Serikali
ya Marekani imetoa msaada wa kuimarisha Mfumo wa Ulinzi baharini wenye
thamani ya dola za Marekani milioni 1 ikiwa ni mafunzo pamoja na vifaa.
Balozi
wa Marekani nchini Tanzania Alfonso Lenhardt ameshiriki katika hafla ya
kukata utepe wa kufungua mafunzo pamoja na msaada huo katika kambi ya
Kigamboni Wanamaji ya Kigamboni ya TPDF jijini Dar es Salaam.
Msaada
huo kwa ujumla utasaidia ushirikiano wa kupata taarifa miongoni mwa
Mamlaka za Bandari, askari wa majini na Jeshi la Wananchi wa Tanzania
ikiwa ni kuongeza usalama majini.
Picha kwa hisani ya Moblog
|
No comments:
Post a Comment