Wednesday, June 27, 2012

Taarifa Kutoka Kampuni Ya Bia Tanzania (TBL)
            TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

                           Toleo la Leo 

MASHINDANO YA NGOMA ZA ASILI YA BALIMI EXTRA LAGER 2012 KUTIMUA VUMBI KUANZIA JUNI 30.

Dar Es Salaam, June 25th 2012:
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia bia yake ya Balimi Extra Lager, leo imezindua rasmi mashindano ya ngoma za asili ya Balimi Extra Lager kwa mwaka 2012. Mashindano haya ambayo yametokea kupendwa sana na wakazi wa kanda ya ziwa yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi katika mikoa mbali mbali ya kanda ya ziwa kuanzia Juni 30.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo Jijini Dar es Salaam, meneja wa Bia ya Balimi Extra Lager Bi. Edith Bebwa alisema; Bia ya Balimi Extra Lager imekuwa ikiendesha mashindano haya maarufu kama “Mashindano ya Ngoma za Asili ya Balimi Extra Lager” kwa zaidi ya miaka saba sasa , na kwa kweli napenda kusema kuwa ni mashindano yaliyotokea kupendwa sana katika kanda yetu hii ya ziwa,
Lengo kuu la kudhamini mashindano haya ni kushirikiana na wakazi wa kanda ya ziwa katika kuenzi na kulinda tamaduni za kanda alisema Bi Edith .
Kwa mwaka huu wa 2012, mashindano yataanza rasmi tarehe 30 Juni katika ngazi za mikoa na kumalizika tarehe 21 Julai. Tutaanza na mkoa wa Mwanza ukifuatiwa na mikoa ya Mara, Kagera, Shinyanga na Tabora, katika mpangilio ufuatao.

Tarehe Mkoa Viwanja
30/06/2012 KAGERA
Kaitaba
07/07/2012 MWANZA Ccm Kirumba
14/07/2012
TABORA Chipukizi
21/07/2012
SHINYANGA Shycom
21/07/2012
MUSOMA Bwalo la Magereza
28/07/2012.
FINALS MWANZA Ccm Kirumba
Akielezea juu ya zawadi za mwaka huu, bi. Edith Bebwa alisema; kama ilivyo ada ya Bia ya Balimi, kila mwaka tumekuwa tukiongeza zawadi ili kuongeza chachu ya ushindani na kuleta tija kwa washindani. Kwa mwaka huu tumeongeza zawadi kwa takribani asilimia 20 ukilinganisha na mwaka jana. Hii yote inaonesha jinsi gani bia ya Balimi inatambua, inajali na kuthamini utamaduni wa kanda yetu. Zawadi kwa washindi ni kama ifuatavyo;
Ngazi ya mkoa Finali
Mshindi wa kwanza 600,000 1,100,000
Mshindi wa pili 500,000 850,000
Mshindi wa tatu 400,000 600,000
Mshindi wa nne 300,000 500,000
Mshindi wa tano hadi wa kumi kila kikundi 150,000 250,000
Pamoja na zawadi hizi nono, pia Balimi Extra Lager itaendelea kutoa huduma muhimu kwa vikundi shiriki kama vile chakula na malazi. Tunaamini kabisa mambo yote haya yataongeza hamasa na msisimko katika mshindano ya mwaka huu. Na kauli mbiu yetu kwa mwaka 2012 “Balimi Extra Lager, twajivunia utamaduni wetu”.

Akizungumzia maandalizi ya fainali hizo, Meneja Masoko wa Tbl Fimbo Buttalah alisema; Maandalizi yote kwa upande wetu sisi wadhamini yameshakamilika, hivyo niwaombe tu washiriki wote ambao nimepata taarifa kuwa wamekuwa mazoezini kwa muda sasa, waendelee na mazoezi ili kuonesha uwezo wa juu utakaoleta ushindani na kutoa burudani yenye kiwango cha juu.

Kwa niaba ya bia ya Balimi Extra Lager, tunapenda kuwakaribisha watu wote kuhudhuria mashindano haya ambayo tarehe na mahali yatakapofanyikia zitakuwa zikitangazwa redioni ili waweze kushuhudia burudani hii na kuuenzi utamaduni wetu. Pia wananchi wasisahau kuwa katika burudani hizi pia wataburudika na Bia yao waipendayo ya Balimi Extra lager baridi, na kushinda zawadi mbali mbali katika promosheni za Balimi zitakazoambatana na Mashindano haya ya Ngoma za asili ya Balimi Extra Lager.
Kwa Maelezo zaidi wasiliana na:
Edith Bebwa, Brand Manager, +255767266410, edith.bebwa@tz.sabmiller.com
Fimbo Butallah, Marketing Manager, +255767266567, fimbo.butallah@tz.sabmiller.com
Editha Mushi, Communications & Media Manager, +255767266420, editha.mushi@tz.sabmiller.com

Kuhusu TBL
Tanzania Breweries Limited (TBL) inatengeneza, kuuza na kusambaza bia, vinywaji vyenye ladha ya matunda vilivyo na kilevi na vinywaji visivyo na kilevi hapa Tanzania. TBL pia ndiyo kampuni mama ya Tanzania Distilleries Limited pamoja na kampuni shiriki ya Mountainside Farms Limited.

Bia zinazotengenezwa na kampuni ya TBL ni pamoja na Safari Lager, Kilimanjaro Premium Lager, Ndovu Special Malt, Castle Lager, Vinywaji vingine vinavyotengenezwa na kundi la makampuni ya TBL ni Konyagi Gin, Amarula Cream, Redd’s Premium Cold na Grand Malt.

Kundi la makampuni ya TBL limeorodheshwa kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam, limeajiri watu wapatao 1,300 na linawakilishwa nchi nzima na viwanda vinne vya bia, kiwanda kimoja cha kutoneshea, kimoja cha kutengenezea kimea pamoja na bohari nane za kusambazia bia.

Kuhusu SABMiller
SABMiller plc moja kati ya makampuni makubwa ya bia duniani ikiwa na mikataba ya kutengeneza na kusambaza bia kwenye nchi zaidi ya 60 katika mabara matano. Bia zake ni pamoja na zile za kimataifa kama Miller Genuine Draft, Peroni Nastro Azzurro na Pilsner Urquell vilevile na bia nyingine zinazoongoza kwenye masoko ya ndani ya nchi mbalimbali. Nje ya Marekani, SABMiller ni moja ya kati ya makampuni makubwa yanayotengeneza vinywaji vya Coca-Cola duniani. Hivi karibuni SABMiller plc ilinunua kampuni ya bia ya Foster’s pamoja na shughuli zake za uzalishaji nchini India.SABMiller imeorodheshwa kwenye masoko ya hisa ya London na Johannesburg.

No comments:

Post a Comment