Na Mwandisi wetu
Bukoba
VIJANA mkoani Kagera wameshauriwa kujishugulisha na kazi mbalimbali za kuwaletea maendeleo na kutakiwa kuachana na matumizi ya dawa za kulevya ili kuweza kuwasaidia kutatua matatizo ambayo yanawakabili kimaisha ili kukabiliana na tatizo kubwa la ajila kwa vijana.
Ushauri huo umetolewa na Godfrey Inocenti ambaye ni mwenyekiti wa shirika la Maejor Allienge education center (MAEC) la mkoani Kagera linalojishugulisha na kupambana na dawa za kulevya hasa kwa vijana wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo ikiwemo utawala bora wa asasi na usimamizi wa fedha kwa wanachama wa shirika hilo.
Alisema kuwa kwa hivi sasa nguvu kazi nyingi ya vijana imepotea kutokana na kujihusisha na madawa ya kulevya ikiwemo uvutaji wa bangi unywaji wa pombe uliokithiri jambo ambalo limepelekea vijana kukumbwa na wimbi la umasikini.
Inocenti aliongeza kuwa shirika hili la MAEC linajitahidi kwa kasi kubwa kuhakikisha linawashawishi vijana kutambua athari za utumiaji wa madawa ya kulevya na kuwataka wapinge utumiaji huo na kujihusisha na shughuliza uzalishaji mali.
Kwa upande wake mratibu wa mafunzo hayo Edwini Sebastiani alisema kuwa jumla ya wanachama 45 wamenufaika kupata mafunzo ambayo yamefadiliwa na shirika la the foundation for civil society ambao wao ndio watakuwa mabarozi wazuri kwa vijana wengine mkoani Kagera na kuomgeza kuwa mbali na kutoa elimu watapata uongozi bora,usimamizi wa fedha na uandishi bora wa miradi.
Aliongeza kuwa shirika hilo lililo anzishwa mwaka 2007 mkoani Kagera limewanufaisha jumla ya vijana 1250 kwa kuwapa elimu bora na kuwanusuru na utumiaji wa dawa za kulevya na wao kuendelea kuwashauri vijana wengine.
No comments:
Post a Comment