Wednesday, June 27, 2012

Polisi Kagera Yatoa Taarifa Za Matukio Mbalimbali


Haya ndio mafanikio ya operation maalumu iliyoendeshwa na jeshi la polisi mkoani Kagera kuanzia juni 8, mwaka huu.




Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera Peter Kalangi akionyesha misokoto ya bangi iliyokamatwa na jeshi la polisi, pembeni yake ni mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai mkoani humo Peter Matagi.




Sehemu ya vifaa vya maabara mali ya shule ya sekondari ya Nyakato iliyoko mkoani Kagera ambavyo jeshi la polisi lilivikamatwa.




JESHI la polisi mkoani Kagera linamshikilia Peter Mabara (28) msukuma mwenyeji wa Kahama kwa tuhuma ya kusababisha kifo mwanafunzi wa kidato cha pili wa shule ya sekondari ya Kaagya iliyoko tarafa ya Bukoba.

Akisimulia tukio hilo mbele ya waandishi wa habari ofisini kwake mbele ya waandishi wa habari jana kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera Peter Kalangi alisema Mabara ambaye ni mchunga Ng’ombe anatuhumiwa kumuua Advea Makanyaga (16) juni 24 mwaka huu.

Kalangi aliwaambia waandishi habari kuwa Marehemu kabla ya kifo chake alitumwa na bibi yake Mariselina Bigira (53) mhaya mkazi wa mshozi kupeleka chakula porini kwa mtuhumiwa wa mahuaji ambaye alikuwa akichunga Ng’ombe wanamilikiwa na bibi yake huyo.

Alisema marehemu huyo alipoenda porini hakurudi tena hadi mwili wake ulioonekana umetelekezwa porini juni 25, mwaka huu, Kalangi alisema mwili wa marehemu huyo ulikutwa umwekewa jiwe kubwa kichwani huku ukiwa na majeraha mbalimbali kwenye mwili na shingo ya marehemu huyo ikiwa inalegea kama iliyonyongwa.

Kamanda huyo alisema jeshi la polisi lilipopata taatifa hizo lilikwenda kwenye tukio na kuanza kufanya kazi ya upelelezi, alisema upelelezi wa awali wa jeshi hilo ulionyesha uhusiano wa kifo mwanafunzi huyo na mchunga ng’ombe.

Aliendelea kusema kuwa kilichodhihirisha uhusiano wa kifo cha marehemu na mchunga ng’ombe huyo ni hatua yake ya kutaka kutoroka, alisema mchunga ng’ombe alinaswa na jeshi la polisi eneo la standi kuu mabasi Bukoba akitaka kutoroka kwenda kwao kahama.

Kalangi alisema taarifa nyingine za awali za kiupelelezi zinaonyesha kuwa mchunga ng’ombe huyo alikuwa akimtaka mapenzi mwanafunzi huyo kwa kipindi kirefu na mwanafunzi huyo alikuwa akimkatalia.

Aidha, kamanda huyo wa jeshi la polisi alieleza mafanikio ya operation iliyoiendesha ya kupambana na uharifu mkoani Kagera kuanzia juni 8, mwaka huu, alisema jeshi hilo lilifanikiwa kukamata shamba la bangi hekta 1 na magunia 2 ya bangi wilayani Biharamulo lililokuwa linamilikiwa Alfred Philip aliyetoroka.

Alisema pia jeshi hilo lilifanikiwa misokoto ya ya bangi ikiwa kwenye gunia, mirungi gunia moja na gramu 400 ambapo watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani, aliendelea kusema katika wilaya za muleba na karagwe jeshi hilo pia lilikamata magunia matatu ya bangi.

Alimaliza kwa kusema jeshi la polisi litaendelea na misako yake ya kupambana na wale wote wanaojihusisha na vitendo vya uharifu,”hii sio nguvu ya soko nitawashughulikia wote wenye nia mbaya ndani ya jamii, ndugu wananchi nawaombeni mniunge mkono” alisema Kalangi.




Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akisalimiana na Mbunge wa Lindi Mjini , Salum Baluany kwnye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma Juni 25,2012. Kulia ni Mtoto wa Waziri Mkuu, George Bush. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)




Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua zabibu wakati alipotembelea shamba la Tendaji Agro lililopo katika kijiji cha Chikopelo wilayani Bahi, Dodoma juni 24, 2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment