Monday, June 11, 2012

Polisi Kagera Yauwa Jambazi Na Kukamata Buduki Tatu Na Mabomu

Na Mwandishi Wetu
Kagera

JESHI la polisi Mkoani Kagera limefanikiwa kumuua jamabazi katika majibizano ya risasi na kufanikiwa kukamata  bunduki tatu risasi 246,mabomu ya kurushwa kwa mkono matatu na sare pea mbili ambazo zionafanana na kabisa na za jeshi la wananchi wa Tanzania.

Akiongea na wandishi wa habari ofisini kwake kamanda wa polisi Mkoani humo Philp Kalangi amesema tukio hilo lilitokea tarehe
9 Juni majira ya saa 10 alfajiri katikaeneo la Mavota-Tulawaka Wilaya ya Biharamulo Mkoani Kagera Mtu anayesadikiwa kuwa ni jambazi ambaye hafahamiki jina wala makazi yake aliuawa baada ya kupigwa risasi na askari polisi katika shambulizi.

Kamanda Kalangi, alisema tukio hilo lilitokea baada ya msiri kufichua mpango uliokuwa umepangwa na majambazi ambayo yalikuwa na lengo la kwenda kuvamia Mgodi wa Barrick Tulawaka ulioko Biharamulo Mkoani humo,jeshi la polisi baada ya kupata taarifa  hizo mkuu wa upelelezi mkoa wa Kagera SSP,Peter Matage aliandaa mtego kupitia njia ambayo ja,bazi hilo lingetumia.

Alisema kutokana na taarifa za msiri jambazo huyo ndiye alikuwa kiongozi na alibeba silaha  zote mwenyewe  na tayari alikuwa amewatanguliza wenzake mbele ambao wangekutana eneo la tukio.

Kamanda alisema katika shambulizi hilo la kushitukiza na kurushiano risasi kati ya jambazi huyo na askari na hatimaye kuuawa kwa jambazi hilo  na kukutwa na bunduki tatu ambazo mbili ni AK  47 ,SMG moja,riasi 246,mabomu ya kurushwa kwa mkono matatu,sare za jeshi la wananchi pea mbili na buti pea moja na makoti mawili ya mvua ambayo yalikuwa yamefungiwa bunduki mbili,na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali teule ya Biharamulo.


Kamanda Kalangi alisema  katika tukio jingine jeshi hilo  linawashikiliwa watuhumiwa wanne aliokuwa wamepanga njama za kutaka kumuua ( ALBINO )aishie Wilayani Missenyi Mkoani humo.

Amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Gaston Galela( 50 ),ambaye ni Mnyarwanda,alikamatwa akiwa Bwanga mkoani Geita kwa mganga wa kienyeji, Njenwa Charles ( 30 )msukuma  na mkazi wa Mutukula Byamungu Felician (  53 )mkazi wa Mutukula na  Masanja Mabula ( 40 )mkazi wa Mutukula.

Alisema wamefanikiwa kuwatia mikoni watuhumiwa hao kufuatia taarifa iliyotolewa kwa jeshi hilo kupitia kwa mpelelezi wa makosa ya jinai mkoani humo Petera Matage aliyeanda mgego wa kuwanasa na kufanikiwa.

Wakati huohuo jeshi hilo Mkoani Kagera wamefanikiwa kumkamata Chamilion Kamugisha miaka ( 20 )mkazi wa Hamgembe Manispaa ya Bukoba Mkoani humo Juni 5 majira ya saa 10.00 asubuhi eneo la Mutukula Wilaya Ya Missenyi akiwa na noti bandia  US Dollar 1000,wakati akiwa katika harakati za kubadilisha katika fedha za kitanzania.

Kamanda huyo wa polisi Mkoani hapa ambaye ndiyo mara yake ya kwanza kufanya kazi mkaoni Kagera amewataka wanachiwa mkoa huo kuwa na usgirikiano na jeshi la polis sambamba na kuachana na mila potofu huku akisema mali azipatikani kwa imani za ushirikina ni juhudi na maarifa.

MWISHO

No comments:

Post a Comment