walikusanyika kwa lengo la kusikiliza tuhuma zinazowakabili wenzao walikamatwa na jeshi la polisi kwa tuhuma ya kupinga kuhesabiwa



Baadhi ya wiaslamu wengine waliokutwa kwenye viwanja vya mahakama kuwatetea waislamu wenzao waliokamatwa kwa tuhuma ya kupinga zoezi la sensa ya watu na makazi.




Baadhi ya waislamu wengine.




Waislamu wa wengine waliokuwa miongoni mwa walioukutwa kwenye viwanja vya mahakama.




Peter Mushi, katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) akifungua mkutano wa uchaguzi wa jumuia ya wazazi ya chama hicho uliofanyika kwenye viwanja vya mtakatifu Francis.

Zoezi La Uwandikishaji Laendelea VIZURI Kaskazini "B"unguja.

Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini "B" Hamis Jabir Makame akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na Zoezi la Sensa linaloendelea katika Mikoa na Wilaya Nchini kote,ambapo katika Wilaya hio zoezi hilo linakwenda vizuri.
Karani wa Sensa akiwa katika kazi ya kuwaandika watu katika kitongoji cha Kiongwe Mkwambani Shehia ya Mafufuni Bumbwini ambapo  watu wa kijiji hicho awali waligoma kuandikisha kutokana na madai ya Elimu ya uwandikishaji kutokuwafikia vya kutosha.
                            
                                 
                                      PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.

Maisha Yanaendelea


Polisi Vs Chadema Iringa







gari za polisi wakiwa tayari kwa lolote baada ya mkutano wa chadema kuahirishwa leo jioni na baadhi ya picha za chiku abwao akiongea na wananchi na nyingine akiongea na kiongozi wa polisi. picha na denis mlowe

Magazeti Magazeti












Thursday, August 23, 2012

Taarifa Kwa Umma



                      JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
                    WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

                          TAARIFA KWA UMMA
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Khamis Sued Kagasheki amebadili taratibu za kuwapata wajumbe wa Bodi mbali mbali zilozoko chini ya Wizara. Kuanzia sasa Wajumbe wa Bodi hizo watapatikana kwa njia ya ushindani badala ya kuteuliwa moja kwa moja na Waziri.
Kwa sasa kuna Bodi nane (8) ambazo muda wake umeisha au unakaribia kuisha.Bodi hizo ni za za Taasisis/Mashirika yafuatayo;-
I. Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro
II. Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI)
III. Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI)
IV. Makumbusho ya Taifa
V. Chuo cha Mafunzo na Usimamizi wa Wanyamapori (MWEKA)
VI. Chuo cha Mafunzo ya Wanyamapori Pasiansi
VII. Wakala wa Mbegu za Miti (TTSA)
VIII. Bodi ya Leseni za Utalii (TTLB)
Watanzania wenye sifa za kuwa Wajumbe wa Bodi hizo wanatakiwa kupeleka maombi kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii.
Maelezo zaidi ya namna ya kupeka maombi yataweka kwenye magazeti na tovuti ya Wizara, www.mnrt.go.tz 

NB: BOFYA HAPA KAMA UNAHITAJI KUOMBA NAFAZI ZA UJUMBE WA BODI http://www.mnrt.go.tz
Reactions::

Mkurungenzi Wa Mashtaka (DPP)Afungua Semina Ya Wapelelezi.Polisi,Mahakimu,Na Majaji Jijini Dar es salaam

Mkurungenzi wa mashtaka (DPP)Dk.Ellezer Feleshi (kulia) akiongea na waandishi wa habari baada ya kufungua semina ya wapelelezi.polisi,mahakimu,na majaji,Dr Ellezer alisema mafunzo hayo yanahusu mbinu za kisasa za kukabiliana na uhalifu wa utakatishaji wa fedha,biashara madawa ya kulevya,utaifishaji wa mali zilizopatikana kwa njia ya haramu na masuala ya ugaidi,semina hiyo ilifanyika katika hotel ya Kunduchi Beach nje kidogo ya jiji la Dar es salaam jana.

