Tuesday, September 11, 2012

Picha Mbali Mbali


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kufungua rasmi Chuo cha UIinzi (National Defence College) leo Septemba 10, 2012 Kunduchi jijini Dar es salaam. Kulia kwake ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange na kushoto kwake ni Mkuu wa Chuo hicho, Meja Jenerali Charles Makalala na kushoto kabisa ni aBalozi wa China nchini Tanzania Mhe. Lu Younqing.



Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka sahihi makubaliano yaliyofikiwa na Wakuu wenzake wa Nchi na Serikali za Ukanda wa Maziwa Makuu baada ya mkutano wao uliofanyika Septemba 8, 2012 katika Hoteli ya Speke Resort Munyonyo mjini Kampala, Uganda. Picha na Ikulu




Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na wazee wakati alipohutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Halmashauri ya wilaya mjini Kahama Septemba 8,2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)




Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu (kulia) akisalimiana na Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Buzwagi wilayani Kahama kwa ziara ya siku moja wilayani huomo, Septemba 8, 2012. Kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum, Azza Hilal na watatu kulia ni mbunge wa Kahama, James Lembeli




Wasanii wa Khama wakicheza ngoma ya Waswezi wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Buzwagi, Kahama kwa ziara ya siku moja Septemba 8, 2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)




Hii ndio hifadhi iliyoko katika kisiwa cha Rubondo, angalia tembo wanaopatikana ndani ya kisiwa hiki.




Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda katika hoteli ya Speke Resort Munyonyo jijini Kampala leo Septemba 7, 2012. Rais Kikwete amewasili nchini Uganda leo kuhudhuria mkutano wa viongozi wa nchi za maziwa makuu.




Mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani ya mkoa wa Kagera Winston Kabantega akiongea na waendesha pikipiki zinazofanya kazi ya kusafirisha abiria, Kabantega ni mdau mkubwa wa jeshi la polisi, amejitoa muanga hasa katika zoezi zima la kuwahamasisha waendesha pikipiki wahudhurie mafunzo ya udereva.




Baadhi ya waendesha pikipiki wengine wakisiliza kwa makini maelekezo yaliyokuwa yakitolewa na viongozi.




Baadhi ya waendesha pikipiki wakimsikiliza Mkonda.




Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani, William Mkonda akiongea na waendesha pikipiki zinazofanya kazi ya kubeba abiria katika halmashauri ya manispaa ya Bukoba.




Baadhi ya pikipiki zinazofanya biashara mkoani Kagera.




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange salamu za rambirambi kuomboleza kifo cha Luteni Kanali (mst) Adam Hussein Mwandu Makwaia (kwenye picha juu), aliyekuwa Mpambe wa Rais wa kwanza wa Tanzania, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na Rais Ali Hassan Mwinyi.

Katika salamu zake, Rais Kikwete amemwambia Jenerali Mwamunyange: “Nimepokea kwa majonzi na masikitiko taarifa za kifo cha Luteni Kanali Makwaia ambaye nimejulishwa kuwa alipoteza maisha Jumanne, Septemba 4, mwaka huu, 2012, katika Hospitali ya Jeshi ya Lugalo mjini Dar es Salaam.” “Katika miaka yote ya utumishi wa Jeshi na utumishi wa umma, Luteni Kanali Makwaia alikuwa mwadilifu na mwaminifu kwa nchi yake, alikuwa na weledi wa kiwango cha juu katika taaluma yake ya kijeshi na alikuwa mtiifu kwa viongozi wake.

Nakutumia wewe Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi salamu zangu za rambirambi kufuatia kifo hiki,” amesema Rais Kikwete na kuongeza: “Aidha, kupitia kwako natuma salamu za pole nyingi kwa familia ya marehemu Makwaia ambao wamempoteza baba na mhimili wa familia. Pia, kupitia kwako, natuma salamu za rambirambi kwa maofisa na wapiganaji wote wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambao wamempoteza ofisa na mpiganaji mwenzao.”

Luteni Kanali (mst) Makwaia alijiunga na Jeshi Machi 24, mwaka 1974, na alilitumikia kwa miaka 23 na miezi tisa kabla ya kustaafu. Alikuwa Msaidizi wa Mpambe wa Rais kati ya mwaka 1978 na 1981 na kuwa Mpambe wa Rais kwa miaka sita hadi 1987. Amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 62.
Imetolewa na: Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu. Dar es Salaam.




