Thursday, September 20, 2012

Mkutano Mkuu Wa Baraza La Usalama Barabarani Wafanyika Mkoani Iringa Leo.

Baadhi ya Wajumbe wa mkutano Mkuu wa Baraza la usalamaBarabarani mkoani  Iringa wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa mapema leo ndani ya ukumbi wa chuo cha RUCO.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani nchini,Mohamed Mpinga akizungumza mambo
mbalimbali mapema leo mchana kwenye mkutano Mkuu wa Baraza la usalama Barabarani mkoani  Iringa uliofanyika ndani ya ukumbi wa chuo kikuu cha Ruaha (RUCO),ambapo pia mada mbalimbali zilijadiliwa ikiwemo  hali ya usalama barabarani nchini,Sera  ya Taifa
ya usalama barabarani,Taarifa ya ukaguzi wa utendaji  wa kikosi cha usalama barabarani katika kusimamia sheria na ukomo wa  mwendokasi wa magari,Rushwa na Miundombinu ya uadirifu na mengineyo.Mkutano huo umefanyika wakati wiki ya usalama barabara ikielekea ukingoni.
Sehemu ya Takwimu za ajali barabarani.

No comments:

Post a Comment