Dkt. Mwakyembe Amsimamisha Kazi Mkurugenzi Mkuu wa Bandari



Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harisson Mwakyembe amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari-TPA-Ndugu Ephrahim Mgawe pamoja na wasaidizi wake wawili ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili.

Wengine waliosimamishwa ni Meneja wa Mafuta ya Ndege Kurasini, Meneja wa JET na Meneja wa Oil Terminal kutokana na tuhuma za kupotea kwa mafuta na kuidanganya serikali kuhusu mafuta masafi na machafu.

Kutokana na kuwasimamisha kazi Wakurugenzi hao Dkt. Harisson Mwakyembe amemteua Injinia Madeni Kipange kukaimu nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA.

Kufuatia tuhuma hizo zinazofanywa Bandarini Dkt. Mwakyembe ameunda Tume wa ya watu saba kufanya uchunguzi kwa wiki mbili na kumpelekea taarifa ofisini kwake ili kubaini ukweli wa tuhuma hizo zikiwemo za wizi.

Pia ameagiaza kufikia Septemba Mosi mwaka huu malipo yote yafanyike benki ili kuondoa rushwa na wizi unaofanyika ndani ya Mamlaka hiyo.

Waziri Mwakyembe anachukua hatua hizo kutokana na wwadao wengi sasa hawaitumii Bandari ya Dar es salaam kupitisha mizigo yao kutokana na kutokuwa na imani na watumishi wake hatua inayoifanya serikali kukosa mapato.

Pia ameagiza kusimamishwa mara moja kwa Kampuni ya Singilimo ambayo inajihusisha na kazi ya kubeba mafuta machafu na badala yake itafutwe Kampuni nyingine.

U.W.T Bukoba Wafanya Mkutano Wa Uchaguzi



Mkuu wa mkoa wa Kagera Bi Ziporah Pangani, akiongea na wajumbe wa jumuia ya wanawake (UWT) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)wakati wa mkutano mkuu wa jumuia hiyo wa kuwachagua viongozi wapya uliofanyika kwenye ukumbi wa amtakatifu Francis, ulioko katika manispaa ya Bukoba.




Mwenyekiti wa UWT wa mkoa wa Kagera ambaye amestaafu nafasi hiyo akitoa hotuba wakati wa mkutano mkuu wa jumuia hiyo uliofanyika kwenye ukumbi wa mtakatifu Francis



Mkuu wa wilaya ya Bukoba Bi. Ziporah Pangani na mkuu wa mwenyekiti wa jumuia ya wazazi wa mkoa wa Kagera walikuwa miongoni mwa walioudhuria mkutano mkuu wa jumuia hiyo.




Hali hii inaonyesha jinsi gani wanawake wanavyoithamini CCM.




Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa wazazi wa CCM wa wilaya ya Bukoba.




Makada wa CCM.



Mama stella (kulia) na Mama Kyaishozi.




Baadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu wa jumuia ya wanawake ya wilaya ya Bukoba ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakifurahia jambo nje ya ukumbi wa mtakatifu Francis uliko katika manispaa ya Bukoba wakijadili jambo kabla ya kufanyika mkutano mkuu wa chama hicho wa kuwachagua viongozi wapya wa jumuia hiyo.




Mulungi Kichwabuta, diwani wa viti maalumu wa chama cha mapinduzi (CCM) akiwa na baadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu wa jumuia ya wanawake wa wilaya ya bukoba mjini, walioudhuria mkutano mkuu wa jumuia hiyo wa kiwachagua viongozi wapya.




Baadhi ya waandishi wa habari mkoani Kagera wanaohudhuria mafunzo ya uchokonozi yanayotolewa na mwandishi mkongwe Fili Karashani wakiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari toka mkoani Singida.