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo leo Keko, jijini Dar es salaam, kufuatia kifo cha Luteni Kanali (mst) Adam Hussein Mwandu Makwaia, aliyekuwa Mpambe wa Rais wa kwanza wa Tanzania, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na Rais Ali Hassan Mwinyi. Marehemu amezikwa leo Septemba 6, 2012 katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam.




Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikabidhiwa Tuzo ya Uongozi Bora wa sera ya Kilimo na Chakula toka kwa Bw. Ajay VAshee, Makamu Mwenyekiti wa asasi isiyo ya kiserikali inayohusika na sera za kilimo na chakula na Maliasili n ijulikanayo kama Food, Agriculture and Natural Resources Policy (FANRPAN) katika hoteli ya White Sands jana Septemba 5, 2012. Anayeshuhudia kulia ni Katibu Mtendaji wa FANRPAN) Dkt Lindiwe Sibanda. Tuzo hiyo, ambayo hutolewa kwa kiongozi aliyefanya juhudi kuhakikisha kuwepo kwa sera bora za kilimo na chakula nchini kwake, ilichukuliwa na Malkia Ntombi Indlovukazi wa Swaziland mwaka jana, wakati Rais Hifikepunye Pohamba alitunukiwa mwaka 2010, Rais Armando Emilio Gwebuza mwaka 2009 na Rais wa Malawi, Hayati Bingu Wa Mutharika, aliipokea mwaka 2008.




Waombolezaji wakiuweka kaburini mwili wa aliyekuwa Katibu wa Chama cha Wanajeshi Wastaafu (RAMETEA),Luteni Kanali Mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, `Adam Hussein Makwaiya katika mazishsi yaliyofanyika kwenye makaburi ya Kisutu jijiniDar es salaam Agust 6, 2012 na serikali iliwakilishwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)




Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Naibu Waziri Mkuu wa China, Mhe. Hui Liangyu wakati alipompokea kwenye wuwanja wa ndege wa Dar es salaam Septemba 5, 2012. Mhe. Hui yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)




Nyumba ya asili ya Wahaya aina ya msonge ambayo huwavutia watalii wengi watembeleao mkoa wa Kagera, msonge huu unapatikana maeneo ya camp site yaliyoko kwenye ufukwe wa ziwa Victoria, msonge huu unatumika kwa malazi na mapumziko ya muda, mtu akiwa ndani hawezi kusikia joto.
Kiroyera Tours www.kiroyeratours.com www.kagera.org www.budap.org http://www.facebook.com/pages/Kiroyera-Tours-and-Consulting/171058592931255 http://www.twitter.com/kiroyeratours http://www.youtube.com/user/kiroyeratours P.O. BOX 485 BUKOBA, KAGERA, TANZANIA Tel: +255 28 2220203 Tel: +255-713-526649 or +255-784-568276 FAX: +255 28-2220009 Wasiliana na uongozi wa Kampuni ya utalii ya Kiroyera kwa maelezo zaidi kupitia kwa mawasiliano yafuatayo-




William Rutta, meneja uendeshaji wa kampuni ya utalii ya Kiroyera iliyoko mkoani Kagera akiwa ndani ya hema maalumu ambalo hutumiwa na watalii mbalimbali kwa ajili ya mapumziko, hema hili linapatikana eneo la Camp site lililoko kwenye ufukwe wa ziwa victoria.




Meneja uendeshaji wa kampuni ya utalii mkoani Kagera ya Kiroyera akiwa ndani ya nyumba asili ya wahaya aina ya msonge iliyoko kwenye eneo la Camp site ambayo ni kivutio kikubwa cha watalii, camp site iko kwenye ufukwe wa ziwa Victoria.




Baadhi ya wageni mbalimbali wakiwa wamekipumzisha kwenye ufukwe wa ziwa Victoria lililopo eneo la Camp site linalotaribiwa na kampuni ya utalii ya Kiroyera iliyoko mkoani Kagera.




Mandhari ya ndani ya nyumba za asili ya wahaya aina ya msonge, zinapatikana kwenye aneo la camp site, nyumba hizi huwavutia sana watalii wa ndani na nje ya nchi.




Mandhari ya camp site iliyoko ufukweni mwa ziwa Victoria inayomilikiwa na kampuni ya utalii ya Kiroyera ambayo watalii huitumia kwa ajili ya mapumziko.




Sehemu nyingine ya mandhari ya camp site.




Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji Dr Diodorus Kamala akishikana mkono na mfalme Albert wa II wa falme ya ubelgiji baada ya kuwasilisha hati ya utambulisho. (picha kwa hisani ya ubalozi wa Tanzania nchini Ubelgiji)

No comments:

Post a Comment