Sunday, June 17, 2012

Wazee Washauriwa Kutojihusisha Na Siasa

Na Mwandishi Wetu 
Bukoba
WAZEE wamashauriwa kutojihusisha na masuala ya siasa na badala yake watafute mbinu mbadala ya kujikwamua kimaisha ili kukabiliana na hari ya ugumu wa maisha ili kuhepuka na suala la kuwa ombaomba katika maisha yao ya kila siku.

Ushauri huo umetolewa na afisa maendeleo ya Jamii Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera Mrisho Issa kwaniaba ya Mkurugenzi wa Manispaa hiyo wakati wa kufungua tawi la Saidia Jamii ya wazee Kagera(SAJAWAKA)  tawi la kata ya Kahororo katika manispaa hiyo ambalo limeanzishwa kwa ajili ya kusaidia wazee.

Alisema kuwa wazee wanapofungua vikundi kama cha (SAJAWAKA) wajue malengo yake na wala wasijihusishe na masuala ya siasa kwani wakati  wa kushabikia  mambo ya siasa uwe nje ya vikundi ambavyo vinatambulika kisheria.

Aliongeza kuwa vipo vikundi vingi vinaanzishwa lakini malengo ambayo wanakuwa wamakusudia luyafanya hawayafanyi na badala yake wanajikuta wameanza kushabikia mambo ya kisiasa nalengowanalokuwa wamekusudia kulifanya halifanyiki.

Katika hatua nyingine alisema kuwa pamoja na kufungua tawi la wazee bado kuna changamoto kwa wazee kutopata huduma ya afya bure hasa wale wanao anzia umri wa miaka 60 na kuendelea kama sera ya wizara husika inavyosema.

Aliongeza kuwa Hospitari nyingi bado jambo hilo hawalitilii maanani na kusababisha usumbufu kwa wazee ambao uwezo wao ni mdogo na kujikuta hawapati huduma ya matibabu bure .

Nae Mwenyekiti wa tawi la Saidia jamii ya wazee Kagera tawi la kata kahororo Silivanu Muyoza alisema kuwa kikundi hicho kina jumla ya wazee 104 na wanatarajia wapewe matibabu bila kudaiwa changizo za tiba kama sra ya wizara ya afya inavyosema na wamepatiwa vitambulisho maalumu vya Chama cha wazeeTanzania (CHAWATA).

Aliongeza kuwa wazee wanatarajia pia kutolipa kodi za viwanja na nyumba zao zisizozalisha biashara kama mwanzo ambapo waliwa wakilipa kodi hizo huku wengine wakiwa na uwezao mdogo.

Aidha alisema kuwa kikundi hicho hakikuanzishwa kwa lengo la siasa na badala yake ni kwa ajili ya kusaidia wazee kimaendelea kwa kubuni mirani mbalimbali ya kuwasaidia katika umri wao wa uzeeni.

Mwisho

No comments:

Post a Comment