Tuesday, June 12, 2012

RPC Kagera Akionyesha Nguo Za JWTZ Walizokamata Wakati Wa Mapambano Kati Ya Polisi Na Majambazi


Huyu ndiye kamanda mpya wa jeshi la polisi mkoani Kagera aliyemrithi Henry Salewi aliyestaafu, anaonekana ameshika bunduki sare za jeshi la wananchi ambazo majambazi yalikuwa yakizitumia kufanya uharifu.




Mkuu wa upelelezi mkoani Kagera Peter Matagi akionyesha dola feki 1,000 ambazo jeshi la polisi lilizinasa kufutia msako mkali unaofanywa na jeshi hilo mkoani humo wa kuthibiti uharifu.




Baadhi ya silaha ambazo jeshi la polisi lilizikamata zilizokuwa zikitumiwa na majmbazi kufanya uharifu mkoani Kagera



 
NARUDIA TENA HII STORI
 
JESHI la polisi limefanikiwa kuliua jambazi sugu lililokuwa linamiliki silaha tatu za kivita zilizokuwa zinatumika kutekeleza vitendo vya uharifu kwenye maeneo mbalimbali yaliyoko mkoani Kagera vikiwemo vya utekaji wa magari na wizi na unyanganyi.

Jambazi hilo ambalo jina lake halikuwe kutambuliwa limeuwawa jana majira ya saa 4.30 halfajiri na kikosi maalumu cha upelelezi kilichooongozwa na mkuu wa upelelezi wa mkoa wa Kagera Peter Matagi.


Kwa mijibu wa kamanda wa jeshi la polsi mkoani Kagera Philip Kalangi ni kwamba jeshi hilo lilifanikiwa kulinasa jambazi hilo na hatimaye kuliua wakati lilipokuwa liko kwenye harakati za kuvamia mgodi unamilikiwa na kampuni ya barrick wa Tulawaka uliko wilayani Biharamulo.


Kalangi ambaye ni kamanda mpya wa jeshi la polisi mkoani Kagera aliwaambia waandishi wa habari kuwa jeshi la polisi kabla ya kukabiliana na jambazi hilo lilipata taarifa za siri toka kwa wasiri wake jambo lililolisaidia jeshi hilo kuweka mtego ulionasa jambazi hilo.


Alisema jambazi hilo wakati likiwa katika harakati za kutekeleza uharifu kwenye mgodi wa Tulawaka huku likiwa na wenzake waliofanikiwa kukimbia lilishtukia mtego ulikuwa umewekwa na jeshi la polisi hivyo likalazimika kuanza kumimina risasi ovyo.


Kamanda huo alisema jeshi la polisi baada ya kuona hivyo lilijibu mapigo yaliyofanikisha kuuawa kwa jambazi huyo huku majambazi wenzake wakikimbilia kusikojilikana, alisema katika tukio hilo jeshi hilo lilifanikiwa kupata silaha mbalimbali, risasi na mabomu ya kutupa kwa mkono.


Alizitaka silaha ambazo jeshi la polsi lilifanikiwa kuzikamata katika tukio hilo kuwa ni pamoja na bunduki moja ya AK 47, Bunduki 2 aina ya SMG, risasi 246, magazini 7 na mabomu 3 ya kurusha kwa mkono.


Kalangi alisema jambazi liliouwawa na askari hao mwili wake umehifadhiwa kwenye hospitali teule ya wilaya ya Biharamulo, alisema jeshi hilo liko katika msako mkali wa kuwanasa majambazi yaliyokimbia wakati wa tukio hilo.


Alipongeza askari walioshiriki katika operationi hiyo maalumu, pia aliwashukuru wananchi waliotoa taarifa za siri zilizilisaidia jeshi la polisi kuyanasa majambazi hayo, aliwaomba wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili liweze kutimiza adhima yake ya kuthibiti uharifu mkoani Kagera.

No comments:

Post a Comment