Thursday, June 21, 2012

Bei Ya Kahawa Mkoani Kagera Yashuka

Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Kagera John Binushu anaye andika akijadiri jambo na Mrajisi wa Vyama Vya Ushirika Mkoani Kagera Rwenkiko Shorosi


 Na Mwandishi Wetu Bukoba
 
CHAMA kikuu cha ushirika mkoani Kagera(KCU 1990 LTD)kimefikia maamuzi ya kushusha bei ya Kahawa,kwa kile kilichodaiwa kusababishwa na kushuka kwa bei hiyo katika soko la Dunia.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa chama hicho John Binunshu,kushuka kwa bei hiyo ni kutokana na bei ya mnadani kuporomoka kwa siku za hivi karibuni hivyo kulazimu KCU kubadirisha bei ya manunuzi tofauti kama ilivyokuwa hapo awali.

Binunshu alisema kuwa hata hivyo pamoja na kushuka bei hiyo,wakulima wa Kahawa mkoani hapa wasiwe na wasiwasi juu ya taarifa hizi kwani wataendelea kupatiwa taarifa za bei kadili hali ya soko itakavyokuwa inabadirika.

Katika taarifa ya Meneja mkuu wa KCU Vedasto Ngaiza,na nakusambazwa kwa mameneja wote wa  vyama vyamsingi vipatavyo 129 ambavyo vinaendelea na ununuzi wa Kahawa kwa msimu huu ambao umefunguliwa rasmi mwezi Mei mwaka huu,bei ya kahawa imeteremka kutoka shilingi 1350/=hadi kufikia shilingi 1100/=kwa Kahawa aina ya robusta maganda,huku robusta safi itakuwa ikinunuliwa kwa shilingi 2,200/= kwa kilo.


Aidha,Ngaiza alibainisha kuwa Kahawa nyingine aina ya Arabika maganda imeshuka kutoka shilingi 1550/=na kufikia shilingi 1300/=huku safi ikinunuliwa shilingi 2600/=.

Hata hivyo,Ngaiza amesisitiza kuwa wakulima wa zao hili wanapaswa kupokea mabadiliko ya bei hiyo,ila endapo bei itaongezeka mnadani uongozi wa KCU hautachelewa kurekebisha bei hiyo kwa mkulima.

Awali mabadiriko ya bei hizi,yalionekana kuanza kuleta wasiwasi juu kwa wakulima huku baadhi yao wakihushutumu uongozi wa KCU umeamua kutelemsha bei mara baada ya kubaini kuwepo wingi za kahawa kwa wakulima.

MWISHO

No comments:

Post a Comment