Thursday, September 13, 2012

JK- Katika Ziara Rasmi Nchini Kenya

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwa katika hafla ya kutoa heshima zao na kuweka mashada ya maua kwenye Kaburi la Mwanzilishi wa Taifa la Kenya, Hayati Jomo Kenyatta jijini Nairobi Septemba 12, 2012 akiwa katika Ziara Rasmi ya Kiserikali (State Visit) ya siku tatu ambayo ni ziara yake ya kwanza rasmi nchini humo ingawa amefanya ziara kadhaa za kikazi nchini Kenya
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alipotembelea na kuweka jiwe la msingi katika jengo jipya la kutengeneza maziwa ya unga katika  Kiwanda cha Maziwa cha Brookside Diary kwenye Barabara ya Thika nje kidogo ya jiji la Nairobi. (n5 - Rais Kikwete akiangalia ng'ombe wanaofugwa kisasa katika shamba la kiwanda hicho, n6- Rais Kikwete akiangalia kondoo  wanaofugwa kisasa katika shamba la kiwanda hicho, n7- Rais Kikwete akiangalia mchoro wa ujenzi wa jengo la kutengeneza maziwa ya unga wa  kiwanda hicho. Anayemuelekeza ni Mwenyekiti wa kampuni ya Brookside Diary Bw. Muhoho Kenyatta, n8- Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiweka jiwe la msingi katika jengo jipya la kutengeneza maziwa ya unga katika  Kiwanda cha Maziwa cha Brookside Diary kwenye Barabara ya Thika nje kidogo ya jiji la Nairobi. Kushoto ni Mwenyekiti wa kampuni ya Brookside Diary Bw. Muhoho 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete  akiwa katika picha ya pamoja na wenyeji wake baada ya  kutembelea Kituo cha Magonjwa ya Moyo na Kansa kwenye Hospitali ya Chuo Kikuu cha Aga Khan jijini Nairobi Septemba 12, 2012 akiwa katika Ziara Rasmi ya Kiserikali (State Visit) ya siku tatu ambayo  ni ziara yake ya kwanza rasmi nchini humo ingawa amefanya ziara kadhaa za kikazi nchini Kenya.

       

                                     PICHA NA IKULU

No comments:

Post a Comment